METDO Tanzania

METDO Tanzania

Sunday, August 23, 2020

RC HAPI: AMTUMBUA MWENYEKITI NA KUCHANGIA MIFUKO 100 YA SARUJI RUNGEMBA

Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi akiongea na wananchi wa kijiji cha Rungemba wakati wa ziara ya kukagua miradi pamoja na kusikiliza kero za wananchi
Stephen Kalinga akiwa kwenye gari ya polisi baada ya mkuu wa mkoa kuamuru akamatwe kwa kosa la kuongea uongo kwenye mkutano wa hadhara
Stephen Kalinga na mwenzake wakiwa kwenye gari ya polisi baada ya mkuu wa mkoa kuamuru wakamatwe kwa kosa la kuongea uongo kwenye mkutano wa hadhara

Na Fredy Mgunda,Iringa. 

Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi ameamuru kukamatwa kwa mwenyekiti wa bodi ya maji ya kijiji cha lungemba wilayani mufindi Stephen Kalinga kwa kosa la kuwa mchonganishi baina ya serikali na wananchi huku akiahidi kuchangia mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa wodi la akinamama. 

Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua miradi halmashauri ya Mji wa Mafinga katika zahati ya kijiji cha Rungemba, mkuu wa mkoa alibaini kuwepo kwa tuhuma ambazo hazina ukweli wote. 

Akisikiliza kero za wananchi wa kijiji hicho,mkuu wa mkoa alipokea barua kutoka kwa mwananchi iliyokuwa inatuhuma kwa baadhi ya viongozi wa kijiji hicho na kuanza kuzitafutia majibu kwa viongozi waliokuwa wametajwa. 

Baada ya kubaini kuwa ndugu Stephen Kalinga alitoa tuhuma ambazo zilikuwa hazina ukweli kwa baadhi ya viongozi wa kijiji hicho ndipo alipoamuru kukamatwa kwa mwananchi huyo ili aende kituo cha polisi kwa mahojiano zaidi. 

Lakini mkuu wa mkoa Ally Hapi alimvua cheo cha kuwa mwenyekiti wa kamati ya maji ya kijiji hicho na kuteua kiongozi mwingine wa muda hadi pale mkutano wa kijiji utakapopitisha jina la kiongozi mpya. 

Hata hivyo viongozi wa kijiji kijiji hicho na wananchi walimuunga mkono mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi kwa uamuzi wa kumvua vyeo bwana Stephen Kalinga kwa kuongea uongo ambao ulitaka kuvuruga amani ya wananchi wa kijiji cha Rungemba. 

Aidha Hapi alitoa ahadi ya kuwa kutoa mifuko mia moja ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa jingo la hodi ya akina mama ikiwa ni kuunga mkono juhudi ambazo zinafanywa na wananchi wa kijiji cha Rungemba kuleta maendeleo na kuboresha sekta ya afya. 

Hapi aliongeza kwa kusema kuwa wananchi watakiwa kuendelea kujitolea katika shughuli za kimaendeleo kama kuiboresha zahanati hiyo hadi kufikia hadhi ya kuwa kituo cha afya lengo kuu likiwa ni kuendelea kuboresha sekta ya afya. 

“Naomba wananchi wengine wa moa wa Iringa kuiga mfano wa wananchi wa kijiji cha Rungemba kwa jitihada zao wanazozifanya kuhakikisha wanafanya shughuli za kimaendeleo kijijini kwao” alisema Hapi.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com