Kufuatia maamuzi ya Mkutano Mkuu wa CCM Taifa kuhusu mapendekezo ya
marekebisho ya katiba ya CCM ya mwaka 1977 toleo 2012, moja ya maamuzi
yaliyo fanyika ni kulifanya Shirikisho kutoka kwenye hadhi ya Mkoa
Maalum (kwa mujibu wa katiba ya CCM, fungu la VI, 89 (1)(b)) kuwa idara
ya "Vyuo na Vyuo Vikuu" ndani ya UVCCM (kwa mujibu wa marekebisho ya
katiba) na (marekebisho ya kanuni za UVCCM, ibara 107).
Kwa mujibu wa marekebisho ya katiba, mabadiliko haya yanalenga kurekebisha muundo, mfumo, uongozi, utendaji na mengineyo. Kwa upande wa Shirikisho;
"Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu ni chombo kipya chenye lengo la kuwashirikisha wanafunzi wasomi katika kuwalea kisiasa na kizalendo wakati wakiwa chuoni na baada ya kuhitimu. Lengo hilo zuri limeshindwa kutekelezeka baada ya kuchomoza changamoto nyingi. Ili kukabiliana na changamoto hizo, Chama kimeutazama upya muundo wa Shirikisho ndani ya CCM na kuamua kuifanya iwe Idara ya Vyuo vya Elimu ya Juu na Sekondari itakayoongozwa na Umoja wa Vijana wa CCM."
Kwa mujibu wa Katiba ya CCM, fungu la VII, 104 (2) inayosema, "Mkutano Mkuu wa CCM wa Taifa utakuwa ndicho Kikao Kikuu cha CCM kupita vyote na ndicho kitakachokuwa na madaraka ya mwisho." Kufuatia maamuzi ya Mkutano Mkuu uliokaa 12. March. 2017 hivyo Shirikisho kwa sasa liko chini ya UVCCM.
Baada ya maamuzi ya Mkutano Mkuu, wajumbe wa Kamati ya Uratibu ya Shirikisho Taifa, chini ya Mwenyekiti wake, Mh Zainab Abdallah Issa na uongozi mzima umefanya uamuzi wa kung'atuka rasmi ili kuendana na mabadiliko hayo. Wajumbe wa kamati hiyo ni viongozi wote wa Shirikisho taifa kama wafuatao:
1. M/kiti Shirikisho Taifa (Mnec)
2. Makamu M/Kiti (Mnec)
3. Katibu Mtendaji Mkuu (Mnec)
4. Wanec 3 ( 2 - Bara, 1 - Zanzibar)
5. Katibu wa Siasa na Uenezi Taifa
6. Katibu Uchumi na Fedha Taifa
7. Katibu Hamasa Taifa
8. Mkuu wa Idara ya Elimu, Tafiti na Uongozi
9. Mkuu wa Idara ya Uwezeshaji
10. Mkuu wa Idara ya Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa.
Sambamba na hao, wakuu wa madawati yote (Dawati la Mikopo, Dawati la Ajira, Dawati la Miradi, Dawati la Diaspora na Dawati la IT) na wao wanalazimika kuendana na mabadiliko hayo.
Kwa historia fupi, Shirikisho liliundwa rasmi 14/05/2012, na chaguzi za kuwapata viongozi wa kitaifa zilifanyika 25/05/2015 ambapo kwa mujibu wa kanuni za Shirikisho (Ibara ya 16 - Kiongozi yeyote wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu aliyechaguliwa kwa mujibu wa Kanuni hizi atashika madaraka yake kwa muda wa miaka mitatu ya uongozi). Hivyo ukomo wa Kamati ya Uratibu ulipaswa kuwa 25/05/2018.
Sababu za Kuundwa kwa Shirikisho.
A} Kabla ya kuundwa kwa Shirikisho, wasomi wa vyuo vikuu walikuwa chini ya "Idara ya Sekondari na Vyuo Vikuu" ndani ya UVCCM. Lakini kutokana na kuungwa mkono na kundi hili kubwa la wasomi, Chama kiliona umuhimu wa kutenganisha kundi hili kuwa taasisi inayo jitegemea ili kuwa na chombo madhubuti kinacho unganisha fikra na vitendo vya vijana wasomi wa Vyuo Vikuu.
B) Wanafunzi wa Vyuo Vikuu walikosa uwakilishi wa moja kwa moja ndani ya Chama hasa katika kuwasilisha changamoto zao. Hivyo, taasisi hii iliundwa kwa ajili ya kuwapa nguvu wasomi wa Vyuo Vikuu kuweza kuwasiliana moja kwa moja na uongozi wa Chama.
C) Kusimamia harakati za kisiasa na za kitaaluma za wanafunzi wa Vyuo Vikuu na kuongeza idadi ya wasomi wa Vyuo Vikuu wanao kiunga mkono Chama Cha Mapinduzi.
Mafanikio ya Msingi ya Shirikisho.
1. Kuwaunganisha vijana wa Vyuo Vikuu na kuongeza idadi ya wasomi wa Vyuo Vikuu wanao fungamana na Itikadi ya CCM
2. Kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi Mkuu wa 2015, katika kampeni za Rais, Wabunge na Madiwani.
3. Kuleta ushindani kwa UVCCM na kuifanya Jumuiya kujiimarisha zaidi.
4. Kuoka viongozi wa Chama na Serikali.
5. Kufanya tafiti mbalimbali na kukabiliana na changamoto za wanafunzi wa Vyuo Vikuu.
Sababu za Mabadiliko haya Mapya.
Kamati ya Uratibu inaitaka UVCCM kupitia upya mambo yafuatayo:
1. Shirikisho limetambulika kama "Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu" kwa mujibu wa marekebisho ya kanuni za UVCCM. Lakini bado kanuni hizi hazijatambua Idara zilizokuwa ndani ya Shirikisho zitakuwa na nafasi gani ndani ya Jumuiya. Ni lazima Idara hizi na madawati yake yatafutiwe utaratibu mpya ndani ya kanuni ili kuleta tija na ufanisi wa kundi hili la vijana wa Vyuo Vikuu.
2. Kuondokana na utendaji wa kianalogia na kurudi kwenye mfumo wa kidigitali utakao ongeza ufanisi, kutunza kumbukumbu na kupunguza gharama. Kwa mfano: Kutumia secured mailing system ya mawasiliano badala ya fax na barua, badala ya kutumia gharama kubwa ya kulipana posho za malazi na usafiri baadhi ya vikao vinaweza kufanyika kwa njia ya mtandao (Online tele conference calls) na kuandaa "Database" maalum itakayo tambua Vijana wa CCM nchi nzima na taarifa zao.
3. Tuifanye Jumuiya kuwa ya wanachama na sio viongozi kwa kuyafikia makundi yote ya vijana na kuskiliza changamoto zao. Jumuiya isiishi kipindi cha Uchaguzi bali ionekane kwa vijana kila siku. Kwa kufanya hivyo tutaongeza kundi kubwa la vijana watakao kipenda chama.
Mwisho, kwa kipindi hiki cha mpito, Ndugu Daniel Zenda ataendelea kuwapa ushirikiano katika kuwafikia wanafunzi wa Vyuo Vikuu mpaka pale uteuzi wa Mkuu wa Idara utakapo fanyika kwa mujibu wa Kanuni zenu. Tunashauri zoezi hili lifanyike mapema ili kuondokana na sintofahamu zisizo za lazima. Tunampongeza sana M/Kiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzania - Dr John Pombe Magufuli kwa kuleta mageuzi makubwa ndani ya CCM. Tutaendelea kumuunga mkono kwa maslahi mapama ya Chama Chetu.
"Mimi nang'atuka, ila naendelea kuamini bila ya CCM Madhubuti nchi yetu itayumba - Mwl Nyerere; Agosti 1990."
Kidumu Chama Cha Mapinduzi.
Imetolewa na:
Kamati ya Uratibu,
Shirikisho Taifa.
14/03/2017

- Chama kinaamini zaidi ya 90% ya wanafunzi wa Vyuo Vikuu ni Vijana, hivyo kuwa sehemu ya UVCCM kutaleta tija na ufanisi zaidi na kuwaunganisha Vijana kuwa kitu kimoja na kuendana na kauli mbiu UMOJA NI USHINDI.
- Katika kuijenga CCM Mpya, moja ya mikakati ni pamoja na kupunguza muundo na taasisi za chama. Kuwa na Chama chenye muundo mdogo utakaoleta tija na kupunguza gharama.
- Katika mageuzi yanayo tarajiwa kufanyika ndani ya CCM, ni pamoja na kufanya mageuzi ndani ya Jumuiya zake. Chama kinaamini kuwaleta Vijana wa Vyuo Vikuu ndani ya UVCCM ni moja ya mageuzi ndani ya Jumuiya na kuifanya Jumuiya kubeba taswira mpya na kutoa muelekeo mpya.
- Mageuzi haya ni lazima yaendane na baadhi ya viongozi na watendaji kujitoa muhanga (make a sacrifice) ili kuijenga Jumuiya Mpya. Kuna haja ya kubadilisha safu nzima ya watendaji wa Jumuiya wanaotokana na mfumo uliopita hasa katika ngazi ya taifa, ili kupata watendaji wapya, watakao weka usawa wa makundi yote ya vijana na kutoa muelekeo mpya wa Jumuiya.
- Baada ya kuwawajibisha wasaliti ndani ya Chama, tunakiomba Chama kiitazame Jumuiya hii kabla ya kuelekea kwenye Uchaguzi. Wasaliti wote wawajibishwe ili tuondokane na makando kando kipindi cha Uchaguzi.
- Katika Uchaguzi huu, hasa ndani ya Jumuiya, Chama kitoe fomu maalum zitakazo ainisha mali anazo miliki mgombea na alipo zitoa, ili tuweze kuwawajibisha viongozi watakao kikuka maadili ya uongozi kwa Mujibu wa Kanuni za Maadili ya Viongozi. Zoezi hili liambatane sambamba na watendaji wote wa Jumuiya.
Kamati ya Uratibu inaitaka UVCCM kupitia upya mambo yafuatayo:
1. Shirikisho limetambulika kama "Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu" kwa mujibu wa marekebisho ya kanuni za UVCCM. Lakini bado kanuni hizi hazijatambua Idara zilizokuwa ndani ya Shirikisho zitakuwa na nafasi gani ndani ya Jumuiya. Ni lazima Idara hizi na madawati yake yatafutiwe utaratibu mpya ndani ya kanuni ili kuleta tija na ufanisi wa kundi hili la vijana wa Vyuo Vikuu.
2. Kuondokana na utendaji wa kianalogia na kurudi kwenye mfumo wa kidigitali utakao ongeza ufanisi, kutunza kumbukumbu na kupunguza gharama. Kwa mfano: Kutumia secured mailing system ya mawasiliano badala ya fax na barua, badala ya kutumia gharama kubwa ya kulipana posho za malazi na usafiri baadhi ya vikao vinaweza kufanyika kwa njia ya mtandao (Online tele conference calls) na kuandaa "Database" maalum itakayo tambua Vijana wa CCM nchi nzima na taarifa zao.
3. Tuifanye Jumuiya kuwa ya wanachama na sio viongozi kwa kuyafikia makundi yote ya vijana na kuskiliza changamoto zao. Jumuiya isiishi kipindi cha Uchaguzi bali ionekane kwa vijana kila siku. Kwa kufanya hivyo tutaongeza kundi kubwa la vijana watakao kipenda chama.
Mwisho, kwa kipindi hiki cha mpito, Ndugu Daniel Zenda ataendelea kuwapa ushirikiano katika kuwafikia wanafunzi wa Vyuo Vikuu mpaka pale uteuzi wa Mkuu wa Idara utakapo fanyika kwa mujibu wa Kanuni zenu. Tunashauri zoezi hili lifanyike mapema ili kuondokana na sintofahamu zisizo za lazima. Tunampongeza sana M/Kiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzania - Dr John Pombe Magufuli kwa kuleta mageuzi makubwa ndani ya CCM. Tutaendelea kumuunga mkono kwa maslahi mapama ya Chama Chetu.
"Mimi nang'atuka, ila naendelea kuamini bila ya CCM Madhubuti nchi yetu itayumba - Mwl Nyerere; Agosti 1990."
Kidumu Chama Cha Mapinduzi.
Imetolewa na:
Kamati ya Uratibu,
Shirikisho Taifa.
14/03/2017
0 comments:
Post a Comment