Rai hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Dkt Angeline Mabula wakati akizungumza na wahitimu wa fani za udaktari, ufamasia, uuguzi, maabara na mionzi wa chuo cha afya na sayansi shirikishi Bugando jijini Mwanza yaliyoandaliwa na chama cha kimitume cha wanafunzi wa kikatoliki TMCS ambapo amewataka wahitimu hao kuhakikisha wanakuwa mabalozi wazuri katika kutoa huduma bora na zenye weredi kwa jamii kwa kuzingatia maadili waliyoyapata wakati wa masomo yao sanjari na kuwaasa juu ya kujiunga katika vikundi kwa kuzingatia taaluma zao ili kuweza kupata mikopo isiyokuwa na riba inayotolewa na halmashauri zote nchini ili kupambana na changamoto ya ajira kwa fani zisizokuwa na fursa ya kuajiriwa moja kwa moja Serikalini
'.. Uadilifu ni miongoni mwa mambo yanayopotea kwa kasi kubwa licha ya kuhitajika sana kwa wakati tulionao, Nendeni mkawe waadirifu, Katika uadirifu kuna upendo, Katika uadirifu kuna weredi ..' Alisema
Aidha Mhe Dkt Mabula akawasisitiza wahitimu hao kuzingatia maadili ya dini, kushiriki zoezi la uchaguzi mkuu linaloendelea nchini ili kupata viongozi wazuri na wenye hofu ya Mungu kama Rais Mhe Dkt John Magufuli, Sambamba na kumpongeza kiongozi huyo kwa namna alivyoiongoza nchi wakati wa mapambano dhidi ya ugonjwa Covid-19 unaosababisha homa ya mafua makali maarufu kwa jina la Corona pamoja na kuvuka malengo kwa kuingia katika nchi zenye uchumi wa kati mapema kabla ya mwaka 2025 ambavyo ilivyotarajiwa.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Jumuiya hiyo ya TMCS Bugando (Tanzania Movement Catholic Students) Ndugu Peter Mbogoni mbali na kupongeza Serikali kwa jitihada zake katika kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo akamshukuru mgeni Dkt Mabula kwa ushirikiano wake sanjari na kuwasilisha changamoto ya ukosefu wa mtaji wa uhakika katika mradi wao wa uzalishaji fulani.
Huku moja ya wahitimu Bi Loveness Avit akihitimisha kwa kushukuru kumalizia salama masomo yake na kuahidi kuitumikia jamii kwa upendo, weredi na uadirifu mkubwa.
0 comments:
Post a Comment