Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Khasim Majaliwa akihutubia wakati wa ufunguzi wa
Mkutano wa Mawaziri wa SADC wa Sekta ya TEHAMA, Habari, Uchukuzi na Hali
ya Hewa wanakutana kwa siku mbili kuanzia leo Septemba 19-20, 2019
jijini Dar es Salaam. Picha zote na Matokeo Chanya+.
……………………………………..
Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim
Majaliwa amewataka mawaziri wanaoshughulikia tehama, habari, uchukuzi na
hali ya hewa kutoka nchi 16 wanachama wa Jumuiya ya maendeleo ya nchi
kusini mwa Afrika (SADC) kusimamia maendeleo ya teknolojia.
Hayo ameyasema leo Septemba 19,
2019 wakati akizindua mkutano wa mawaziri hao, ambao ulitanguliwa na
majadiliano yaliyowakutanisha makatibu wakuu na viongozi wa juu
wanaoshughulikia sekta hizo kutoka nchi wanachama ambao walikaa kwa siku
tatu kabla ya baraza la mawaziri lililoanza juzi.
Kati ya maagizo hayo ni pamoja na
kushughulikia masuala ya mtandao, mkakati wa posta kuurejesha katika
teknolojia ya sasa, kuondoa vikwazo vya kibiashara kati ya nchi na nchi,
maendeleo kiteknolojia.
Katika hotuba yake, amesema mkutano huo ni wa kwanza kisekta baada ya mkutano wa awali.
“Ni matarajio yetu kuwa mkutano
huu utajadili utekelezaji wa mikakati mbalimbali, programu na miradi
kama ilivyoainishwa kwenye mpango mkakati elekezi wa maendeleo ya sadc
wa mwaka 2015 mpaka 2030.
“Pamoja na mpango kabambe wa
maendeleo ya miundombinu wa mwaka 2019 mpaka 2023 utajadili na kufanya
tathmini na kuja na njia mbadala ya utekelezaji uchumi kikanda ili
kuharakishwa,” alisema.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhandisi Isack Kamwelwe
akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mawaziri wa SADC wa Sekta
ya TEHAMA, Habari, Uchukuzi na Hali ya Hewa wanakutana kuanzia leo
Septemba 19-20, 2019 jijini Dar es Salaam.
Nae Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Isack Kamwelwe amesema mkutano huo umewakutanisha
wataalamu wa tehama, hali ya hema, uchukuzi na mawasiliano kutoka nchi
wanachama pamoja na wakuu wa taasisi na mashirika pamoja na viongozi
waliopo katika sekta binafsi nchi za SADC.
Amesema katika majadiliano wote
kwa pamoja wanazo changamoto mbalimbali wanazoshabihiana katika hali ya
hewa, miundombinu mbalimbali ambayo inarudisha nyuma nchi kujikomboa
kiuchumi na kuwa wana mjadala wa pamoja katika kuzileta nchi kiuchumi
kwa manufaa ya wananchi wa ukanda huu.
“Kipindi cha asubuhi tumeshaanza
na tumeendelea na mjadala wajumbe walileta hoja mbalimbali
kushuhghulikia reli, majanga na hali ya hewa, manufaa ya teknolojia ya
habari na mawasiliano katika kuboresha uchumi na maisha ya wana SADC.
“Aidha wataalamu kutoka sekta za
kibenki maendeleo ya Afrika na Benki ya Maendeleo ya Afrika Kusini
wameelezea uwezo wao katika kusaidia ujenzi na uboreshaji wa miundombinu
katika sadc, lakini pia maeneo mengine yaliyoangaziwa ni pamoja na
ushirikishwaji wa wanawake na sekta binafsi,” amesema Kamwelwe.
Mkurugenzi wa Miundombinu wa
SADC, Mapolao Mokoena amesema mkutano huo utaweza kusaidia uelewa wa
watendaji wa Serikali kujua njia ya kupita katika kuifanya jumuiya
ifikie malengo yake hasa katika miundombinu.
Mawaziri wa SADC wa Sekta ya
TEHAMA, Habari, Uchukuzi na Hali ya Hewa wanakutana kwa siku mbili
kuanzia leo Septemba 19-20, 2019 jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Khasim Majaliwa akiwa na Mkurugenzi wa Miundombinu
wa SADC, Mapolao Mokoena (kushoto).
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhandisi Isack Kamwelwe
(wa kwanza kushoto) akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (katikati) pamoja
na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Sekta ya Uchukuzi Bw. Leonard
Chamriho.
Mawaziri wa SADC wa Sekta ya
TEHAMA, Habari, Uchukuzi na Hali ya Hewa wanakutana kwa siku mbili
kuanzia leo Septemba 19-20, 2019 jijini Dar es Salaam.
Meza kuu.
Meza kuu wakiendelea na majadiliano.Meza kuu.
Mawaziri wa SADC wa Sekta ya TEHAMA, Habari, Uchukuzi na Hali ya Hewa wakiuliza maswali wakati wa majadiliano.
Majadiliano yakiendelea…
Mawaziri wa SADC wa Sekta ya
TEHAMA, Habari, Uchukuzi na Hali ya Hewa wanakutana kwa siku mbili
kuanzia leo Septemba 19-20, 2019 jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment