Bw. Elijah Mwandumbya Kamishna wa
Kodi za Ndani Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) akizungumza na
waandishi wa habari Kariakoo jijini Dar es salaam jana mara baada ya
msako mkali wa wauzaji wa kazi feki za wasanii nchini Tanzania ambapo
wamefanikiwa kukamata CD nyingi ambazo hazina stika za TRA na kuonyesha
wazi kwamba kazi hizo ni feki,
Kamishna Elijah Mwandumbya
amesema wataendelea na kazi hiyo na kuwasaka wote wanaojihusisha na kazi
hiyo haramu inayoinyima serikali mapato , lakini pia inayodhulumu jasho
la wasanii nchini Tanzania, Amewashukuru wadau mbalimbali
wanaoshirikiana na Mamlaka hiyo katika kufanikisha kazi hiyo na
kumpongeza Bw. Alex Msama na kampuni yake ya Msama Auction Mart kwa
jinsi ambavyo inajituma na kutetea haki ya wasanii nchini.
Bw. Elijah Mwandumbya Kamishna wa
Kodi za Ndani Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) akizungumza akitoa
maelezo kwa mmoja wa vijana walikokamatwa wakiuza kazi feki za wasanii
Kariakoo jana.
Bw. Alex Msama Mkurugenzi wa
kampuni ya Msama Auction Mart akikamata moja ya kompyuta ambazo
zinatumika kutoa kopi feki za nyimbo na filamu za wasanii huku mmoja wa
vijana wanaojihusisha na kazi hiyo akiwa chini ya ulinzi.
Bw. Elijah Mwandumbya Kamishna wa
Kodi za Ndani Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) akitoa maagizo kwa
mmoja wa vijana walikokamatwa wakiuza kazi feki za wasanii Kariakoo
jana.
Bw. Alex Msama Mkurugenzi wa
kampuni ya Msama Auction Mart akiongozana na Bw. Elijah Mwandumbya
Kamishna wa Kodi za Ndani Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakati
walipofanya msako huo Kariakoo jijini Dar es salaam jana.
Mmoja wa watuhumiwa
wanaojihusisha na kazi hiyo akijijitetea mbele ya askari wakati
alipkamatwa katika duka lake akiuza CD feki za nyimbo na filamu.
Bw. Alex Msama Mkurugenzi wa
kampuni ya Msama Auction Mart akionyesha moja ya CD feki zilizokamatwa
katika moja ya duka kwa maofisa wa TRA.
Watuhumiwa wa uuzaji wa CD feki
za Muziki na Filamu wakiwa chini ya Ulinzi na maboksi ya CD zao mara
baada ya kufikishwa kwenye kituo Kikuu cha cha polisi kanda maalum ya
Dar es salaam.
Mmoja wa maaskari akiimarisha ulinzi kwa watuhumiwa hao katika kituo kikuu cha Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam
0 comments:
Post a Comment