Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI na Mbunge wa Kisarawe Selemani
Jafo akijiandaa kukata keki katika katika sherehe ya kuwapongeza walimu wa
shule za msingi wilayani Kisarawe.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI na Mbunge wa Kisarawe Selemani
Jafo akikata keki maalum kwa ajili ya walimu wa Kisarawe.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI na Mbunge wa Kisarawe Selemani
Jafo akiwa na walimu wanaostaafu katika sherehe ya kuwapongeza walimu wa shule za
msingi wilayani Kisarawe.
Walimu wa shule za msingi Kisarawe waliohudhuria katika ya
sherehe ya kuwapongeza walimu hao.
..........................................................
Wilaya ya Kisarawe imedhamiria kuongeza kiwango cha ufaulu kwa
wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kwa kuweka mikakati kabambe
itakayowezesha wanafunzi kuwa mahiri katika masomo pamoja na mitihani.
Hayo yamebainishwa na Mbunge wa jimbo la Kisarawe Selemani Jafo
katika sherehe ya kuwapongeza walimu wa shule za msingi wilayani Kisarawe iliyofanyika
katika ukumbi wa shule ya sekondari ya minaki.
Katika sherehe hiyo, Jafo ambaye pia ni Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais, TAMISEMI, amewapongeza walimu wa wilaya hiyo kwa kuongeza ufaulu
na kwamba inahitajika mikakati mingi zaidi ili wanafunzi wawe mahiri kwenye
mitihani.
Hata hivyo amesema hali ya baadhi ya shule za Kisarawe kuwa
miongoni mwa shule kumi za mwisho katika mitihani kwasasa imetoweka.
Aidha Jafo ametoa maelekezo ya ununuzi wa mtambo mkubwa wa kudurufu
mitihani ili suala la uchapishaji wa mitihani ya shule za msingi na sekondari
usiwe tatizo tena.
Jambo hilo limeleta faraja kubwa kwa walimu waliokuwepo katika
sherehe hiyo kwani itawezesha kufanyika kwa mitihani ya kujipima kwa urahisi
wilayani humo.
Mtambo huo mpya unatarajiwa kununuliwa ndani ya wiki hii kwa
kuwa fedha zimeshapatikana kutokana na michango kutoka kwa wadau mbalimbali
wanao endelea kuchangia kampeni ya "Ondoa Zero Kisarawe"
Kampeni hii imeonyesha kuzaa matunda kwani idadi ya wanafunzi
waliopata daraja la sifuri imepungua kutoka wanafunzi 457 hadi 256. Pia
wanafunzi waliopata daraja la kwanza hadi daraja la nne wameongezeka na kufikia
163 wakati hapo awali walikuwa chini ya wanafunzi 50.
0 comments:
Post a Comment