Waziri Mkuu
Mhe. Kassim Majaliwa ameagiza watumishi wote waliohusika na ubadhilifu wa zaidi
ya shilingi bilioni tatu katika Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale mkoani
Geita kukamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Aidha Mhe.
Majaliwa ameagiza Mkaguzi wa Ndani wa Halmashauri hiyo, Gavana Mateso akamatwe
kwa kushindwa kutoa taarifa kwa mamlaka husika baada ya kuwepo harufu ya
ubadhilifu wa fedha za maendeleo ikiwemo mradi wa maji Nyamtukuza ambao tangu
mwaka 2014 hadi sasa haujakamilika.
Baadhi ya fedha
za miradi ambayo inaelezwa kuwa na harufu ya ubadhilifu ni pamoja na shilingi
bilioni 1.2 za ujenzi wa ofisi ya halmashauri ya Nyang’hwale, shilingi milioni
400 za ukarabati wa Kituo cha Afya Nyang’hwale, shilingi milioni 611.230 za
mradi wa maji, shilingi milioni 536.119 za mpango wa malipo kulingana na huduma
(EP4R), shilingi milioni 125.914 za ushuru wa huduma, milioni 109 za mfuko wa
barabara na shilingi milioni 31 za ujenzi wa ofisi ya mbunge.
Tayari watumishi
saba akiwemo aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Nyang’hwale, Carlos
Gwamagobe wamekamatwa kwa ajili ya uchunguzi kuhusiana na ubadhilifu huo. Mhe.
Majaliwa yuko mkoani Geita kwa ziara ya kikazi ya siku nne aliyoianza juzi Novemba
27, 2018.
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na wakazi wa Nyang'hwale kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Sabasaba.
Baadhi ya wakazi wa Nyang'hwale wakimsikiliza Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (hayuko pichani).
Tazama Video hapa chini
0 comments:
Post a Comment