Na Mwandishi wetu - Mara
WAZIRI wa Afya maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Mhe.Dkt. Dorothy Gwajima, amesisitiza kujengwa kwa mifumo ya TEHAMA ikiwa ni mpango wa kuwezesha huduma bora za afya katika jamii.
Dkt. Gwajima amesema hayo baada ya kuwasili mkoani Mara, kwa ajili ya Ziara ya Kikazi, ambapo ameanza kwa kukutana na Sekretarieti ya Mkoa na kusisitiza kufunga mifumo ya TEHAMA katika maeneo yakutolea huduma Bora za Afya ili kuziba mianya ya upotevu wa mapato.
0 comments:
Post a Comment