Mkurugenzi
wa Shirika la kutetea haki za wasichana na wanawake KIVULINI la Jijini Mwanza,
Yassin Ally, akizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni ya kutokomeza ukatili wa
Kijinsia katika wilaya ya Tarime mkoani Mara. Uzinduzi huo ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango wa Kitaifa wa Kutokomeza Ukatili wa Kijinsia kwa Watoto na Wanawake katika kipindi cha mwaka 2017/22.
Uzinduzi huo ulifanyika Novemba
28, 2018 katika Kata ya Muriba ukienda sanjari na uzinduzi wa kampeni ya Siku
16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia Duniani. Siku 16 za Kupinga
Ukatili wa Kijinsia Duniani ni kampeni ya Kimataifa inayoongozwa na Kituo cha Kimataifa cha
wanawake katika uongozi tangu mwaka 1991 kutokana na mauaji ya kinyama ya akina
dada wa Mirabelle yaliyofanyika nchini Dominica mwaka 1960.
Mwaka 1991 Umoja wa
Mataifa (UN) ulichagua Novemba 25 kuwa siku ya Kimataifa ya Kupinga Ukatili wa
Kijinsia ambapo kilele chake huadhimishwa siku ya 16 ambayo ni Disemba 10 ya
kila mwaka.
Picha na Frankius Cleoface, Tarime
Afisa Ustawi
wa Jamii Mkoa wa Mara, Elizabert Mahinya, akizungumza kwenye uzinduzi huo kwa
niaba ya mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya Tarime Glorious Luoga (hayuko pichani).
Baadhi ya
wananchi wakiwa katika maandamano ya amani kufikisha ujumbe kuhusu jamii
kuondokana na aina zote za vitendo vya Ukatili wa Kijinsia ikiwemo ukeketaji.
Baadhi ya wanafunzi wakiwa kwenye maandamo hayo.
Wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari walishiriki uzinduzi huo, lengo ikiwa ni kufikisha elimu kuhusu jamii kuondokana na aina zote za ukatili wa Kijinsia ikiwemo kwa watoto na wanawake.
Maadhimisho ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia hufanyika kila mwaka kote duniani kufikisha elimu kwa jamii kuondokana na aina zote za vitendo vya ukatili wa Kijinsia.
"Chapa Kazi, Siyo Mkeo"
"Kukeketa Sasa Basi"
Taswira ulipofanyika uzinduzi wa kampeni ya kupinga vitendo vya Ukatili wa Kijinsia wilayani Tarime.
Viongozi wa Serikali, Wanaharakati, Jesho la Polisi, Madiwani pamoja na Serikali za Mitaa walishiriki kwenye uzinduzi wa kampeni hiyo ya kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii. Kampeni hiyo ya Kitaifa inatekelezwa na Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo shirika la KIVULINI katika mikoa mbalimbali ikiwemo Mwanza, Mara na Shinyanga.
Na BMG
Jeshi la
Polisi katika Wilaya ya Tarime mkoani Mara limetakiwa kutowafumbia macho wale
wote watakaobainika kujihusisha na suala la Ukeketaji kwa watoto wa kike na badala
yake kuwachukulia hatua kali za kisheria.
Kauli hii
imekuja wakati ambao baadhi ya wanajamii katika kabila la Wakurya mkoani Mara, wamejipanga
kwa ajili ya kutekeleza mila potofu ya ukeketaji ambayo kwa kabila hilo
hutekelezwa kila mwaka unaogawanyika kwa mbili.
Mkurugenzi
wa Shirika la Kutetea Haki za Wasishana na Wanawake KIVULINI la Jijini Mwanza,
Yassin Ally alitoa rai hiyo Novemba 28, 2018 kwenye uzinduzi wa kampeni ya
kitaifa ya kupinga ukatili wa kijinsia kwa watoto na wanawake uliofanyika
katika Kata ya Muriba wilayani humo.
Ally alisema
vitendo vya Ukatili ikiwemo Ukeketaji, ndoa na mimba za utotoni vinakwamisha kasi
ya maendeleo katika jamii pamoja na kuchochea ufaulu hafifu kwa wanafunzi wa
kike na hivyo kuwahimiza wazazi na walezi wilayani Tarime kujiepusha na vitendo
hivyo.
Akizungumza
kwenye uzinduzi huo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya Tarime Glorious Luoga, Afisa
Ustawi wa Jamii Mkoa Mara, Elizabert Mahinya alisema kampeni hiyo itasaidia
kuongeza uelewa kwa wananchi kuhusu dhana ya kutokomeza ukatili wa kijinsia na
hivyo kuifikia Tarime Mpya isiyo ukatili.
Uzinduzi wa
kampeni ya kupambana na Ukatili wa Kijinsia wilayani Tarime ni sehemu ya
utekelezaji wa Mpango wa Kitaifa wakutokomeza Ukatili wa Kijinsia kwa wanawake
na watoto unaotekelezwa katika kipindi cha mwaka 2017/18 ambapo uzinduzi huo
ulienda sanjari na kampeni ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia Duniani
itakayofikia kilele chake Disemba 10.
0 comments:
Post a Comment