Na Hamis Hussein - Singida
SERIKALI
kupitia bajeti ya wizara ya maji kwa mwaka wa fedha 2021-2022 imetenga jumla ya
shilingi milioni 316 kijiji cha mitula shilingi milioni 500 kijiji cha Mwighaji
huku milioni 565 ambazo ni hela ya uviko kwa kijiji cha migugu kwaajili ya
utekelezaji wa mradi wa maji katika huku kwaajili ya kijiji ya migugu vijiji
vyote vipo katika wilaya ya singida ambapo zoezi la usambazaji wa mitambo ya
maji limeanza kufanyika.
Meneja
wa wakala ya maji na usafi wa mazingira vijijini ruwasa wilaya ya singida
Athuman Abdul Mkalimoto amesema kuwa
jumla ya miradi mine itatekelezwa kukamilisha huduma maji katika wilaya ya
singida ambapo mradi wa ughandi ‘B’ umeshafikia asilimia 75
na miradi mingine inaendelea kutelezwa kuanzia mwezi huu wa January 2022.
“Katika
kutekeleza bajenti ya mwaka wa fedha 2021-2022 tumepanga kutekeleza miradi
mikuu minne. Mradi wa kwanza ni wa mighaji wenye thamani ya milioni 500, miradi
wa mipili ni wa kijiji cha migugu wenye thamani ya milioni 565 kupitia fedha za
uviko mpaka sasa mkandarasi ameshapatikana. mradi mwingine ni ule wa ughandi B Umeshafikia
asilimia 75%”. Alisema Mkalimoto Meneja wa Ruwasa
Meneja
Mkalimoto aliongeza kuwa mradi wa kijiji
cha mitula chenye wakazi zaidi ya 2000 sasa umeanza utekelezaji ambapo zoezi la
usambazji wa mitambo ya maji imepokelewa ambapo kukamilika kwa mradi huo utawasaidia
wakazi wa kijiji hicho.
“Tunashukuru
sana serikali tumepokea mabomba yatakayokamilisha mradi wa maji katika kijiji
hichi ya mitula itatusaidia kukamilisha kwa haraka mradi huu kuwanufaisha
wananchi , tutahakikisha mradi huu unakamilika kabla ya mwezi wa tano.
Alisema Mkalimoto Meneja wa RUWASA wilaya singida.
Mhandisi
wa Ruwasa wilaya ya singida Eng. Joel Kibusi amesema uwepo wa miradi ya maji ni
fursa kwa wakazi wa kijiji husika kujipatia
kipato kwa kushiriki katika kazi za uchimbaji wa mtaro na utandazaji wa
mitambo na kuwataka kuvitunza vyanzo vya maji .
“Mtu atoke
hapa aende achukue wasukuma shinyanga kweli wakati kuna vijana wenyenguvu kwahiyo nawaomba wananchi wa
hapa hasa vijana na utakapotumika unalipwa . niwaombe sana mazingira yenu
muyatunze kuna sehemu tunajenga kituo cha maji siku tunakwenda kukagua tunakuta
kuna mtu kashusha mzigo hadi tunaoneka na hatuna kitu” alisema Eng.
Kibusi .
Baadhi
ya wakazi wa kijiji cha mitula walionesha kufurahishwa na ujuo wa mradi huo wa maji kwa wamekuwa wakitaabika kupata huduma ya maji
katika maisha ya kila siku wanayokuwa
wanaishi
Jamani
mimi nawapongeza ruwasa yaani mitula
nilikuwa najua ni ndoto lakini alipoongea mkuu wa msafara nimefurahi sana . kwa
sababu hichi kisima tumengojea kwa muda mrefu na sisi tulikuwa tunasema kuwa
kwa kuwa mradi umeanza hawatatutelekeza . walisema
wakazi wa mitula wakati wa kupkea paipu za maji kijijini hapo .
Zoezi
la kusambaza mabomba ya maji limeanzakufanyika katika kijiji cha mitula
ambapo utekelezaji wake unaaza mwezi huu
wa January jumla ya vituo vya 7 maji (Domestic Point ) taki la maji la lita
75000 litapelekwa kijiji cha mitula , taki la lita 90000 kijiji cha
mwighaji na sasa uchimbaji na ulazaji wa mabomba na kutandika paipu
unaendelea.
0 comments:
Post a Comment