Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo akiwa na viongozi mbalimbali katika ukaguzi wa miradi ya maendeleo Mbeya.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo akizungumza mara baada ya kukagua miradi ya maendeleo Mbeya.
Wananchi wa Mbeya wakiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo akizungumza mara baada ya kukagua miradi ya maendeleo Mbeya.
Ujenzi majengo mbalimbali ukiendelea Mbeya
.................................................................................................................
Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo amempongeza
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila na viongozi wa Wilaya ya Mbeya kwa
usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo.
Jafo ametoa pongezi
hizo Leo hii alipotembelea mkoani huo kukagua miradi ya maendeleo iliyo chini
ya Ofisi ya Rais,TAMISEMI.
katika ziara hiyo,
Waziri Jafo ametembelea miradi ya elimu pamoja na miradi ya afya ikiwemo shule
ya msingi Azimio inayofanyiwa ukarabati mkubwa pamoja na Kituo cha afya
Uyunga kinachojengewa miundombiu mbalimbali baada ya kupokea pesa ya ukarabati
Sh.Milioni 400 kutoka serikali.
Waziri Jafo
amefurahishwa kwa ubora wa majengo yanayojengwa huku akiwataka viongozi hao
kuendelea kusimamia ubora wa majengo hayo hadi yatakapokamilika.
Aidha, Waziri Jafo
amewapongeza viongozi wa Chama cha Mapinduzi(CCM) mkoani humo kwa kushiriki pia
kusimamia kwa karibu miradi hiyo kwa maslahi mapana ya wananchi.
0 comments:
Post a Comment