METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, September 25, 2018

MBUNGE JIMBO LA NYAMAGANA MTAA KWA MTAA KUSIKILIZA NA KUTATUA KERO ZA WANANCHI

Mbunge Jimbo la Nyamagana Mhe Stanislaus Mabula kabla na baada ya ziara zake za mrejesho wa Bunge la bajeti kwa wananchi kila Kata, sasa ameanza ziara ya Mtaa kwa Mtaa  katika mitaa yote yenye changamoto za muda mrefu na za muda mfupi.

Haya yamebainishwa na Mhe. Stanislaus Mabula alipowatembelea wananchi wa Mtaa wa Nyamayuki Kata ya Mahina kusikiliza malalamiko yaliyowasilishwa kwake  kupitia mikutano ya hadhara sanjari na maombi kupitia Ofisi yake. Miongoni mwa malalamiko na changamoto alizozipokea ni pamoja na miundo mbinu mibovu ya barabara ya Nyakurunduma iliyopo  Mtaa huo inayounganisha Kata tatu, ikiwemo Kata ya Mahina, Mkuyuni na  Butimba, Shida ya maji, changamoto za ardhi pamoja na Umeme. Akijibu hoja hizo Mhe. Mabula aliwaaahidi kuleta wataalum kutoka Halmashauri ya Jiji la Mwanza, TANESCO, TARURA na MWAUWASA siku ya alhamisi ili kutatua changamoto hizo ambazo zimekuwa sugu.

Akijibu hoja ya huduma ya Afya Mhe. Mabula amesema tayari serikali imeboresha huduma ya Afya na imedhamilia kufikisha huduma karibia na wananchi. Ambapo katika mwaka huu wa fedha Kata ya Mahina imepatiwa  shilingi 87,000,000.00 kukamilisha jengo lililojengwa katika Zahanati ya Kata  toka mwaka 2013 ili kujifungulia Wanawake wajawazito pamoja na chumba kwaajili ya kupumzikia Wazazi. Natayari kamati ya usimamizi inapitia ili kuanza kazi mara moja.

Mhe. Mabula kesho ataendelea na ziara hii Mtaa huo akiwa na wataalamu ili kupata suluhu ya kudumu, na kisha kesho kuywa atakuwa Kata ya Lwanimah kuwafikiwa wananchi wa maeneno ya Sawa, mitaa ya Nyamaranga, Igwambiti C pamoja na Shibahi.

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Nyamagana

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com