METDO Tanzania

METDO Tanzania
Showing posts with label General News. Show all posts
Showing posts with label General News. Show all posts

Thursday, December 9, 2021

TFRA YAWASISITIZA WAKULIMA KUACHA DHANA POTOFU MATUMIZI YA MBOLEA YA CHUMVICHUMVI MASHAMBANI

Mkurugenzi mtendaji TFRA  Dkt. Stephen Ngailo. akiwa katika picha na Matlida Kasanga afisa mawasiliano na mahusiano wa TFRA na ofisa udhibiti ubora  Cothal Samwel Kwenye mafunzo ya matumizi sahihi ya mbolea ukumbi wa Halmashauri ya Ikungi Singida.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya matumizi sahihi ya mbolea na kanuni bora za kilimo hususani kwa zao la alizeti wakisikiliza mada mbalimbali zikitolewa na wataalamu kutoka TFRA.

Kaimu mkuu wa idara ya kilimo umwagiliaji na ushirika kutoka Halmashauri ya wilaya ya ikungi  Gurisha Msemo akitoa taarifa ya hali ya kilimo katika halmashauri hiyo  wakati wa mafunzo ya matumizi sahihi ya mbolea na kanuni bora za kilimo.

Mkurugenzi wa TFRA Dkt. Stephen Ngailo akielezea malengo ya kutoa elimu ya matumizi sahihi ya mbolea kwa wakulima wa mikoa ya singida , Dodoma na Tabora .


Na Hamis Hussein - Singida 

Mamlaka ya udhibiti wa mbolea nchini TFRA imewataka wakulima kila mmoja kuwa balozi katika kutoa elimu juu ya matumizi sahihi ya mbolea na kanuni bora za kilimo ili kuongeza tija kwao binafsi na taifa kwa ujumla .

zaidi ya wakulima 200 kutoka halmashauri ya ikungi wameshiriki mafunzo ya matumizi ya mbolea yaliyoratibiwa na TFRA ambapo mikoa ya Singida , Dodoma na Tabora imepewa kipaumbele kwa kuwa ndio wazalishaji wakuu wa zao la alizeti .

Akizungumza katika mafunzo yao mkurugenzi Mtendaji wa TFRA Dkt. Stephen Ngailo amesema wao kama mamlaka ya udhibiti wa mbolea kwa kushirikia na wizara ya kilimo na wadau wengine kwa ujumla lengo la kutoa mafunzo hayo ni kuona mnufaika mwa mwisho wa mbolea aidha muuzaji au mkulima apate tija kulinga na mbolea hiyo ili kuongeza uzalishaji .

"Tunatoa sahihi kwa wakulima, afisa kilimo na wadau wengine kama vile wauzaji wa pembejeo  kuhakikisha ile elimu  iwasaidie kutumia mbolea kwa usahihi , lengo ni kuwa wewe unayetumia mbolea shambani unapata faida , kuwe na tofauti  ya tija kwa wewe ulieweka mbole, kuonyesha kuwa kuweka mbolea inalipa ". alisema Dkt. Ngailo 

Dkt. Ngailo ametumia nafasi hiyo kusisitiza juu ya matumizi sahihi ya mbolea na kanuni  bora za kilimo ikiwa ni lengo la serikali katika mkakati wake wa kuhakikisha zao la alizeti linazalishwa kwa wingi ili kupunguza uagizaji wa mafuta toka nje ambapo mikoa ya kimkakati ni singida , dodoma na Tabora.

"Mheshimiwa  waziri mkuu alikuja singida kuhamisisha mkakati kuuu ikiwa nia adhma ya kuongeza wa zao la alizeti ili kujitoshereza katika uzalishaji wa mafuta . kuna mikoa ya kimkakati ,  Kuna mkoa wa dodoma niwashuruku wataalamu wetu wametoa mafunzo kama haya , mkoa wa singida na baadaye ni igunga mkoa wa Tabora na haya ndio maeneo yalichaguliwa kuwa ndio wazilishaji  wakuu wa zao la alizeti" . Ameongeza Dkt. Ngailo.

Kaimu mkuu wa idara ya kilimo ushirika na umwagiliaji kutoka halimshauri ya Ikungi Mkoani singida Gurisha Msemo amesema  hali halisi ya matumizi ya mbolea katika halmashauri hiyo bado ipo chini kwa mpaka sasa 5%  ya wakulima ndio wanautumia mbolea ya chumvichumvi.

" Matumizi ya mbolea katika halmashauri ya ikungi ni 5 % asilimia nyingine wanatumia samadi lakini pia kuna familia au wakulima hawatumii kabisa mbolea kwa hiyo sasa baada ya mafunzo haya tunatumaini watakuwa wamepata elimu ya juu ya matumizi ya mbolea". alisema Gurisha 

Baadhi ta washiriki wa washa hiyo  ilikusudia kutoa elimu ya matumizi sahihi ya mbolea  na kanuni bora zakilimo wamesema dhana potofu iliyopo mtaani ya kuamini kuwa mbolea ya chumvi chumvi inaharibu ardhi ndio sababu kuu ambayo ilikuwa inapelekea wao kutotumia mbolea katika mashamba yao .

Halmashauri ya Ikungi inatarajia kuzalisha tani 72000 za alizeti kutoka kwa wakulima 95000 na kupitia mafunzo hayo tija ya mkulima mmoja mmoja  kama atazingatia kanuni bora za kilimo kama ambavyo mamlaka ya udhibiti wa mbolea nchini TFRA  kiwago za uzalishaji wa mafuta kitakuwa juu sana.

Share:

Sunday, November 28, 2021

SERIKALI YATOA SHILLINGI BILIONI 5.9 UJENZI HOSPITALI YA RUFAA MKOA WA SINGIDA UJENZI WAFIKIA ASILIMIA 70

 Na Hamis Hussein - Singida

Serikali imetoa shilling bilioni 5.9 kwaajili ya kuendeleza ujenzi wa majengo mapya ya  hospitali ya rufaa ya mkoa  wa Singida ambayo itarahisisha huduma mbalimbali afya  ikiwemo upasuaji , tiba za kibingwa na  kupunguza gharama za matibabu kwa  wananchi kufuata huduma hizo  hospitali zingine za mbali  kama  Benjamini Dodoma , au muhimbili.



Waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Dr Doroth Gwajima ametembelea kukagua ujenzi huo akiwa kwenye  ziara ya kikazi  na kuridhishwa ujenzi huyo baada ya  kuona umefikia  asilimia 70  ikiwa ni  awamu ya kwanza ya fedha zilizotengwa .

DR. Gwajima alisema kukamilika kwa hospitali hiyo kutasaidia  kuruhusu wodi za hospitali ya rufaa ambayo majengo yake  yameshachakaa kuhamishiwa kwenye majengo mapya  ambayo yanajengwa  eneo la mandewa  pamoja na  kurahisisha huduma za afya kwa jamii.

“Kutoka singida nimekuja ziara fupi kuangalia maendeleo ya ujenzi wa hospitali mpya . iliyopo sasahivi ile hospitali iliyopo katikati ya mji imebanwa majengo yake yamepitwa na wakati   , umefika wakati wa kuongeza  kasi ili huduma za rufaa zihamie hospitali mpya ya mandewa  ambayo ni ya kisasa. Serikali  haiko nyuma imeshatenga  na kuleta shilingi bilioni 5.9 . Jengo lote linavyooneka hapa  ni kubwa  kuna sehemu ya upasuaji , maabara na wodi mbalimbali . hii itaruhusu wodi za kule zilizobanana kuhamia huku na  majengo ya hospitali ile yatumike na halmashauri  na hospitali hii itakapo kamilika itatoa nafuu kwa hospitali ya Benjamini mkapa pamoja na gharama za kwenda kutibiwa mbali ”. amesema Dr. Doroth Gwajima.


Wakati akikagua ujenzi wa majengo mapya ya hospitali Waziri Doroth Gwajima ametoa maagizo kwa viongozi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa singida pamoja na watendaji wengine kutoka serikalini kuundwa kwa kamati mbalimbali ikiwemo kamati ya fedha ,  pamoja na dawa ili kuweza kubadilisha na kumaliza matatizo ambayo yamekuwa sugu hususani dawa ambalo limekuwa kama wimbo wa taifa .

Wapo watu wajanja wanaofanya dawa hizi zisifike kwa wagonjwa, utafiti umefanywa  na nyinyi wenyewe, kamati ya dawa iundwe  sio ile kubwa  hii  ni ndogo ya kuhakikisha pale dirishani kwa mfamasia ni wangapi wamepata dawa zote, wangapi wamekosa , lakini katika mifumo yetu ya fedha viko vitengo vinatumia   vifaa tiba vibaya rasilimali  lakini ukiangalia wateja wangapi wamechangia hakuna takwimu , tunataka kamati ya fedha itakayosimamia hayo.

Aliongeza kutaja kamati nyingine ya damu itakayosisimamia uchangiaji wa damu   

Mfumo wa damu salama wananchi wanalalamika   watu wanakosa damu wanashurutishwa wachangie kwanza ndipo wapewe damu nimefika kwenye vituo malalamiko yapo sahihi ni kikundi cha watu wachache wajanja wajanja , lakini wananchi suala lingine  na ninyi hamchangii damu  nimeona hapa kuanzia julai mpaka septemba   asilimia 27 %  ya chupa zilizotakiwa kupatikana asilimi ni ndogo sana lakini je tunashirikishaje mifumo ya wadau waliopo kwenye mkoa huu ili waweze kuhamasisha wananchi kuchagia damu . kamati ya damu iuundwe ili kusimamia hili.




Akizungmza kwa niaba ya  mkuu wa mkoa  , Mkuu wa wilaya Mhandisi Pascas Mulagiri amethibitisha kupokea shilingi bilioni 5.9 ambapo ameanisha kuwa fedha hizo zinatumika katika ujenzi wa hospitali ya rufaa ya mkoa

“Sisi ni miongoni mwa wanufaika wakubwa mipango ya afya singida tayari tumepokea  bilioni 5.9 katika uendelezaji wa hospitali ya rufaa ya mkoa singida  na ujenzi wake unaendelea na haya  lakini tuna pesa  Bilioni 5.3 kwaajili ya ujenzi wa majengo mbalimbali ambayo yataanza hivi karibuni  haya yakifanyika itakuwa ni mapinduzi makubwa sana katika sekta ya afya hospitali yetu inakuwa  ya rufaa na ukiwa na hospitali hiyo itasaidia kuwa huduma nzuri na kuwa madaktari bingwa” . alisema Mhandisi Mulagiri

Kuhusu changamoto ambayo waliyokuwa nayo halmashauri kukosa hospitali ya wilaya mkuu huyo wa wilaya wa Singida Mhandisi Mulagiri amesema walikosa huduma nyingi ikiwemo madaktari bingwa ngazi ya wilaya.

Suala la kutokuwepo kwa hospitali ya wilaya lilituaathiri  kwa kiasi Fulani ukiangalia katika sekta ya aafya mgawanyo wa huduma za afya , madawa , wahudumu waafya unaendana na kituo hivyo tulikuwa tunakosa mgawanyo wa dawa  na huduma zingine hivyo ujio wa hii nafasi ya kutimia majengo ya hospitali ya general utawasogezea wananchi huduma kuwa karibu.

Mkandarasi wa hospitali ya rufaa ya mkoa  kutoka kambuni ya MCB Justine Kyando amesema kwa sasa ujenzi huo umefikia asilimia 70 huku akitoa makadirio ya kumalizika kwa ujenzi huo ili hospitali inaze kuanza kutumika

“Tunashukuru ujio wa mheshimiwa waziri . kwa sasa tumefikia asilimia 70 , kwa sahivi kwa sababu wanataka kutuongezea mkataba  kumaliza hadi ghorofa  tunaweza inaweza kutumia mwaka mmoja na nusu kwa maana hadi mwaka 2023 tunaweza kumaliza ianze kutumika.”


Share:

Saturday, November 27, 2021

ZAIDI YA WAGONJWA 1141 WA VIKOPE WATIBIWA MKOANI SINGIDA

 

Na Hamis Hussein-Singida

Jumla ya kaya 212,952 kati ya walengwa 212812 sawa na asilimia 100.1 % zimefikiwa na mradi wa vikope kutoka shirika la Hellen Keller International ambapo shirika hilo limezitembelea moja kwa moja kaya hizo kuwabaini  wagonjwa wa vikope kisha kuwapatia matibabu ikiwa ni lengo la  kutokomeza ungonjwa huo kwa mkoa wa singida kwani  ni miongoni mwa magonjwa  makuu matano ambayo hayapewi kipaumbele.

Baadhi ya washiriki wa kikao cha kufunga mradi wa vikope mkoani singida wakisikiliza na kujadiliana mambo mbalimbali.

Mradi huyo uliodumu kwa miaka mitatu tangu kuanzishwa kwake 2019 ni miongoni mwa jitihada za wizara ya afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto kupitia mpango wa taifa wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele NTDCP kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ulilenga kupunguza au kuufuta kabisa ungonjwa wa trakoma au vikope ambapo mikoa 20 ikiwemo mkoa wa singida ndiko utekelezaji wake unafanyika ikiwa mradi ambao  unakotekelezwa kupitia shirika la Hellen Keller International kutoka nchini marekani.

 

Mganga mkuu wa mkoa wa Singida Dr. Viktorina Ludovick amelipongeza shirika hilo kwa namna ambayo limeisaidia serikali na jamii katika kutokomeza  ungonjwa wa trakoma alipokuwa akizungumza na washiriki wa kikao cha ufungaji wa mradi huo kumwakilisha katibu tawala wa mkoa.

 

 “Kwa kushirikia na timu zetu za mikoa na halmashauri pamoja na mdau wetu Hellen Keller International tumeweza kutekeleza mpango wa kutokomeza vikope kwa Halmashauri zeto sita  Manyoni , Itigi Ikungi Mkalama Singida Vijijini na Singida Manispaa  jumla 212952 kati ya walengwa 212812 sawa na 100.1% . Hapa tunaona uhitaji ulikuwa mkubwa na tumetekelea mpaka tumevuka lengo”.  amesema Dr Ludovick 

 

Mganga Mkuu mkoa wa singida Dr. Viktorina Ludovick akizungumza na washiriki wa kikao cha kufunga  mradi wa vikope kutoka shirika la HKI katika ukumbi wa Aqua Vitae Resort Singida.


Ameyataja mafanikio mengine kuwa ni pamoja na kutoa mafunzo ya kubaini na kutibu wagonjwa wa vikope wataalamu wawili ngazi ya mkoa, wataalamu 13 ngazi ya halmashauri, wahudumu wa afya 1308 ngazi ya kata na vijiji pamoja na wahudumu afya 2851 ngazi ya jamii.

Dr Ludovick ameongeza kuyataja mafanikio kupitia mradi wa vikopte kutoka shirika La Hellen Keller Interentaional kuwa wagonjwa 1141 wa vikope ambao walikuwa na tatizo hilo aidha  bila kujua au  kukosa sehemu ya kupata msaada walipata huduma.

 

Meneja mradi wa trakoma kutoka shirika la Hellen Keller International (HKI) Athuman Tawakal amesema lengo kubwa la kuleta mradi huo ilitokana na takwimu zilizoonyesha uhitaji wa huduma hizo kwa waathirika wa ugonjwa wa vikope.

“ Tumekuja katika maeneo haya  baaada ya kupata takwimu kutoka wizara ya afya kuonyesha ukubwa wa ugonjwa huu wa trakoma  katika maeneo haya na tuliagizwa na wizara kupitia mpango wa kutokomeza magonjwa yasiopewa kipaumbele ili kusaidia halmashauri  na mkoa  katika kuwatafuta wagonjwa na kuwapatia matibabu na tumeweza kufanikiwa . tumeweza kuwasidia watanzania zaidi ya 1100 kuwapatia matibubu na tumekuwa tukifanya ufutiliaji”.

 

Meneja mradi kutoka shirika la HKI Athuman Tawakal Akizungmza na washiriki wakati wa kufunga mradi wa vikope mkoani singida tangu ulipoanzishwa 2019


Dr. Julius Nyenje mratibu wa magonjwa yasiopewa kipaumbele kutoka wilaya ya Mkalama amelishukuru shirika la HKI kwa kuwajengea uwezo wa mapambano dhidi ya ungonjwa wa trakoma.

“Trakoma au ungonjwa wa vikope ilikuwa moja ya  magonjwa  makuu matano ambayo yalikuwa hayapewi kipaumbele na HKI mmechukua nafasi kubwa sana  na jamii yetu imepata huduma njema .tunawashukuru sana”. alisema dr. Julius mratibu wa magonjwa yasiopewa kipaumbele kutoka wilaya ya Mkalama.

Mratibu wa magonjwa ambayo yalikuwa hayapewi kipaumbele kutoka wilaya ya Mkalama Dr. Julius Nyenje akitoa shukrani kwa shirika la Hellen Keller International wakati wa kufunga mradi wa vikope .


Fatuma Jumapili, Elizabeth Wilbroad na Shabani Hamisi  ni Baadhi ya wanufaika wa mradi wa vikope kutoka shirika la HKI wamesema huduma ya matibabu ya vikope imewasaidia sanaa kurejesha uwezo wao wa kuona na kulipongeza shirika hilo kwa namna lilivyotekeleza mradi huo.

 

Dr Upendo Mwakabalile mratibu wa huduma za macho mkoa wa singida amewasisitiza wataalamu wengine waliopata mafunzo ya namna ya kuwahudumia  wagonjwa wa vikope kutunza takwimu ili ziweze kusaidia baaadae na kuwataka elimu waliopata kuifanyia kazi kwa watu wengine wenye uhitaji.


“Naomba kila mtu azingatie sana kwa sababu pasipotakwimu kazi yetu tulioifanya kwa miaka mitatu itakuwa imepotea, kwahiyo takwimu inakuwa ni ushahidi. hawa wahudumu 13 tuliopewa mafunzo tusipofanyia kazi hiyo elimu yetu itakuwa sawa na bure”.  
amesema Dr. upendo

Mradi wa vipoke mkoani singida umetekelezwa na shirika la Hellen Keller International ikiwa ni miongoni mwa jitihada za wizara ya afya  maendeleo ya jamii  jinsia wazee na watoto kupitia mpango wa  taifa wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele NTDCP kwa kushirikiana na timu za mikoa na wilaya  na wadau mbalimbali ambapo mradi umetekelezwa kwenye wilaya sita ambazo  ni manyoni , itigi , ikungi ,mkalama , singida manispaa na singida  vijijini  ambazo ziliathiliwa na ungojwa wa vipoke kwa kiwango kikubwa .





 

 

Share:

Thursday, November 25, 2021

FPTC YATOA MAFUNZO UTETEZI WA HAKI ZA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM


Na, Nathaniel Limu - Singida 

KANISA  la Pentekoste Tanzania (FPCT) Singida mjini kati, kupitia kitengo chake cha Singida,Town Centre  Church (STCC),  limetoa mafunzo juu ya mpango kazi wa utetezi wa haki za watoto wenye mahitaji maalum, ili kuwajengea uwezo wajumbe wa mradi wa Elimu jumuishi, waweze kutekeleza  majukumu yao kwa ufanisi.


Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na shirika la  Singida,Town Centre  Church (STCC), yalitolewa na shirika la International Aid services (IAS) la Dermark kwa njia ya  mtandao yaani Zoom.

Mkurugenzi wa shirika la IAS, Jovben Madsen, amesema wameamua kutoa mafunzo hayo, kwa watu wenye uwezo wa kutoa sauti, ili waweze kupaza sauti kwa niaba ya watu wasio na sauti wweze kupata haki zao za msingi.


watoto na hata baadhi ya watu wazima,bado  wanaendelea kudhulumiwa haki zao.Watu wazima wameathirika kiuchumi.Pia wanafanyiwa  vitendo vya unyanyasaji mbavyo vipo kinyume na haki za kibinadamu. Mbaya zaidi  hawana uwezo wa  kutetea haki zao. Amefafanua mkurugenzi wa IAS Madsen

Mkurugenzi huyo ameongeza  kwamba watu wasio na uwezo wa kujisemea au kutetea haki zao, wapo sehemu mbalimbali duniani. Akiijengea nguvu hoja yake hiyo, alinukuu kifungu kwenye kitabu kitakatifu cha Biblia Methali 31-9 (kifungu cha nane na tisa). Nukuu inasema “Fumbua kinywa chako kwa ajili yake aliye bubu, uwatetee watu wote walioachwa peke yao”.

Mkurugenzi Madsen, amefarijika kwa kitendo cha kiongozi wa serikali ngazi ya juu mkoani Singida,Fatuma Malenga, kuwa ni miongoni  mwa viongozi wa mradi wa elimu jumuishi na mchango wake utakuwa na tija zaidi.



Katika hatua nyingine, mratibu wa mipango shirika la IAS Katja, amesema katika kitabu kitakatifu cha Biblia, nacho kimeainisha kwamba baadhi ya watu wenye madaraka, nao wanatumia nafasi  hizo, kunyanyasa watu wasio na sauti.  Kwani katika biblia takatifu  Isaya 3 mstari wa 14, nukuu yake inasema “Bwana ataingia katika kuwahukumu wazee na watu wake na wakuu wao, ‘ninyi ndio mliokula shamba la mzabibu, vitu mlivyowateka maskini, vii ndani ya nyumba zenu”. 

Kuhusu changamoto zinazojitokeza,Katja ameshauri mjumbe yeyote wa mradi endapo atakabiliwa na changamoto ya aina yo yote, asiikabili peke yake,ashirikishe wenzake.

Wakati huo huo,mjumbe wa shirika la walemavu SHIVYAWATA manispaa ya Singida,Idd Hassan,amesema mafunzo hayo yalikuwa mazuri, na kwa vyo vyote yataleta matokeo chanya na kutumia fursa hiyo kuiomba serikali ngazi mbalimbali kuangalia uwezekano wa kutunga sheria ndogo ndogo, zitakazowadhibiti wazazi wanaoficha watoto wao wenye ulemavu kupata haki zao.


“Naziomba  mamlaka na wadau wengine  kusaidia kujenga miundo mbinu rafiki  katika maeneo ya shule,vyuo na sehemu zingine.Ili kuwaondolea usumbufu/kero watu wenye ulemavu.Na vile vile serikali iangalie uwezekano wa kumaliza uhaba mkubwa wa walimu wa viziwi”,alisema Hassan.


Share:

Thursday, July 30, 2020

WAZIRI HASUNGA AWEKA BAYANA MAMBO YALIYOSISITIZWA NA HAYATI BENJAMI MKAPA KWENYE SEKTA YA KILIMO

Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye maonesho ya kilimo yaliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo-TARI SERIAN Jijini Arusha
Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga akikagua shamba la maharage wakati alipotembelea Jijini Arusha kufungua maonesho ya kilimo yaliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo-TARI SERIAN Jijini Arusha
Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga akikagua shamba la mahindi yaliyozalishwa kwa kutumia mbolea ya Minjingu wakati alipotembelea Jijini Arusha kufungua maonesho ya kilimo yaliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo-TARI SERIAN Jijini Arusha
Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga akikagua bidhaa mbalimbali za maharage wakati alipotembelea Jijini Arusha kufungua maonesho ya kilimo yaliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo-TARI SERIAN Jijini Arusha
Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga akikagua mazao mbalimbali ya mizizi wakati alipotembelea Jijini Arusha kufungua maonesho ya kilimo yaliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo-TARI SERIAN Jijini Arusha

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Arusha

Rais wa awamu ya tatu wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Benjamini Mkapa wakati wa utawala wake aliainisha kuwa nia na lengo kuu la sekta ya kilimo ni pamoja na kuhakikisha wakulima wa Tanzania wanapata elimu na ujuzi wa kutosha wa vitendo, hivyo Wizara ya Kilimo inatakiwa kujizatiti kikamilifu kuwasaidia wakulima kuishi katika uchumi wa viwanda.

Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga amebainisha hayo hivi karibuni wakati akizungumza kwenye maonesho ya kilimo yaliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo-TARI SERIAN Jijini Arusha na kuongeza kuwa Mkapa alieleza dhamira ya serikali kuhakikisha kuwa inafikia uchumi wa kati na wa viwanda kwa kuwa na uwekezaji mkubwa katika sekta ya kilimo.

“Hayati Rais Mkapa wakati wa utawala wake alilisisitiza kuwa nchi yoyote ili iwe na Usalama na Amani ni lazima wananchi wawe wamejitosheleza kwa chakula endapo kutakuwa na upungufu wa chakula ni dhahiri kuwa nchi haiwezi kuwa na utulivu wa kisiasa na kimaendeleo’’ Alisema

Pia Hayati Mkapa alipiga vita kwa nguvu kubwa umasikini ambapo alianzisha kauli mbiu ya MTAJI WA MASIKINI NI NGUVU ZAKE MWENYEWE ikilenga kuhamasisha wananchi kufanya kazi kwa bidii ili kuchagiza shughuli za maendeleo.

Kadhalika Hayati Benjamin Mkapa alisisitiza ulazima wa maafisa Ugani kufanya kazi mashambani kwa wakulima badala ya kuishi mjini pekee kwani kwa kufanya hivyo watawasaidia wananchi kunufaika na kilimo kwa kuwa na tija kubwa katika uzalishaji hivyo kuwa na kilimo cha kibiashara.

Waziri Hasunga amesema kuwa Hayati Rais Mkapa alikuwa muumini wa teknolojia bora za kilimo hivyo aliitaka Wizara ya Kilimo kuhakikisha kuwa inatumia teknolojia na zana bora za kilimo ili kuhakikisha kuwa malighafi zinazotokana na mazao ya kilimo zinaendelea kuzalishwa kwa wingi.

Kadhalika, Hayati Mkapa alisema kuwa kilimo bila utaalamu hakiwezi kumkomboa mkulima hivyo aliagiza Taasisi za utafiti wa Kilimo na vyuo vya mafunzo ya ufundi kuhakikisha kuwa vinaendeleza juhudi za kuimarisha elimu kwa wananchi na wakulima ili kuwa na taifa bora lenye wakulima wazuri.

MWISHO

Share:

Thursday, December 6, 2018

Benki ya KCB yawapiga msasa wafanyabiashara Jijini Mwanza

Meneja wa Mauzo ya Kibiashara wa Benki ya KCB, Lightness May akizungumza kwenye kwenye semina kwa wadogo na wa kati waliokutanishwa na benki hiyo kupitia KCB Biashara Club. Semina hiyo ilifanyika Novemba 29, 2018 Gold Crest Jijini Mwanza na kuhudhuriwa na washiriki zaidi ya 200 lengo likiwa ni kuwapa mafunzo kuhusu muhusu usimamizi wa fedha, uendeshaji wa biashara pamoja na sheria za kodi.
Share:

Tuesday, December 4, 2018

Uzinduzi wa Kampeni ya Kupinga Ukatili wa Kijinsia wilayani Tarime

Mkurugenzi wa Shirika la kutetea haki za wasichana na wanawake KIVULINI la Jijini Mwanza, Yassin Ally, akizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni ya kutokomeza ukatili wa Kijinsia katika wilaya ya Tarime mkoani Mara. Uzinduzi huo ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango wa Kitaifa wa Kutokomeza Ukatili wa Kijinsia kwa Watoto na Wanawake katika kipindi cha mwaka 2017/22.
Share:

Benki ya CRDB yapata Daktari mpya

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Meneja Biashara wa Benki ya CRDB tawi la Mwanza, Danford Muyango (pichani) ametunukiwa Shahada ya Uzamivu (PhD) ya Chuo Kikuu cha Dodoma “UDOM” na hivyo kuwa daktari mpya kwa sasa anayefanya kazi na benki hiyo.
Share:

Friday, November 30, 2018

Majaliwa akasirika wafanyabiashara Katoro kuchangishwa fedha

Na George Binagi-GB Pazzo

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa, Novemba 30, 2018 amehitimisha ziara yake ya siku nne mkoani Geita kwa kuzungumza na wakazi wa Katoro akiwa njiani kuelekea uwanja wa ndege Chato ambapo pamoja na mambo mengine alikasirishwa kusikia wafanyabiashara wamechangishwa fedha kwa ajili ya mafuta ya ukarabati wa barabara za mitaa.
Share:

Waziri Mkuu awatoa hofu wafugaji wilayani Bukombe

Novemba 29, 2018 Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa alifanya ziara ya kikazi wilayani Bukombe ambapo aliweka jiwe la msingi kwenye ukarabati wa Kituo cha Afya Ushirombo na baadae kuzungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa stendi Ushirombo.
Share:

Thursday, November 29, 2018

Wednesday, November 28, 2018

Majaliwa aanza na wanaotuhumiwa kutafuna mabilioni ya fedha wilayani Nyang'hwale

Na George Binagi-GB Pazzo
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ameagiza watumishi wote waliohusika na ubadhilifu wa zaidi ya shilingi bilioni tatu katika Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale mkoani Geita kukamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Share:

Tuesday, November 27, 2018

RC Geita mbele ya Waziri Mkuu “nafuu tukikagua tukute mtu kajinyonga”

Mkuu wa Mkoa Geita, Mhandisi Robert Gabriel (katikati) akitoa salamu za shukrani na kumkaribisha Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (kushoto) aliyeanza ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani Geita jana, kulia ni mbunge wa Chato na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Medard Kalemani.
Share:

Sunday, November 25, 2018

JAFO AWAPONGEZA VIONGOZI MBEYA KWA USIMAMIZI MZURI WA MIRADI

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya  Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo akimsikiliza mtaalum katika ukaguzi wa miradi ya maendeleo Mbeya.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya  Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo akiwa na viongozi mbalimbali katika ukaguzi wa miradi ya maendeleo Mbeya.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya  Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo akizungumza mara baada ya kukagua miradi ya maendeleo Mbeya.
 Wananchi wa Mbeya wakiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya  Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya  Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo akizungumza mara baada ya kukagua miradi ya maendeleo Mbeya.
Ujenzi majengo mbalimbali ukiendelea Mbeya
.................................................................................................................

Waziri wa Nchi, Ofisi ya  Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila na viongozi wa Wilaya ya Mbeya kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo.  


Jafo ametoa pongezi hizo Leo hii alipotembelea mkoani huo kukagua miradi ya maendeleo iliyo chini ya Ofisi ya Rais,TAMISEMI.  


katika ziara hiyo, Waziri Jafo ametembelea miradi ya elimu pamoja na miradi ya afya ikiwemo shule ya msingi Azimio inayofanyiwa ukarabati mkubwa pamoja na Kituo  cha afya Uyunga kinachojengewa miundombiu mbalimbali baada ya kupokea pesa ya ukarabati Sh.Milioni 400 kutoka serikali.  


Waziri Jafo amefurahishwa kwa ubora wa majengo yanayojengwa huku akiwataka viongozi hao kuendelea kusimamia ubora wa majengo hayo hadi yatakapokamilika. 


Aidha, Waziri Jafo amewapongeza viongozi wa Chama cha Mapinduzi(CCM) mkoani humo kwa kushiriki pia kusimamia kwa karibu miradi hiyo kwa maslahi mapana ya wananchi.



Share:
Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com