
Na Datus Mahendeka Polisi Iringa
Wafanyakazi wawili wa Tarura Mkoa wa Songwe wamefariki kwa ajali ya uso kwa uso wakitokea Mkoa wa Iringa wakielekea Dodoma.
Waliofariki ni Lodrick Richard,
miaka 35,kabila Mchaga mkazi wa Dar es Salaam ambaye ni dereva wa gari
waliokuwa wakisafiria pamoja na Joyce Enezer, miaka 45, kabila Mchag
mkazi wa Moshi.
Akizungumza na waandishi wa
habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Kamishna Msaidizi wa Polisi
Juma Bwire amesema ajali hiyo imetokea Juni 25 majira ya saa 11:45
alfajiri.
“Wafanyakazi hawa waliokuwa
wanaenda Dodoma kikazi ambapo waliofika maeneo ya Izazi Tarafa ya
Isimani wakiwa kwenye gari lenye namba za kusajili Stl 3807 aina ya
Toyota Hilux mali ya Tarura walikutana na Fuso.
Kwa mujibu wa Kamanda Bwire, Fuso
hilo lenye namba za usajili T 146 BAZ mali ya Wilson Msenga
likiendeshwa na mtu kwenye jina moja la Amos ambalo lilikuwa likitokea
Dodoma kuja Iringa ambapo waligongana uso kwa uso ambao miili yao
imekabidhiwa kwa Meneja wa Tarura Manispaa ya Iringa ili kupelekwa
Dodoma kwa tararibu zingine.
Aidha alitaja majeruhi wa ajali
hiyo kuwa ni Ernest Mgeni, miaka 49, kabila Mkinga, Gervas Myovela,
miaka 44, kabila Mhehe na Jamadin Mikata, miaka 32 wote wakazi wa Mbozi
ambao wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa Iringa kwa matibabu.
Alisema dereva wa Fuso anatafutwa
baada ya kulimbia mara baada ya ajali hiyo, kutokana na uzembe wake wa
kuhama upande wake wa barabara.
0 comments:
Post a Comment