
Mwanariadha
Damian Christian wa Arusha (mbele) akiwaongoza wenzake Robert Francis wa
Singida aliyeshika nafasi ya pili na Hoja Samwel wa Simiyu wakichuana
vikali katika mbio za mita 1500.

Salma Ismail (392) kutoka Mwanza
ambaye alishinda mbio za mita 1500 wasichana akiwa mbele ya wenzake
Valaria charles (569) wa Singida ambaye alishika nafasi ya pili na Grace
Mpina (080) kutoka Geita ambaye alishika nafasi ya tatu mara baada ya
kumaliza mbio hizo leo asubuhi.

Washiriki wa mchezo wa riadha
fainali maalum za UMITASHUMTA wakikimbia mbio za mita 100 leo katika
viwanja vya chuo cha ualimu Mtwara
*****************
Na Mathew Kwembe, Mtwara
Wanariadha Damian Christian kutoka
mkoa wa Arusha na Salma Ismail wa Mwanza wameshinda medali za dhahabu
kwa wavulana na wasichana kwenye fainali za mbio za mita 1500
zilizofanyika leo katika viwanja vya chuo cha ualimu Mtwara.
Damian alitumia dakika 4:16:47
kumaliza mbio hizo huku akifuatiwa kwa karibu na Mwanariadha Robert
Francis kutoka Singida ambaye alitumia muda wa dakika 4:17:00, huku
nafasi ya tatu ikichukuliwa na Hoja Samwel wa Simiyu ambaye alitumia
dakika 4:19:88.
Kutokana na matokeo hayo Damian
amejinyakulia medali ya dhahabu, Robert atapata medali ya fedha ambapo
Hoja atapata medali ya shaba.
Kwa upande wa wasichana medali ya
dhahabu imechukuliwa na mwanariadha Salma Ismail wa Mwanza ambaye
alikimbia kwa muda wa dakika 4:46:65, ambapo medali ya fedha
ilichukuliwa na mwanariadha Valaria Charles wa Singida ambaye alishika
nafasi ya pili baada ya kutumia muda wa dakika 4:47:15 huku medali ya
shaba ilikwenda kwa mwanariadha Grace Mpina wa Geita aliyetumia muda wa
dakika 4:47:25.
Katika mashindano ya kuruka juu
ambayo yalifanyika leo katika viwanja vya chuo cha ualimu Mtwara
wanariadha watatu wa kutoka mikoa ya Mara, Kilimanjaro na Geita
wamejinyakulia medali za dhahabu, fedha na shaba.
Nafasi ya kwanza ilishikwa na
Mwanariadha Yunus Chacha Mondera wa Mara ambaye aliruka urefu wa mita 1
na sentimita 38, nafasi ya pili imechukuliwa na mwanariadha Witness
Martin kutoka Kilimanjaro ambaye aliruka urefu wa mita 1 na sentimita
37, huku nafasi ya tatu ilichukuliwa na Mectrida Kasandhao wa Geita.
Matokeo hayo yamewawezesha wanariadha Yunus, Witnes na Mectrida
kujinyakulia medali za dhahabu, fedha na shaba.
0 comments:
Post a Comment