Mkuu wa kitengo cha Masoko na Ubunifu Bwana. Deogratius Lazari Mosha akifafanua jambo kwa Waandishi wa habari (hawapo pichani)
Kampuni ya Maxcom Africa
(Maxmalipo) inawakaribisha watanzania kushiriki manunuzi ya hisa za
makampuni yaliyoorodheshwa kwenye Soko la hisa la Dar es salaam(DSE)
kwa njia ya mtandao (simu za kiganjani) na kufanya malipo kupitia kwa
mawakala wa Maxmalipo waliopo nchi nzima Tanzania.
Mkuu wa kitengo cha Masoko na
Ubunifu Bwana. Deogratius Lazari Mosha, Leo 13/03/2017 amewaambia
waandishi wa habari kwamba Maxcom Africa (Maxmalipo) ikishirikiana na
soko la hisa la Dar es Salaam(DSE) kwa kutumia mfumo madhubuti wa simu
za viganjani unamwezesha Mtanzania kuweza kushiriki kwenye Manunuzi ya
hisa za makampuni yaliyoorodheshwa kwenye soko la awali la mitaji
(primary markets ) kwa kupiga *150*36#, ameongeza kwamba baadhi ya
makampuni hayo kwa sasa ni Vodacom na TCCIA.
Akifafanua hili Bw. Deogratius
Lazari amesema ili Mtanzania aweze kushiriki Manunuzi ya hisa kwa mfumo
huu anatakiwa kubonyeza *150*36# kisha ataingia kwenye Menyu ya soko la
hisa na Kuchagua IPO kisha atachagua kampuni anayotaka kununua hisa,
baada ya kufanya hivyo mteja atalazimika kujisajili na kisha atapata
nafasi ya kuainisha idadi ya hisa anazohitaji(zisizo pungua 100 katika
awamu ya kwanza).
Bw. Deogratius Lazari
ameongeza kwamba baada ya hatua ya uanishaji wa hisa, mteja atapokea
ujumbe mfupi wa simu kutoka DSE wenye nambari ya kumbukumbu ya malipo,
idadi ya hisa na kiasi anachotakiwa kulipia. Ili kukamilisha malipo
haya mteja atatakiwa kufika kwa wakala yeyote wa Maxmalipo aliye karibu
naye na kufanya malipo kama ilivyo ainishwa kwenye ujumbe aliopokea
kwenye simu yake. Mteja anahimizwa kuhakikisha kwamba anapatiwa risiti
pindi anapolipia hisa kwa mawakala wa Maxmalipo ili kutunza kumbu kumbu
zake.
Kwa kuongezea Bw. Deogratius
Lazari ameeleza kwamba mfumo huu rafiki unamwezesha mteja kushiriki
manunuzi ya hisa kadiri ya uwezo wake (Mfano, Mteja Anaweza kila siku
akanunua hisa 100 kulingana na kipato chake au zaidi). Pamoja na mwakala
wa Maxmalipo mteja anaweza kulipia kwa kutumia mitandao ya simu.
Mfumo huu wa kununua hisa kwa
simu za kiganjani ( *150*36#) umetengenezwa na kampuni ya kitanzania ya
Maxcom Africa (Maxmalipo) ikishirikiana na Soko la hisa la Dar es
Salaam(DSE) na ni mfumo rasmi wa kuuza na kununua hisa kwenye soko la
hisa .
Bw. Deogratius Lazari ametoa wito kwa
watanzania kushiriki ununuzi wa hisa kwa njia ya simu ya kiganjani na
kuhakikisha wanafanya malipo mapema kupitia kwa mawakala wa Maxmalipo
walioko nchi nzima takribani Mawakala Elfu kumi na sita .
0 comments:
Post a Comment