Meneja wa Mauzo ya Kibiashara wa Benki ya KCB, Lightness May akizungumza kwenye kwenye semina kwa wadogo na wa kati waliokutanishwa na benki hiyo kupitia KCB Biashara Club. Semina hiyo ilifanyika Novemba 29, 2018 Gold Crest Jijini Mwanza na kuhudhuriwa na washiriki zaidi ya 200 lengo likiwa ni kuwapa mafunzo kuhusu muhusu usimamizi wa fedha, uendeshaji wa biashara pamoja na sheria za kodi.

Mkuu wa Kitengo cha Wafanyabishara wadogo na wa kati (SME) Benki ya KCB, Abdul Juma akizungumza na wafanyabiashara wa Jijini Mwanza kupitia Klabu ya Wafanyabiashara (KCB Busness Club) Jijini Mwanza.
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya KCB wakijitambulisha kabla ya kuanza kwa semina ya "KCB Club Workshop" Jijini Mwanza.
Washiriki wa semina hiyo iliyoandaliwa na Benki ya KCB Jijini Mwanza.
Hii ni semina ya pili kuandaliwa na benki ya KCB kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati (SME) baada ya semina kama hiyo kufanyika Jijini Dar es salaam mwanzoni mwa mwaka huu ambapo "KCB Busness Club" ilizinduliwa mwaka jana.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Benki ya KCB
Tanzania imetoa semina kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati (SME’s) zaidi ya
200 Jijini Mwanza, lengo likiwa ni kuwajengea uwezo kuhusu masuala ya usimamizi
wa fedha, uendeshaji wa biashara pamoja na sheria za kodi.
Semina hiyo
ilifanyika Novemba 29, 2018 kupitia Klabu ya Wafanyabiashara KCB (KCB Busness Club)
Jijini Mwanza, ambapo wafanyabiashara waliojiunga na klabu hiyo wanapata fursa mbalimbali
ikiwemo mafunzo/ semina pamoja na kupanua wigo wa biashara zao ndani na nje ya
nchi.
Akizungumza
kwenye semina hiyo, Meneja wa Benki ya KCB Tawi la Mwanza, Emmanuel Mzava
alisema benki hiyo itaendelea kutoa semina/ mafunzo mbalimbali kwa wateja wake
ili kuwasaidia kukuza biashara zao hivyo wategemee semina zaidi hapo baadae.
Akiwasilisha
mada kwenye semina hiyo, Sweetbert Thomas ambaye ni Mtaalamu wa Kodi
aliwahimiza wajasiriamali na wafanyabishara hao kutambua umuhimu wa mifumo ya
kodi nchini inavyoguza biashara zao hatua itakayosaidia biashara zao kuendelea
kukua.
Nao baadhi
ya wafanyabiashara akiwemo Kitana Chacha Mnanka ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni
ya Mkombozi inayojishughulisha na usafirishaji wa abiria/ mizigo majini na nchi
kavu mkoani Mwanza, waliishukuru Benki ya KCB kwa kuwapatia semina hiyo na
kueleza kwamba itawasaidia kukuza biashara zao ambapo pia walitoa rai kwa
wafanyabiashara wengine kujiunga na Benki hiyo ili kunufaika na huduma zake
ikiwemo elimu kupitia semina mbalimbali.
Nchini
Tanzania, Benki ya KCB ina matawi 14 huku pia huduma zake zikipatikana katika
nchi mbalimbali ikiwemo Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Sudani Kusini pamoja na
Ethiopia ambapo ina matawi 262, mashine za kutolea fedha (ATM) 962 pamoja na
mawakala zaidi ya 15,000 katika ukanda wa Afrika Mashariki huku ikisifika kwa
utoaji wa huduma bora kwa wateja wake.
0 comments:
Post a Comment