METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, May 20, 2025

DC WILAYA YA ARUSHA AWATAKA WAFANYABIASHARA KUSHIRIKIANA NA TRA KATIKA MASUALA YA KODI.









WAZOHURU ARUSHA:

Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Joseph Modestus Mkude amewataka wafanyabiashara Wilayani hapo kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania ikiwemo kulipa kodi zao stahiki kwa hiari na kwa wakati.

Mkuu wa Wilaya hiyo ameyasema hayo tarehe 19 Mei, 2025 wakati alipokutana na Maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambao wapo mkoani Arusha kwa ajili ya kampeni ya elimu kwa Mlipakodi ya mlango kwa mlango.

Aidha, amesema kuwa kodi mbalimbali zinazolipwa na wananchi wa eneo hilo ndizo zinasaidia katika kuleta maendeleo nchini ikiwemo katika sekta ya elimu, afya na ujenzi wa miundombinu mbalimbali nchini.

Baadhi ya wafanyabiashara wilayani hapo wameiomba TRA kuendeleza elimu ya kodi ikiwemo kuskiliza kero zao za kikodi na wameahidi kuonesha ushirikiano kwa TRA ili waweze kulipa kodi zao stahiki.

Kampeni ya elimu kwa Mlipakodi ya mlango kwa mlango ni zoezi endelevu linalofanywa na TRA katika mikoa mbalimbali nchini kwa lengo la kuwaelimisha walipakodi kuhusu masuala ya kodi ili waweze kulipa kodi zao kwa hiari kwa ajili ya maendeleo ya nchi ambapo kwa sasa kampeni hiyo inafanyika katika Mikoa ya Arusha, Iringa na Pwani.

Share:

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2025 WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com