Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza
Kikao cha Kamati ya Pamoja ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT)
na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kujadili masuala ya Muungano. Kikao
hicho kimefanyika leo Februari 9, 2019 katika ukumbi wa Kambarage, jengo la
Hazina Square, Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
Sehemu
ya Mawaziri kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) wakifuatilia kwa
makini Kikao cha Kamati ya Pamoja ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kujadili
masuala ya Muungano. Kikao hicho kimefanyika leo Februari 9, 2019 katika ukumbi
wa Kambarage, jengo la Hazina Square, Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa
Rais).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akimkabidhi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif ali Iddi
(kushoto) hati ya umiliki wa ardhi yenye ukubwa wa hekari 30 kwenye mji
wa Serikali Dodoma kwa ajili ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakati wa
ufunguzi wa Kikao cha Kamati ya Pamoja ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kujadili
masuala ya Muungano. Kikao hicho kimefanyika leo Februari 9, 2019 katika
ukumbi wa Kambarage, jengo la Hazina Square, Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu
wa Rais).
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba
akihutubia wakati wa kikao cha Kamati ya Pamoja ya Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ)
kujadili masuala ya Muungano. Kikao hicho kimefanyika leo Februari 9, 2019
katika ukumbi wa Kambarage, jengo la Hazina Square, Dodoma. (Picha na Ofisi ya
Makamu wa Rais).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema vikao vya masuala ya Muungano vinaendeshwa
kirafiki kama ndugu wawili ambao wamekaa na kujadili mambo yao.
Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa
kikao cha Kamati ya Pamoja ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT)
na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kujadili masuala ya Muungano kilichofanyika
februari 9, 2019 katika ukumbi wa Kambarage, Jengo la Hazina Square, Dodoma.
“Vikao hivi vina mambo mengi
mchanganyiko si sheria na katiba peke yake vinavyofanya kazi kuna mengine,
consideration zingine zinabidi ziingie ili kupata njia sahihi” alisema Makamu wa Rais
Kwa upande wake Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi alikabidhi kiwanja chenye ukubwa wa
hekari 30 kilichopo kwenye eneo la mji wa Serikali Dodoma kwa Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar bila gharama yeyote kama alivyoelekeza Mhe. Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
“kiwanja ni kikubwa sawa na viwanja
vilivyotolewa kwa Wizara 10 za bara” alisema
Waziri Lukuvi.
Awali Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais
Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba alisema kikao hicho ni cha kawaida
ambacho kimejadili masuala ya Muungano na kilitanguliwa na vikao vingine
vilivyojumisha Makatibu Wakuu pamoja na Mawaziri.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Samia Suluhu Hassan alikabidhi hati ya umilikiwa wa kiwanja hicho chenye
ukubwa wa hekari 30 kilichopo mji wa Serikali Dodoma kwa Makamu wa Pili wa Rais
wa Zanzibar Balozi Seif Iddi.
Kikao hicho cha Kamati ya Pamoja ya Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ)
kujadili masuala ya Muungano kilihudhuriwa na Mawaziri wa Serikali zote mbili
pamoja na Makatibu Wakuu na Timu ya Wataalamu.
0 comments:
Post a Comment