Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa
Barabara Vijijini na Mjini Mhandisi Victor Seif akieleza majukumu ya
TARURA kwenye kikao cha kamati ya kudumu ya bunge ya utawala na Serikali
za mitaa na kamati ya kudumu ya bunge ya hesabu za Serikali za Mitaa
kilichofanyika katika ukumbi wa Hazina mjini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo akiongea kwenye
kikao cha kamati ya kudumu ya bunge ya utawala na Serikali za mitaa na
kamati ya kudumu ya bunge ya hesabu za Serikali za Mitaa kilichofanyika
katika ukumbi wa Hazina mjini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa
Barabara Vijijini na Mjini Bw.Abdul Digaga akiongea kwenye kikao cha
kamati ya kudumu ya bunge ya utawala na Serikali za mitaa na kamati ya
kudumu ya bunge ya hesabu za Serikali za Mitaa kilichofanyika katika
ukumbi wa Hazina mjini Dodoma.
……………
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo amesema
hatavumulia kuwa na watumishi mizigo ambao hawatimizi majukumu yao
kikamilifu na kuleta mabadiliko katika sekta ya barabara ambayo ni nguzo
ya uchumi nchini.
Waziri Jaffo ameyasema hayo wakati
wa ufunguzi wa semina ya siku moja kwa wabunge wa Kamati ya kudumu
Serikali za mitaa(TAMISEMI) sambamba na Kamati ya Hesabu za Serikali
za Mitaa(LAAC) kuhusu majukumu ya Wakala wa barabaraza vijijini na
mijini(TARURA) iliyofanyika katika ukumbi wa Hazina Mjini Dodoma
Mhe. Jaffo amesema Serikali
ilishatoa muongozo wa malengo ya utendaji kazi katika utumishi wa umma
na kuwapima kulingana na malengo yao hivyo watumishi ambao watashindwa
kutekeleza na kufikia malengo waliyopangiwa Serikali haitasita
kuwachukulia hatua za kiutumishi.
Amesema kuwa Serikali haitavumilia
suala zima la ubadhilifu kwa watumishi wa umma, kwa kuwa Serikali
haiwezi kumbeba mtu ambaye ni mbadhilifu kwa kuwa Serikali inahitaji
kuleta mabadiliko katika utendaji kazi na kuleta maendeleo kwa jamii.
Amesema kuwa Taruara ni chombo
kipya hivyo haitaji kuajiri watumishi ambao ni mzigo ambao waleta sura
mbaya kwa jamii kabla chombo hiki hakijafanya kazi ya kuwahudumia
wananchi katika kutatua kero ya miundombinu ya barabara vijijini na
mijini.
Amewataka Wabunge wa kamati zote
mbili (LAAC&TAMISEMI) kusimamia utekelezaji wa miradi iliyoko chini
ya TARURA na kuhakiki ubora wa miradi hiyo na kukosoa pale wanapoona
miradi haitekelezwi kwa viwango vinavyotakiwa ili wahusika waweze
kurekebisha makosa kabla ya kukabidhi miradi hiyo kwa wahusika.
Aidha aliwahisi Wabunge kuendelea
kuishauri TARURA kwa kuwa chombo hiki kimeundwa kwa ajili ya kutoa
majibu ya changamoto za Wananchi hivyo ni wajibu wetu kuwasilisha yale
yote ambayo tunaona yanawakwaza wananchi katika majimbo yetu.
Mhe Jafo amemuuagiza Mkurugenzi wa
TARURA Mhandishi Victor Seif kuhakikisha Mameneja katika ngazi ya
Wilaya wanasaini Mkataba wa Makubaliano ya kazi “Performance contract”na
kuwafuatilia utendaji wao kwa mujibu wa Mkataba na atakeyeshindwa
kufikia malengo yaliyowekwa atolewe bila kigugumizi ili kupisha
watendaji wengine watakaofanya kazi kulingana na matakwa ya Serikali.
Wakati huohuo Mkurugenzi Mtendaji
wa Wakala wa barabara vijijini na mijini (TARURA) Mhandisi Victor Seif
amesema kulingana na muundo na majukumu ya Wakala wa Barabara
mahitaji halisi ya watumishi ni 3,222 lakani mpaka sasa ni watumishi
1,147 wameshapatikana ambapo 47 wako Makao Makuu, 103 Mikoa na 997
katika halmashauri, na pia kuna upungufu wa watumishi 2,075 katika kada
mbalimbali.
TARURA ina majukumu ya Msingi ya
ujenzi, ukarabati na matengenezo ya mtandao wa barabara zenye urefu wa
Km 108,946.2 za vijini, mijini pamoja na madaraja, na kati ya hizo
barabara 56,000 zinafanyiwa uhakiki ili ziweze kutangazwa kwenye Gazeti
la Serikali ili zitambulike kisheria na Km 52,946.2 tayari
zimeshatambulika na kutangazwa kwenye Gazeti la Serikali.
0 comments:
Post a Comment