Na Hamis Hussein-Singida
Jumla ya kaya 212,952 kati ya walengwa 212812 sawa na asilimia 100.1 % zimefikiwa na mradi wa vikope kutoka shirika la Hellen Keller International ambapo shirika hilo limezitembelea moja kwa moja kaya hizo kuwabaini wagonjwa wa vikope kisha kuwapatia matibabu ikiwa ni lengo la kutokomeza ungonjwa huo kwa mkoa wa singida kwani ni miongoni mwa magonjwa makuu matano ambayo hayapewi kipaumbele.
Baadhi ya washiriki wa kikao cha kufunga mradi wa vikope mkoani singida wakisikiliza na kujadiliana mambo mbalimbali.Mradi huyo uliodumu kwa miaka mitatu
tangu kuanzishwa kwake 2019 ni miongoni mwa jitihada za wizara ya afya
maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto kupitia mpango wa taifa wa kudhibiti
magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele NTDCP kwa kushirikiana na wadau
mbalimbali ulilenga kupunguza au kuufuta kabisa ungonjwa wa trakoma au vikope
ambapo mikoa 20 ikiwemo mkoa wa singida ndiko utekelezaji wake unafanyika ikiwa
mradi ambao unakotekelezwa kupitia shirika la Hellen Keller International
kutoka nchini marekani.
Mganga mkuu wa mkoa wa Singida Dr.
Viktorina Ludovick amelipongeza shirika hilo kwa namna ambayo limeisaidia
serikali na jamii katika kutokomeza ungonjwa wa trakoma alipokuwa
akizungumza na washiriki wa kikao cha ufungaji wa mradi huo kumwakilisha katibu
tawala wa mkoa.
“Kwa kushirikia na timu zetu za
mikoa na halmashauri pamoja na mdau wetu Hellen Keller International tumeweza
kutekeleza mpango wa kutokomeza vikope kwa Halmashauri zeto
sita Manyoni , Itigi Ikungi Mkalama Singida Vijijini na Singida
Manispaa jumla 212952 kati ya walengwa 212812 sawa na 100.1% . Hapa
tunaona uhitaji ulikuwa mkubwa na tumetekelea mpaka tumevuka lengo”. amesema
Dr Ludovick
Mganga Mkuu mkoa wa singida Dr. Viktorina Ludovick akizungumza na washiriki wa kikao cha kufunga mradi wa vikope kutoka shirika la HKI katika ukumbi wa Aqua Vitae Resort Singida.
Ameyataja mafanikio mengine kuwa ni pamoja na kutoa mafunzo ya kubaini na kutibu wagonjwa wa vikope wataalamu wawili ngazi ya mkoa, wataalamu 13 ngazi ya halmashauri, wahudumu wa afya 1308 ngazi ya kata na vijiji pamoja na wahudumu afya 2851 ngazi ya jamii.
Dr Ludovick ameongeza kuyataja
mafanikio kupitia mradi wa vikopte kutoka shirika La Hellen Keller
Interentaional kuwa wagonjwa 1141 wa vikope ambao walikuwa na tatizo hilo
aidha bila kujua au kukosa sehemu ya kupata msaada
walipata huduma.
Meneja mradi wa trakoma kutoka shirika
la Hellen Keller International (HKI) Athuman Tawakal amesema lengo kubwa la
kuleta mradi huo ilitokana na takwimu zilizoonyesha uhitaji wa huduma hizo kwa
waathirika wa ugonjwa wa vikope.
“ Tumekuja katika maeneo
haya baaada ya kupata takwimu kutoka wizara ya afya kuonyesha ukubwa
wa ugonjwa huu wa trakoma katika maeneo haya na tuliagizwa na wizara
kupitia mpango wa kutokomeza magonjwa yasiopewa kipaumbele ili kusaidia
halmashauri na mkoa katika kuwatafuta wagonjwa na
kuwapatia matibabu na tumeweza kufanikiwa . tumeweza kuwasidia watanzania zaidi
ya 1100 kuwapatia matibubu na tumekuwa tukifanya ufutiliaji”.
Meneja mradi kutoka shirika la HKI Athuman Tawakal Akizungmza na washiriki wakati wa kufunga mradi wa vikope mkoani singida tangu ulipoanzishwa 2019
Dr. Julius Nyenje mratibu wa magonjwa
yasiopewa kipaumbele kutoka wilaya ya Mkalama amelishukuru shirika la HKI kwa
kuwajengea uwezo wa mapambano dhidi ya ungonjwa wa trakoma.
“Trakoma au ungonjwa wa vikope ilikuwa
moja ya magonjwa makuu matano ambayo yalikuwa hayapewi
kipaumbele na HKI mmechukua nafasi kubwa sana na jamii yetu imepata
huduma njema .tunawashukuru sana”. alisema dr. Julius mratibu wa
magonjwa yasiopewa kipaumbele kutoka wilaya ya Mkalama.
Mratibu wa magonjwa ambayo yalikuwa hayapewi kipaumbele kutoka wilaya ya Mkalama Dr. Julius Nyenje akitoa shukrani kwa shirika la Hellen Keller International wakati wa kufunga mradi wa vikope .
Fatuma Jumapili, Elizabeth Wilbroad na Shabani Hamisi ni Baadhi ya wanufaika wa mradi wa vikope kutoka shirika la HKI wamesema huduma ya matibabu ya vikope imewasaidia sanaa kurejesha uwezo wao wa kuona na kulipongeza shirika hilo kwa namna lilivyotekeleza mradi huo.
Dr Upendo Mwakabalile mratibu wa huduma
za macho mkoa wa singida amewasisitiza wataalamu wengine waliopata mafunzo ya
namna ya kuwahudumia wagonjwa wa vikope kutunza takwimu ili ziweze
kusaidia baaadae na kuwataka elimu waliopata kuifanyia kazi kwa watu wengine
wenye uhitaji.
“Naomba kila mtu azingatie sana kwa sababu pasipotakwimu kazi yetu tulioifanya kwa miaka mitatu itakuwa imepotea, kwahiyo takwimu inakuwa ni ushahidi. hawa wahudumu 13 tuliopewa mafunzo tusipofanyia kazi hiyo elimu yetu itakuwa sawa na bure”. amesema Dr. upendo
Mradi wa vipoke mkoani singida umetekelezwa na shirika la Hellen Keller International ikiwa ni miongoni mwa jitihada za wizara ya afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto kupitia mpango wa taifa wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele NTDCP kwa kushirikiana na timu za mikoa na wilaya na wadau mbalimbali ambapo mradi umetekelezwa kwenye wilaya sita ambazo ni manyoni , itigi , ikungi ,mkalama , singida manispaa na singida vijijini ambazo ziliathiliwa na ungojwa wa vipoke kwa kiwango kikubwa .
0 comments:
Post a Comment