METDO Tanzania

METDO Tanzania
Showing posts with label Habari za biashara. Show all posts
Showing posts with label Habari za biashara. Show all posts

Friday, March 18, 2022

KATIBU MKUU WIZARA YA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA AFUNGUKA UKAMILISHAJI WA AWAMU YA KWANZA YA UUNDWAJI WA MFUMO WA KIELEKTRONIKI WA HUDUMA ZA PAMOJA KWA WAWEKEZAJI





KATIBU Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda, Biashara Prof. Godius Kahyarara ameitembelea kamati maalumu iliyoundwa ikishirikisha taasisi mbalimbali za Serikali kwa lengo la kutengeneza mfumo wa kielektroniki wa huduma za pamoja kwa wawekezaji unaojulikana kama Tanzania Electronic Investment Window – TeIW.

Prof. Kahyarara amesema kuwa utengenezwaji wa mfumo huu ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alilolitoa akihitaji Wizara kuanzisha mfumo wa utoaji huduma kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi ili kuwa na dirisha moja la huduma.

Prof. Kahyarara alieleza kuwa timu hii imeanza kazi hii tangu tarehe 7 Desemba, 2021 ambapo walianza kutengeneza mfumo huu katika awamu ya kwanza na upo katika hatua ya mwisho kukamilika na kuanza majaribio na kwa awamu ya kwanza mfumo umeziweka pamoja taasisi saba ikiwemo NIDA, TRA, BRELA, ARDHI, KAZI, UHAMIAJI na TIC.

Alisema kuwa awamu ya pili ya utengenezwaji wa mfumo huu utahusisha taasisi tano zilizosalia ambazo ni TMDA, OSHA, TANESCO, TBS na NEMC.

“Faida za mfumo huu ni kuwa utasaidia upatikanaji wa vibali vyote vinavyotolewa nchini kupatikana kwa urais na kwa haraka kwani huduma zote zitapatikana kupitia dirisha moja na mwekezaji ataweza kuomba vibali husika mahali popote alipo, pia utasaidia kufuatilia hatua za maombi ya uwekezaji”. Alisema Prof. Kahyarara.

Aliongeza kwa kusema kuwa kuanza kutumika kwa mfumo huu utasaidia kupunguza urasimu, gharama na muda kwani mwekezaji atapata huduma zote kupitia mfumo huu na sio kukutana na watoa huduma na hii itasaidia hata kupunguza rushwa na udanganyifu.

Prof. Kahyarara akatumia fursa hiyo kuwashukuru wabia wa maendeleo Trade Mark East Afrika (TMEA) ambao wamefadhili kuwaweka pamoja wataalamu wa kuandaa mfumo huu na sasa nchi yetu inaenda kunufaika kwani wawekezaji watazidi kuja kwa wingi kwani urasimu utapungua kwa kiasi kikubwa.

Kwa upande wake Mratibu wa mradi wa uaandaaji wa mfumo wa dirisha moja kwa wawekezaji (One Stop Centre) Robert John Mtendamema alisema kuwa kituo cha uwekezaji nchini kilianzishwa mwaka 1997 kikiwa na lengo la kuwahudumia wawekezaji kwa haraka chini ya mwamvuli wa dirisha moja (One stop shop) ambapo taasisi mbalimbali za Serikali zinahudumia wawekezaji zimeweka maafisa ambao wana uwezo wa kutoa maamuzi ya kutoa vibali hivyo.

Mtendamema alisema kuwa kupitia mfumo huu unaoundwa sasa utawezesha kuondoa kero mbalimbali kwa wawekezaji hasa zile za kumlazimisha mwekezaji kuingia katika mifumo mbalimbali kutafuta vibali na sasa ataingia katika dirisha moja na kukuta taasisi zote na kufanya maombi kwa wakati mmoja, pia kupitia mfumo huu utawarahisishia wawekezaji kufanya maombi ya vibali na hii itapelekea kuongezeka kwa wawekezaji nchini kwa sababu ya urahisi wa kufanya maombi ya vibali mbalimbali.

Mtendamema aliongeza kwa kusema kuwa kutokana na kukua kwa maendeleo ya sayansi na teknolojia ya TEHAMA kila taasisi ndani ya One Stop Centre wameweza kuwa na mfumo wa kutoa kutoa huduma mbalimbali ambapo mwekezaji anapofika TIC inamuhitaji kuingia katika mifumo isiyopungua 12 ya kila taasisi yenye nywila tofauti kwa ajili ya kufanya maombi.

 

 

Share:

Thursday, December 6, 2018

Benki ya KCB yawapiga msasa wafanyabiashara Jijini Mwanza

Meneja wa Mauzo ya Kibiashara wa Benki ya KCB, Lightness May akizungumza kwenye kwenye semina kwa wadogo na wa kati waliokutanishwa na benki hiyo kupitia KCB Biashara Club. Semina hiyo ilifanyika Novemba 29, 2018 Gold Crest Jijini Mwanza na kuhudhuriwa na washiriki zaidi ya 200 lengo likiwa ni kuwapa mafunzo kuhusu muhusu usimamizi wa fedha, uendeshaji wa biashara pamoja na sheria za kodi.
Share:

Monday, November 12, 2018

Saturday, November 10, 2018

Wazalisha mvinyo wa matunda nchini waiomba Serikali kuwapunguzia kodi ya ushuru wa bidhaa

Na George Binagi-GB Pazzo
Chama cha wazalishaji wa mvinyo wa matunda Tanzania (TALMA) kimeiomba Serikali kupunguza kodi ya ushuru wa bidhaa kutoka shilingi 200 hadi 63 kwa lita moja, hatua itakayosaidia wazalishaji wa bidhaa hiyo kumudu gharama za uendeshaji.
Share:

Tuesday, November 14, 2017

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji akutana na Mkuu wa Mkoa wa Iringa.

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage amekutana na Mkuu wa Mkoa wa Iringa alieambatana na wawekezaji wa Kichina walioonesha nia ya kuwekeza katika mkoa wa Iringa.
 

katika Ziara hiyo, Mkuu wa mkoa wa Iringa Mhe Bi. Amina Masenza ameelezea mikakati iliyopo katika mkoa wake ya kuhakikisha anapokea wawekezaji na kuwapatia maeneo ya kujenga Viwanda ili kuhahakisha wananchi wanaajiriwa kukuza kipato chao.

Mhe. Waziri amesifu jitihada zinazofanywa na Viongozi wa Mkoa wa Iringa katika kuhakikisha wanahimiza ujenzi wa Viwanda na kushirikiana na wawekezaji.

 
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage (Mb) akimsikiliza kwa makini mkuu wa mkoa wa Iringa Mhe. Bi, Anna Masenza.
Wawekezaji walioonesha nia ya ya kuwekeza katika Mkoa wa Iringa, wakisikiliza kwa makini majadiliano yakiendelea katika ofisi ya Mhe. Waziri wa Viwanda.
Wajumbe kutoka Mkoa wa Iringa wakimsikiliza Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji wakati wakujadili masuala mbalimbali ya uwekezaji katika mkoa wa Iringa.
Share:

Wednesday, August 31, 2016

Kampuni ya TTCL yajitosa kudhamini Miss Higher Learning Institutions 2016


Meneja Huduma kwa Wateja wa Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL), Aron Msonga (kulia) akiwagawia line za TTCL zenye huduma za 4G LTE kwa baadhi ya washiriki wa shindano la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016 walipotembelea Makao Makuu ya Ofisi za TTCL jijini Dar es Salaam leo. TTCL ndiye mdhamini mkuu wa shindano la Miss Higher Learning Institutions kwa mwaka 2016.
Washiriki wa shindano la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016 wakiwa katika pozi walipotembelea Makao Makuu ya Ofisi za TTCL jijini Dar es Salaam.
Meneja Huduma kwa Wateja wa Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL), Aron Msonga akizungumza na washiriki wa Shindano la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016 pamoja na wageni wengine walipotembelea Makao Makuu ya Ofisi za TTCL jijini Dar es Salaam. Nyuma yake ni washiriki wa shindano la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016.
Meneja Huduma kwa Wateja wa Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL), Aron Msonga akizungumza na washiriki wa Shindano la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016 pamoja na wageni wengine walipotembelea Makao Makuu ya Ofisi za TTCL jijini Dar es Salaam. TTCL ndiye mdhamini mkuu wa shindano la Miss Higher Learning Institutions kwa mwaka 2016.
Mkuu wa Hitifaki Kamati ya Miss Tanzania 2016, Albert George Makoye (wa kwanza kushoto) akizungumza kutoa shukrani kwa kampuni ya TTCL kwa kukubali kuwa mdhamini mkuu wa Miss Higher Learning Institutions 2016. Wengine ni viongozi na washiriki wa TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016. TTCL ndiye mdhamini mkuu wa shindano la Miss Higher Learning Institutions kwa mwaka 2016.
Mratibu wa shindano la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016, Bi. Maya Nkiru (kushoto) akizungumza kuishukulu kampuni ya TTCL kwa kukubali kuwa mdhamini mkuu wa shindano hilo. Kulia ni Meneja Masoko wa TTCL, Beda Kinunda akiwa katika hafla hiyo.
Mkuu wa duka la huduma za TTCL Makao Makuu ya shirika hilo jijini Dar es Salaam, Diana Obed (kulia) akitoa maelekezo kwa washiriki wa shindano la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016 juu ya bidhaa na huduma mbalimbali za TTCL zinazopatikana katika duka hilo.
 Meneja wa Biashara wa TTCL Mkoa wa Dar es Salaam, Augustino Mwakyembe (kushoto) akitoa ufafanuzi kwa washiriki wa Shindano la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016 walipotembelea Kituo cha Huduma kwa Wateja cha TTCL Makao Makuu ya Ofisi za TTCL jijini Dar es Salaam.
 Na Mwandishi Wetu.
KAMPUNI ya Simu nchini Tanzania (TTCL) wameingia kama mdhamini mkuu wa mashindano ya urembo kutafuta mrembo toka vyuo vikuu nchini 'TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016' atakaye shiriki katika fainali za urembo kumpata mlibwende wa Tanzania 2016.
 TTCL wametangaza kuingia katika udhamini huo leo jijini Dar es Salaam ambapo warembo wa shindano la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016 walipotembelea Makao Makuu ya TTCL kujifunza mambo mbalimbali yanayofanywa na shirika hilo la umma nchini Tanzania.
 Akizungumza katika tukio hilo Meneja Huduma kwa Wateja wa TTCL, Aron Msonga amesema shirika hilo limevutwa kusaidia mashindano hayo ili kuweza kuwapata warembo wenye sifa stahiki watakao shinda katika kinyang'anyiro cha 'TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016' na baadaye kushiriki shindano la Miss Tanzania 2016. 
Amesema TTCL kwa sasa inafanya mageuzi makubwa ya kibiashara na uendeshaji ambayo yameboresha huduma za shirika hilo na bidhaa zake kwa ujumla yanayoinufaisha jamii, hivyo haiwezi kujitenga na shughuli za kijamii ikiwemo mashindano ya urembo. 
Aidha amewashauri waandaaji wa TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016 kufuata taratibu zote bila upendeleo ili kuweza kuwapata wawakilishi wasomi na wenye sifa za ulimbwende ambao watashiriki vema katika kumpata Miss Tanzania 2016. 
Kwa upande wake Mratibu wa shindano la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016, Bi. Maya Nkiru ameishukuru kampuni ya TTCL kwa kuunga mkono mashindano hayo na kuahidi kutoa ushirikiano wa hali ya juu ili kuhakikisha yanafanyika kwa mafanikio makubwa na hatimaye kupatikana warembo wenye vigezo na sifa kuwakilisha tawi hilo kwa ufasaha. Mratibu huyo alisema shindano la kumpata mrembo atakayewakilisha 'TTCL Miss High Learning 2016' kwa mwaka huu limeboreshwa na litakuwa na burudani za kutosha na utofauti mkubwa hivyo kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi siku hiyo ili kuweza kushuhudia shindano hilo. Aidha alitaja baadhi ya wasanii watakaotumbuiza katika shindano hilo kuwa ni pamoja na msanii Ney wa Mitego, MB Dog, Msaga Sumu na kundi la QS. TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016 itafanyika Septemba 17, 2016 katika Ukumbi wa TTC Chang'ombe jijini Dar es Salaam.
Share:

Monday, August 22, 2016

Wezi fedha za TASAF kikaangoni

SERIKALI imetoa siku 30 kukamatwa kwa watumishi waliosababisha matumizi mabaya ya fedha za Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (TASAF) III, kwa kuingiza majina ya watu masikini wasiostahili ili kujipatia fedha za mradi huo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene akizungumza na baadhi ya wakuu wa mikoa, wilaya na wakurugenzi, jana alisema ni lazima watumishi wa umma waliohusika katika kuisababishia hasara Serikali wawajibishwe.
Share:

Saturday, August 20, 2016

KAMANDA MPINGA AHITIMISHA KILELE CHA SHINDANO LA UCHORAJI


Hii ni zawadi ya heshima (tuzo) iliyotolewa na kampuni ya Puma Energy Tanzania na kukabidhiwa kwa mshindi wa kwanza,Mwanafunzi wa darasa la sita kutoka shule ya Msingi Bunge,Veronika Inocent.
OTH2
Mkurugenzi Mkuu kutoka kampeni ya Puma Energy Tanzania Ltd,Philippe Corsaletti akimkabidhi tuzo/zawadi ya Begi na cheti mwanafuzi wa darasa la sita kutoka shule ya Msingi Bunge,Veronika Inocent baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika Kilele cha shindano la Uchoraji kwa ajili ya kuhamasisha usalama barabarani katika shule za msingi jijini Dar Es Salaam kwa mwaka 2016,hafla hiyo fupi iliyoandaliwa na Kampuni ya Puma Energy Tanzania ilifanyika mapema leo katika viunga vya shue ya msingi Bunge.

Mashindano hayo yalihusisha shule kumi kwa upande wa Dar Es Salaam ambazo ni   Mwananyamala, Kisutu, Bunge, Kisiwani, Mchangani, Mnazini, Mwananyamala, Mikocheni, Mtendeni, Kisutu, Kisiwani na Ugindoni,Shule nyingine tatu ni kutoa mkoa wa Geita ambazo zitashiriki na mchakato wa kuwapata washindi,matokeo ya washindi wa mwisho yatatangazwa wakati wa kilele cha cha wiki ya Usalama barabarani ambayo inatarajia kufanyika hivi karibuni.
 
Mwanafuzi wa darasa la sita kutoka shule ya Msingi Bunge,Veronika Inocent akilia kwa furaha mara baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika Kilele cha shindano la Uchoraji kwa ajili ya kuhamasisha usalama barabarani katika shule za msingi jijini Dar Es Salaam kwa mwaka 2016,hafla hiyo fupi iliyoandaliwa na Kampuni ya Puma Energy Tanzania ilifanyika mapema leo katika viunga vya shue ya msingi Bunge.

Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini,Kamanda Mohamed Mpinga pamoja na Waandaji kutoka kampuni ya Puma Energy Tanzania na AMEND wakitafuta washindi watatu wa shindano la uchoraji katika masuala mazima ya kuhamasisha usalama barabarani 2016.
Share:

OSHA kuendesha zoezi maalum la upimaji afya za waliokuwa wafanyakazi wa mgodi wa Bulyanhulu

gyun
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) Dkt. Akwilina Kayumba akiongea na Waandishi wa Habari ( hawapo pichani) kuhusu utaendesha wa zoezi maalum la upimaji afya za waliokuwa wafanyakazi wa mgodi wa Bulyanhulu ambao waliachishwa kazi na mgodi huo mnamo mwaka 2007 bila kupimwa afya zao kinyume na Sheria ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi ya mwaka 2003.
Share:

SERIKALI KUNUNUA RADA SITA ZA KISASA

REIA1
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akizungumza na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi Ally Karume mara baada ya kumtembelea ofisini kwake Kisiwani Unguja.
RIA2
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akifafanua jambo kwa wakati viongozi wa taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo Kisiwani Unguja. Kulia ni Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi Ally Karume.
RIA5
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akijadiliana jambo na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi Ally (kulia) Karume wakati alipotembelea taasisi zilizochini ya Wizara hiyo. Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar hiyo Mustafa Abood Jumbe.
Share:

Waziri Mkuu Ziarani Katavi


MAPOKEZI makubwa yanamsubiri Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa anayetarajiwa kuwasili leo mchana mjini Mpanda kuanza ziara ya kikazi ya siku nne mkoani Katavi inayoambatana na kutembelea, kukagua miradi kadhaa ya maendeleo na kuhutubia mikutano ya hadhara.

Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa kiongozi wa juu wa kitaifa kutembelea mkoa wa Katavi tangu Serikali ya Awamu ya Tano ilipoingia madarakani, ziara ambayo itamfikisha pia katika mkoa jirani wa Rukwa.
Share:

Tanzania kuachana na nguo za mitumba ifikapo mwaka 2018


Na Beatrice Lyimo-MAELEZO
Serikali imeazimia kuachana na biashara ya kuingiza nguo za mitumba kutoka nje ya nchi ifikapo mwaka 2018.

Maazimio hayo yamebainishwa na Waziri wa nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama katika uzinduzi wa mafunzo ya uanagenzi ya ushonaji nguo katika kiwanda cha Tanzania Tooku Garments Company, Ltd.
Share:
Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com