METDO Tanzania

METDO Tanzania

Sunday, November 28, 2021

SERIKALI YATOA SHILLINGI BILIONI 5.9 UJENZI HOSPITALI YA RUFAA MKOA WA SINGIDA UJENZI WAFIKIA ASILIMIA 70

 Na Hamis Hussein - Singida

Serikali imetoa shilling bilioni 5.9 kwaajili ya kuendeleza ujenzi wa majengo mapya ya  hospitali ya rufaa ya mkoa  wa Singida ambayo itarahisisha huduma mbalimbali afya  ikiwemo upasuaji , tiba za kibingwa na  kupunguza gharama za matibabu kwa  wananchi kufuata huduma hizo  hospitali zingine za mbali  kama  Benjamini Dodoma , au muhimbili.



Waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Dr Doroth Gwajima ametembelea kukagua ujenzi huo akiwa kwenye  ziara ya kikazi  na kuridhishwa ujenzi huyo baada ya  kuona umefikia  asilimia 70  ikiwa ni  awamu ya kwanza ya fedha zilizotengwa .

DR. Gwajima alisema kukamilika kwa hospitali hiyo kutasaidia  kuruhusu wodi za hospitali ya rufaa ambayo majengo yake  yameshachakaa kuhamishiwa kwenye majengo mapya  ambayo yanajengwa  eneo la mandewa  pamoja na  kurahisisha huduma za afya kwa jamii.

“Kutoka singida nimekuja ziara fupi kuangalia maendeleo ya ujenzi wa hospitali mpya . iliyopo sasahivi ile hospitali iliyopo katikati ya mji imebanwa majengo yake yamepitwa na wakati   , umefika wakati wa kuongeza  kasi ili huduma za rufaa zihamie hospitali mpya ya mandewa  ambayo ni ya kisasa. Serikali  haiko nyuma imeshatenga  na kuleta shilingi bilioni 5.9 . Jengo lote linavyooneka hapa  ni kubwa  kuna sehemu ya upasuaji , maabara na wodi mbalimbali . hii itaruhusu wodi za kule zilizobanana kuhamia huku na  majengo ya hospitali ile yatumike na halmashauri  na hospitali hii itakapo kamilika itatoa nafuu kwa hospitali ya Benjamini mkapa pamoja na gharama za kwenda kutibiwa mbali ”. amesema Dr. Doroth Gwajima.


Wakati akikagua ujenzi wa majengo mapya ya hospitali Waziri Doroth Gwajima ametoa maagizo kwa viongozi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa singida pamoja na watendaji wengine kutoka serikalini kuundwa kwa kamati mbalimbali ikiwemo kamati ya fedha ,  pamoja na dawa ili kuweza kubadilisha na kumaliza matatizo ambayo yamekuwa sugu hususani dawa ambalo limekuwa kama wimbo wa taifa .

Wapo watu wajanja wanaofanya dawa hizi zisifike kwa wagonjwa, utafiti umefanywa  na nyinyi wenyewe, kamati ya dawa iundwe  sio ile kubwa  hii  ni ndogo ya kuhakikisha pale dirishani kwa mfamasia ni wangapi wamepata dawa zote, wangapi wamekosa , lakini katika mifumo yetu ya fedha viko vitengo vinatumia   vifaa tiba vibaya rasilimali  lakini ukiangalia wateja wangapi wamechangia hakuna takwimu , tunataka kamati ya fedha itakayosimamia hayo.

Aliongeza kutaja kamati nyingine ya damu itakayosisimamia uchangiaji wa damu   

Mfumo wa damu salama wananchi wanalalamika   watu wanakosa damu wanashurutishwa wachangie kwanza ndipo wapewe damu nimefika kwenye vituo malalamiko yapo sahihi ni kikundi cha watu wachache wajanja wajanja , lakini wananchi suala lingine  na ninyi hamchangii damu  nimeona hapa kuanzia julai mpaka septemba   asilimia 27 %  ya chupa zilizotakiwa kupatikana asilimi ni ndogo sana lakini je tunashirikishaje mifumo ya wadau waliopo kwenye mkoa huu ili waweze kuhamasisha wananchi kuchagia damu . kamati ya damu iuundwe ili kusimamia hili.




Akizungmza kwa niaba ya  mkuu wa mkoa  , Mkuu wa wilaya Mhandisi Pascas Mulagiri amethibitisha kupokea shilingi bilioni 5.9 ambapo ameanisha kuwa fedha hizo zinatumika katika ujenzi wa hospitali ya rufaa ya mkoa

“Sisi ni miongoni mwa wanufaika wakubwa mipango ya afya singida tayari tumepokea  bilioni 5.9 katika uendelezaji wa hospitali ya rufaa ya mkoa singida  na ujenzi wake unaendelea na haya  lakini tuna pesa  Bilioni 5.3 kwaajili ya ujenzi wa majengo mbalimbali ambayo yataanza hivi karibuni  haya yakifanyika itakuwa ni mapinduzi makubwa sana katika sekta ya afya hospitali yetu inakuwa  ya rufaa na ukiwa na hospitali hiyo itasaidia kuwa huduma nzuri na kuwa madaktari bingwa” . alisema Mhandisi Mulagiri

Kuhusu changamoto ambayo waliyokuwa nayo halmashauri kukosa hospitali ya wilaya mkuu huyo wa wilaya wa Singida Mhandisi Mulagiri amesema walikosa huduma nyingi ikiwemo madaktari bingwa ngazi ya wilaya.

Suala la kutokuwepo kwa hospitali ya wilaya lilituaathiri  kwa kiasi Fulani ukiangalia katika sekta ya aafya mgawanyo wa huduma za afya , madawa , wahudumu waafya unaendana na kituo hivyo tulikuwa tunakosa mgawanyo wa dawa  na huduma zingine hivyo ujio wa hii nafasi ya kutimia majengo ya hospitali ya general utawasogezea wananchi huduma kuwa karibu.

Mkandarasi wa hospitali ya rufaa ya mkoa  kutoka kambuni ya MCB Justine Kyando amesema kwa sasa ujenzi huo umefikia asilimia 70 huku akitoa makadirio ya kumalizika kwa ujenzi huo ili hospitali inaze kuanza kutumika

“Tunashukuru ujio wa mheshimiwa waziri . kwa sasa tumefikia asilimia 70 , kwa sahivi kwa sababu wanataka kutuongezea mkataba  kumaliza hadi ghorofa  tunaweza inaweza kutumia mwaka mmoja na nusu kwa maana hadi mwaka 2023 tunaweza kumaliza ianze kutumika.”


Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com