Na, Nathaniel Limu - Singida
KANISA la Pentekoste Tanzania (FPCT) Singida mjini kati, kupitia kitengo chake cha Singida,Town Centre Church (STCC), limetoa mafunzo juu ya mpango kazi wa utetezi wa haki za watoto wenye mahitaji maalum, ili kuwajengea uwezo wajumbe wa mradi wa Elimu jumuishi, waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na shirika la Singida,Town Centre Church (STCC), yalitolewa na shirika la International Aid services (IAS) la Dermark kwa njia ya mtandao yaani Zoom.
Mkurugenzi wa shirika la IAS, Jovben
Madsen, amesema wameamua kutoa mafunzo hayo, kwa watu wenye uwezo wa kutoa
sauti, ili waweze kupaza sauti kwa niaba ya watu wasio na sauti wweze kupata
haki zao za msingi.
watoto na hata baadhi ya watu
wazima,bado wanaendelea kudhulumiwa haki
zao.Watu wazima wameathirika kiuchumi.Pia wanafanyiwa vitendo vya unyanyasaji mbavyo vipo kinyume
na haki za kibinadamu. Mbaya zaidi
hawana uwezo wa kutetea haki zao. Amefafanua mkurugenzi wa IAS
Madsen
Mkurugenzi huyo ameongeza kwamba watu wasio na uwezo wa kujisemea au
kutetea haki zao, wapo sehemu mbalimbali duniani. Akiijengea nguvu hoja yake
hiyo, alinukuu kifungu kwenye kitabu kitakatifu cha Biblia Methali 31-9
(kifungu cha nane na tisa). Nukuu inasema “Fumbua kinywa chako kwa ajili yake aliye
bubu, uwatetee watu wote walioachwa peke yao”.
Mkurugenzi Madsen, amefarijika kwa kitendo cha kiongozi wa serikali ngazi ya juu mkoani Singida,Fatuma Malenga, kuwa ni miongoni mwa viongozi wa mradi wa elimu jumuishi na mchango wake utakuwa na tija zaidi.
Katika hatua nyingine, mratibu wa
mipango shirika la IAS Katja, amesema katika kitabu kitakatifu cha Biblia,
nacho kimeainisha kwamba baadhi ya watu wenye madaraka, nao wanatumia
nafasi hizo, kunyanyasa watu wasio na
sauti. Kwani katika biblia takatifu Isaya 3 mstari wa 14, nukuu yake inasema “Bwana
ataingia katika kuwahukumu wazee na watu wake na wakuu wao, ‘ninyi ndio
mliokula shamba la mzabibu, vitu mlivyowateka maskini, vii ndani ya nyumba zenu”.
Kuhusu changamoto zinazojitokeza,Katja
ameshauri mjumbe yeyote wa mradi endapo atakabiliwa na changamoto ya aina yo
yote, asiikabili peke yake,ashirikishe wenzake.
Wakati huo huo,mjumbe wa shirika la
walemavu SHIVYAWATA manispaa ya Singida,Idd Hassan,amesema mafunzo hayo
yalikuwa mazuri, na kwa vyo vyote yataleta matokeo chanya na kutumia fursa hiyo
kuiomba serikali ngazi mbalimbali kuangalia uwezekano wa kutunga sheria ndogo
ndogo, zitakazowadhibiti wazazi wanaoficha watoto wao wenye ulemavu kupata haki
zao.
“Naziomba mamlaka na wadau wengine kusaidia kujenga miundo mbinu rafiki katika maeneo ya shule,vyuo na sehemu
zingine.Ili kuwaondolea usumbufu/kero watu wenye ulemavu.Na vile vile serikali
iangalie uwezekano wa kumaliza uhaba mkubwa wa walimu wa viziwi”,alisema Hassan.
0 comments:
Post a Comment