Waziri wa Madini Doto Biteko wa
nne kulia akitembelea eneo la uzalishaji katika mgodi wa STAMIGOLD. Wa
tatu kulia ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Biharamumo ambae ni Kaimu Mkuu
wa Wilaya Agness Alex na wa pili kulia ni meneja Mkuu wa Mgodi Mhandisi
Gray Shamika.
Waziri wa Madini Doto Biteko wa
tatu kulia akimsikiliza Kamishna wa Tume ya Madini Dkt. Athanas
Machiyeki wakiwa kwenye eneo la Mgodi wa STAMIGOLD.
…………………….
Na Issa Mtuwa – Biharamulo Kagera.
Waziri wa Madini Doto Biteko
ameagiza mgodi wa dhahabu wa Mistamigold unaomilikiwa na Shirika la
madini la Taifa STAMICO kuanzia Mwezi Desemba 2019 dhahabu inayozalishwa
mgodini hapo iuzwe kwenye masoko ya dhahabu ya hapa nchini hususani
kwenye soko la Biharamulo.
Biteko amesema hayo leo tarehe
19/09/2019 alipotembelea mgodi huo uliopo wilaya ya Biharamulo. Amesema
aiwezekani serikali ihimize dhahabu yote iuzwe kwenye masoko ya ndani
wakati mgodi wa serikali dhahabu yake inazwa Ususwi.
“Naagia kuanzia Desemba mwaka huu,
dhahabu yote inayo zalishwa katika mgodi huu iuzwe kwenye masoko ya
ndani, mara baada ya mkataba wenu kuisha mwezi Novemba. Kwa kufanya
hivyo gharama isiyo ya lazima mtaiepuka.” amesema Biteko.
Wakati huo huo Biteko amemuagiza
Afisa Madini Mkazi mkoa wa Kagera Mhandisi Lucas Mlekwa kuzifuta leseni
159 ambazo haziendelezwi ili zigawiwe kwa wanaohitaji kuendeleza leseni
hizo na serikali ipate mapato yake.
Awali, akitoa taarifa ya madini
mkoa wa Kagera Mhandisi Mlekwa pamoja na mambo mengine alimwambia Waziri
kuwa kuna changamoto nyingi kwenye mkoa wake pamoja na nyingine ni
uwepo wa leseni nyingi zisizo endelezwa.
Ameongeza kuwa kila anapo jaribu kufanya mawasiliano na wamiliki wa leseni hizo ili waendeleze hawapatikani.
Kwa upande wake, Meneja Mkuu wa
mgodi wa STAMIGOLD Mhandisi Gray Shamika amemueleza Waziri jinsi mgodi
unavyo endeshwa na kwa sasa wanajiendesha wenyewe kwa kugharamia gharama
zote ikiwemo kulipa mishara ya watumishi na kulipa wazabuni. Amesema
taarifa za kijiolojia zinaonyesha kuwa mgodi bado utaendelea kuishi pamoja na uwepo wa changamoto mbalimbali zikiwemo za madeni.
Akitoa taarifa yake kwa Waziri
Mhandisi Shamika amesema, kwa sasa Mgodi upo kwenye utaratibu kuanzisha
mradi wa kuchenjua Visusu (Tailings) mradi utakao upa uhai wa mgodi hadi
miaka 7-10 ijayo. Kuhusu kupunguza gharama za uzalishaji Shamika
amesema mgodi umepunguza gharama za uzalishaji kutoka 1800 hadi 940 kwa
wakia (Ounce) moja.
Kufuatia taarifa hiyo, Waziri
Biteko ameupongeza uongozi na wafanyakazi wote kwa hatua hiyo na
kuwaomba kuendela kupunguza gharama hiyo angalau kufikia 800 kwa wakia.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji wa STAMICO Brigadia Jenerali Silvester Ghuliko amesema wako
teyari kutekeleza maagizo ya Waziri na walisha anza kujipanga kutekeleza
maagizo hayo hususani kuanza kuuza dhahabu katika soko la ndani mara
baada ya mkataba wa kuuza dhahabu nje kumalizika mwezi Novemba mwaka
huu.
Akimkaribisha Waziri wa Madini,
Katibu Tawala wa Wilaya ya Biharamumo ambae ni Kaimu Mkuu wa Wilaya hiyo
Agness Alex amemwambia waziri hali halisi ya sekta ya madini wilayani
humo pamoja na changamoto mbalimbali ikiwemo deni la Halmashauri yake
kwa mgodi huo.
Kufuatia hoja hiyo ya deni la
Halmashauri, Biteko amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Biharamulo
Ionde Ng’ahala kutuma timu ya wahasibu wake kwenda STAMIGOLD kukaa na
uongozi kupitia deni hilo na kuhakiki na kukubaliana namna ya kulipa
deni hilo.
0 comments:
Post a Comment