
Mhandisi Suk-Joo Lee kutoka katika
kampuni ya Yooshin Engineering akimueleza Rais Magufuri namna ujenzi wa
daraja la Tanzanite ukiendelea kufanyika

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Magufuri akiwa katika eneo ambalo ujenzi wa daraja la
Tanzanite ukiendelea baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika ujenzi
huo.
***********************
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 24 Juni, 2019
amefanya ziara ya kushtukiza katika mradi wa ujenzi wa daraja
linalokatiza baharini kwa kuunganisha maeneo ya Aga Khan na Coco Beach
Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujionea maendeleo ya ujenzi wa daraja
hilo.
Mhe. Rais Magufuli ameshuhudia shughuli za ujenzi zikiendelea
vizuri ambapo mkandarasi ambaye ni kampuni ya GS Engineering ya Korea
anakamilisha kuunganisha daraja la muda litakalomwezesha kuanza ujenzi
wa nguzo za daraja. Kwa ujumla kazi imefikia asilimia 10.12.
Akiwa katika mradi huo Mhe. Rais Magufuli amekutana na Mhandisi
Mshauri kutoka kampuni ya Yooshin Engineering Mhandisi Suk-Joo Lee na
kumuelezea kufurahishwa kwake na maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo
ambalo linatarajiwa kusaidia kupunguza msongamano wa magari kutoka na
kuingia katikati ya Jiji la Dar es Salaam.
Nae Bw. Suk-Joo Lee ameelezea kufurahishwa kwake kufanya kazi Tanzania na ameahidi kuwa kazi hiyo itakwenda vizuri.
Daraja hilo litakuwa na urefu wa kilometa 1.03 na barabara za
kuunganisha zenye urefu wa kilometa 6.23. Ujenzi wake unahusisha ujenzi
wa nguzo za msingi zenye urefu wa kati ya meta 14 na 65 na utagharimu
takribani shilingi Bilioni 255.
Daraja hilo limependekezwa kuitwa Tanzanite Bridge na litakamilika Oktoba 2021.
0 comments:
Post a Comment