Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka (katikati), Katibu
Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante ole Gabriel
(kushoto), na Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya uchapishaji wa Magazeti ya
serikali (TSN) Tanzania Standard Newspaper Dkt Jim Yonazi (kulia) wakisikiliza
maelezo mbalimbali katika Kongamano hilo
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante ole Gabriel
akisisitiza umuhimu wa Viwanda nchini Tanzanai
Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Masoko kutoka TIB Corporate
Bank Ltd Bi Theresia Soka (kulia) akiwa na Zacharia Kicharo Meneja wa TIB Development
Bank Ltd Lake Zone wakifatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi katika ufunguzi
wa Kongamano la Jukwaa la Biashara Mkoani Simiyu
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu Ndg Jumanne Sagin
akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka
kuzungumza na wafanyabiashara na wawekezaji waliojitokeza katika kongamano la
uwekezaji
Kutoka Kulia ni Emmanuely Gungu Silanga Mwenyekiti wa
Viwanda Mkoa wa Simiyu, Peter Bahini Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wataalamu
na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato (ATAPE) Kanda ya Nyanza
Kusini (SNC) na Emmanuely Lupembe Mwenyekiti wa Chama cha Wataalamu na
Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato (ATAPE) Kanda ya Nyanza Kusini
(SNC wakifatilia kwa makini kongamano la uwekezaji Mkoani Simiyu
Meza kuu wakifatilia mjadala katika Kongamano la Jukwaa la Biashara Simiyu
Kwaya ya AIC Bariadi, Simiyu wakiimba wimbo maalumu kwa ajili ya kuhamasisha ulipaji kodi
Mhariri
Mtendaji wa Kampuni ya uchapishaji wa Magazeti ya serikali (TSN) Tanzania
Standard Newspaper Dkt Jim Yonazi akisisitiza akielezea dhamira ya TSN kuamua kufanya kongamano hilo kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu
Mbunge wa Jimbo la Itilima Njalu Silanga ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Mkoani Simiyu akitoa salamu zake za pongezi kwa ufanikishaji wa kongamano hiloKatikati ni Emmanuely Gungu Silanga Mwenyekiti wa Viwanda Mkoa wa Simiyu akifuatilia kwa makini Kongamano
Wafanyakazi wa Kampuni ya uchapishaji wa Magazeti ya serikali (TSN) Tanzania Standard Newspaper
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka
Kutoka Kulia ni Mtafiti Mwandamizi (TSN) Bw Akim Joseph, Afisa masoko Mwandamizi (TSN) Goodluck Chuwa, Mwakilishi wa TSN Kanda ya ziiwa Patrice Simbachawene na Meneja wa Masoko na Mauzo wa TSN Bw Januarius MagangaMbunge wa Busega Mkoani Simiyu Mhe Raphael Chegeni akitoa salamu za shukrani kwa kufanikiwa kwa kongamano hilo
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante ole Gabriel
(kushoto), na Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya uchapishaji wa Magazeti ya
serikali (TSN) Tanzania Standard Newspaper Dkt Jim Yonazi (kulia) wakiteta jambo wakati wa Kongamano
Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Masoko kutoka TIB Corporate
Bank Ltd Bi Theresia Soka akiwasilisha MadaMhariri Mtendaji wa www.wazo-huru.blogspot.com Ndg Mathias Canal akiendelea na kazi ya kuhabarisha kuhusu kongamano hilo
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa mlipa kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw Richard Kayombo akielezea namna ya ukusanyaji Mapato
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka akiwa katika picha ya pamoja na wadau wawezeshaji wa Kongamano hilo
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka akiwa katika picha ya pamoja na wawekezaji Mkoani Simiyu
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa
Kampuni ya uchapishaji wa Magazeti ya serikali (TSN) Tanzania Standard Newspaper
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka akiwa katika picha ya pamoja na Waimbaji wa Kwaya ya AIC Bariadi
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka akiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari walioshiriki kuhabarisha kuhusu Kongamano hilo
Na Mathias Canal,
Simiyu
Wafanyabiashara na wadau wa Mkoa wa Simiyu wametakiwa kutumia
fursa za uwekezaji wa biashara hususani katika kuwekeza kwenye viwanda kwani
mipango mingi inayopangwa na serikali inatoa fursa zaidi kwa wawekezaji wa
ndani ya nchi jambo ambalo litaifanya Tanzania kuondokana na umasikini kutokana
na fursa zilizopo.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony
Mtaka wakati akifungua Jukwaa la Biashara Mkoani Simiyu lililofanyika katika
Ukumbi wa Parokia ya Mtakatifu John lililopo katika Halmashauri ya Wilaya ya
Bariadi.
Rc Mtaka amesema kuwa Katika kuchochea na kuleta
maendeleo kwa wananchi katika Mkoa wa
Simiyu uongozi wa Mkoa huo una dhamira ya dhati kuwafanya wananchi wake kuingia
katika ramani ya Mkoa unaotumainiwa nchini.
“Sisi viongozi kwa kushirikiana na wananchi tunapaswa
kutumia Busara nyingi, Hekima na Utii ili kuimarisha utendaji katika maendeleo
ya Mkoa kwa kujitokeza kwenye shughuli za maendeleo pasina kutumia majungu
ambayo yatadhoofisha maendeleo” Alisisitiza Mhe Mtaka
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Profesa Elisante ole
Gabriel amewasihi wananachi ambao ni wafanyabiashara na wawekezaji katika Mkoa
wa Simiyu na wale wanaotaka kuwekeza Mkoani humo kufanya biashara na kuhakikisha
wanalipa kodi kwa mujibu wa sheria kwani wasipofanya hivyo biashara zao
haziwezi kuwa na maendeleo kwani watakuwa wameenda kinyume na mamlaka ya Mungu
inayoagiza kulipa kodi.
Prf Gabriel amebainisha hayo huku akihuisha na maneno
yaliyoandikwa katika Biblia Takatifu kwenye Kitabu cha Warumi 13:1-7 ambayo
inaeleza vyema kwamba Mtu wa kodi apewe kodi na Mtu wa Ushuru apewe ushuru
hivyo wafanyabiashara hao wanapaswa kutii mamlaka iliyo kuu kwa maana hakuna
mamlaka isiyotoka kwa Mungu.
Amesema Uongozi wa Mkoa wa Simiyu kupitia Mkuu wa Mkoa huo kuwa
wanapaswa kuendelea zaidi kuwa wabunifu katika shughuli mbalimbali ili Simiyu
iendelee kukua zaidi katika uwekezaji na maendeleo.
Kwa upande wake Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya uchapishaji
wa Magazeti ya serikali (TSN) Tanzania Standard Newspaper inayochapisha magazeti
ya Habari Leo, Daily News na Sport Leo Dkt Jim Yonazi amesema kuwa kampuni hiyo
ya TSN imeamua kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu ili kuufanya
mkoa huo kuungana na Dunia katika kuakisi uwekezaji hususani katika sekta ya
Viwanda.
Dkt Yonazi amesema kuwa kampuni ya TSN ina amini kuwa
maendeleo ni habari hivyo kupitia Jukwaa hilo la Biashara katika Mkoa wa Simiyu
watanzania na Dunia kwa ujumla itafahamu vyema juu ya umuhimu wa uwekezaji
hivyo kupitia umoja na mshikamano kwa wafanyabiashara na wawekezaji katika Mkoa
huo utakuwa chachu ya mafanikio ya Tanzania nzima.
Hata hivyo amesema kuwa Mkutano huo umefanikiwa kwa kiasi
kikubwa kwa sababu ya nguvu ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
ambapo hata hivyo amewasihi wawekezaji na wadau wa Maendeleo kutumia nguvu hiyo
kwa ajili ya biashara zao.
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa mlipa kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw Richard Kayombo ameelezea sababu za wawekezaji na wananchi kulipa kodi ambapo amesema kuwa njia pekee ya ambayo serikali inaweza kujipatia kipato chake kwa ajili ya kuwajengea wananchi Miundombinu bora, Kudumisha sekta ya Afya, Elimu na sekta zingine nyingi ni kukusanya kodi pekee.
Hata hivyo alisema kuwa zipo sekta ambazo kisheria zinapewa msamaha wa kutokulipa kodi ambapo ni pamoja na sekta ya Kilimo sambamba na sekta ya elimu na afya.
Naye Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Masoko kutoka TIB Corporate Bank Ltd Bi Theresia Soka amesema kuwa Bank hiyo ni maalumu kwa ajili ya shughuli za maendeleo na Biashara hivyo wajibu wake ni kufanya kazi ili kuhakikisha maendeleo yanawafikia wananchi hususani katika msaada wa kifedha.
Wadau wengine walioshiriki katika Jukwaa hilo la Biashara ni pamoja na TIB Development Bank, National Microfinance Bank (NMB), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na TIB Development Bank Ltd.
0 comments:
Post a Comment