Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (kulia) akitambulisha msafara wake kwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bw. Godfrey Zambi (hayupo pichani) wakati walipomtembelea ofisini kwake mjini Lindi. Kushoto ni Meneja Mikopo, Bw. Samuel Mshote na Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa TADB, Bw. Augustino Matutu Chacha (katikati).
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bw. Godfrey Zambi (hayupo pichani) wakati walipomtembelea ofisini kwake mjini Lindi.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bw. Godfrey Zambi akizungumza na ugeni kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania wakati walipomtembelea ofisini kwake mjini Lindi.
Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa TADB, Bw. Augustino Matutu Chacha (aliyesimama) akiwasilisha mada juu ya fursa za mikopo zinazotolewa na Benki ya Kilimo kwa Wadau wa Korosho na Ufuta Mkoa wa Lindi uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi.
Wadau wa Korosho na Ufuta Mkoa wa Lindi uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi.
Wadau wa Korosho na Ufuta Mkoa wa Lindi uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi.
Wadau wa Korosho na Ufuta Mkoa wa Lindi uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi.
Na
Mwandishi wetu, Lindi
Mkuu
wa Mkoa wa Lindi, Bw. Godfrey Zambi ameiomba Benki ya Maendeleo ya Kilimo
Tanzania (TADB) kukopesha wakulima wa mazao ya ufuta na mihogo ili waweze
kulima kilimo cha kisasa na cha kibiashara hasa kwa wakulima wadogo wadogo wa
mkoani humo.
Bw.
Zambi alitoa wito huo wakati wa mkutano wa Wadau wa Korosho na Ufuta Mkoa wa
Lindi uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi.
Bw.
Zambi alisema kuwa mkoa wa Lindi ni mkoa uliojaaliwa katika kuzalisha mazao ya
ufuta na mihogo lakini changamoto kubwa ni mtaji wa kulima kibiashara ili
kukidhi mahitaji ya soko la ndani na nje ya nchi.
“Wakulima
wa mkoa wa Lindi wapo tayari kushiriki katika kuleta mapinduzi ya Kilimo kutoka
kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara lakini kwa sasa suala la mtaji wa
kilimo cha kibiashara ni changamoto kubwa,” alisema Bw. Zambi.
Kwa
upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga alisema kuwa
Benki ya kilimo ipo tayari kutoa mikopo kwa wakulima wadogo wadogo waliokuwa
kwenye vikundi ili waweze kukopeshwa.
Bw.
Assenga aliongeza kuwa Benki ya Kilimo pia ipo tayari kuwekeza kwenye miradi ya
maendeleo ya Kilimo kwa kuipatia mikopo yenye riba nafuu zilizo chini ya
viwango vya kibiashara kwenye soko.
“Kwa
kutambua umuhimu wa wakulima wadogo wadogo nchini TADB imedhamiria na
kujizatiti kuhakikisha inachangia kwa kiasi kikubwa katika kuleta
Mapinduzi yenye tija katika Sekta ya Kilimo nchini kwa kusaidia upatikanaji na
utoaji wa fedha ikiwa ni pamoja sera nzuri zitakazosaidia maendeleo ya kilimo
nchini,” alisema.
Naye,
Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa TADB, Bw. Augustino Chacha alisema kuwa
TADB inalenga kuongeza upatikanaji wa huduma zisizo za kifedha kwa wakulima
kama vile kujengewa uwezo juu ya uandaaji wa andiko la miradi ya Kilimo, pamoja
na upatikanaji wa taarifa za masoko, usimamizi wa biashara, mafunzo juu ya
miradi ya Kilimo na mbinu za majadiliano ya mikataba.
“Tupo
tayari kutoa mikopo kwa ajili ya kuwanyanyua wakulima kama ilivyolengwa na
Serikali kupitia mikopo ya pembejeo kuongeza tija kwenye uzalishaji, miundo
mbinu ya umwagiliaji na ununuzi wa zana za kilimo,” alisema.
Bw.
Chacha aliongeza kuwa kwa upande wa mikoa ya kusini Benki ya Kilimo imejipanga
kueendeleza miundombinu ya umwagiliaji na maghala pamoja na uzalishaji wa mbegu
bora za mazao ya korosho na mihogo na kuimarisha viwanda vya kubangua mazao ya
korosho, na kusindika ufuta, mihogo.
Bw.
Chacha aliongeza kuwa Benki imejipanga kuwezesha uanzishaji wa mashamba mapya
na ya kisasa ya mihogo, korosho na ufuta mkoani Lindi.
0 comments:
Post a Comment