Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri
ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga akizungumza wakati wa kikao cha
Baraza la Madiwani kwa ajili ya kupokea taarifa za kata.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya
Wilaya ya Kishapu Boniphace Butondo akifungua kikao cha Baraza la
Madiwani katika ukumbi wa halmashauri.
Madiwani wakiimba wimbo wa taifa kabla ya kuanza kwa kikao hicho.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya
Wilaya ya Kishapu Boniphace Butondo (kushoto) akiwa katika picha ya
pamoja na Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri, Stephen Magoiga na Makamu
Mwenyekiti, Edward Shigela.
…………………………………………………………………………..
Na Robert Hokororo, Kishapu DC
Baraza la Madiwani katika
Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga limekutana kwa ajili
ya kuwasilisha na kupokea taarifa za miradi ya maendeleo ya kata zake
mbalimbali.
Katika kikao hicho cha kujadili
taarifa za robo ya kwanza ya Julai hadi Septemba, Mwenyekiti wa
halmashauri hiyo, Mhe. Boniphace Butondo aliipongeza Kishapu kwa kupata
hati safi kutokana na ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu (CAG).
Mhe. Butondo ambaye pia ni diwani
wa kata ya Lagana aliwataka madiwani waendelee kushikamana na
kuwahudumia wananchi katika kata zao ili kueleta maendeleo katika
halmashauri ya wilaya hiyo.
Alisema ni wajibu wao
kuwahamasisha wananchi kuchangia maendeleo katika kata zao sambamba na
kuendelea kuwahamasisha kuhusu kilimo hususan cha mazao yanayostahimili
ukame.
“Waheshimiwa tuwahudumie wananchi
katika kata zetu na hasa ukizingatia hivi sasa Serikali inapiganaia
katika kufufua zao la pamba katika wilaya yetu nasi tuwahamasishe
kulima,” alisema.
Aliongeza kuwa katika kikao hicho
Baraza linajipima wapi wamefikia katika miradi ya maendeleo na wapi
wamekwama hivyo kuweza kutatua changamoto hizo na hatimaye kusonga
mbele.
0 comments:
Post a Comment