Mkuu wa Mkoa Geita, Mhandisi Robert Gabriel (katikati) akitoa salamu za shukrani na kumkaribisha Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (kushoto) aliyeanza ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani Geita jana, kulia ni mbunge wa Chato na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Medard Kalemani.
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akiweka jiwe la msingi la ukarabati na ujenzi wa Kituo cha Afya Bwanga wilayani Geita.
Wakazi wa Geita walijitokeza kwa wingi kumlaki Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa.
Na George Binagi-GB Pazzo
Waziri Mkuu
Mhe. Kassim Majaliwa amesifia ukarabati na ujenzi wa Kituo cha Afya Bwanga
kilichopo wilayani Geita, na kueleza kwamba serikali itaendelea kuboresha
huduma za afya nchini ikiwemo kuhakikisha hakuna uhaba wa dawa na wataalamu wa
afya.
Mhe.
Majaliwa aliyasema hayo jana wakati wakiweka jiwe la msingi la ukarabati na
ujenzi wa Kituo hicho, kilichopokea shilingi Milioni 500 kupitia mfumo wa “Force
Account” na kujenga majengo matano ambayo ni nyumba ya mtumishi (Two in one),
maabara, wadi ya akina mama, jengo la upasuaji pamoja na chumba cha kuhifadhia
maiti ambapo bado chenchi ilibaki na kufanya shughuli zingine ikiwemo ujenzi wa
njia za wateja kutembea (walking way) na eneo la wagojwa/ wateja kupumzika
wakati wakisubiri huduma.
“Tuliwaambia
nafuu tukikagua tukute mtu amejinyonga siyo amekula hela ya wananchi”, Alisema
Mkuu wa Mkoa Geita Mhandisi Robert Gabriel wakati akitoa salamu za shukrani.
Tazama Video hapa chini
0 comments:
Post a Comment