
***************
Kocha Mkuu wa timu ya soka ya
Tanzania Taifa Stars, Emmanuel Amunike,anamatumaini ya kufanya vizuri
katika mchezo wa pili wa mashindano ya Mataifa Afrika (AFCON) dhidi ya
Kenya,katika mchezo utakaofanyika Juni 27,katika Uwanja wa 30
Juni,Misri.
Akizungumza na waandishi wa
habari,Amunike,alisema anatambua Kenya ni timu nzuri na ina wachezaji
wazuri,lakini hilo halimpi shida kwakuwa viwango vya wachezaji wa Kenya
na vya wachezaji wa Tanzania vinalingana,hivyo hana wasiwasi wa kupata
matokea katika mchezo huo..
“Timu zote ni za kutoka Afrika
Mashariki na Kenya ni majirani zetu,na wote tunazungumza lugha ya
Kiswahili,kwahiyo hakuna kitu cha kujificha ,kitu kikubwa ni kwamba ni
kwa jinsi gani tutaweza kufanya katika huo mchezo,tulionao katika
mchezo wa Senegal wachezaji walikuwa na uoga,lakini siwezi kuwalaumu,
kwakuwa haya ni mashindano yao makubwa kucheza,”alisema na kuongeza:
“Kitu kikubwa cha muhimu
ambacho tunachokifanya kwasasa ni kuwapa moyo kuwajenga kiakili na
kuwajengea ubora zaidi uwanjani wachezaji kabla ya mchezo wetu
unaofuata,binafsi nina wachezaji bora na wenye uwezo,kwahiyo katika
soka la kisasa naamini wanasifa za kushindana.”
Taifa Stars,inatarajia kushuka
dimbani Alhamisi wiki hii, ikiwa na matumaini ya kupata alama tatu
muhimu, ambazo zitaisaidia kuiweka katika mazingira mazuri ya kuweza
kupata nafasi ya kufuzu kwa raundi ya pili ya mashindano.
0 comments:
Post a Comment