METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, April 25, 2017

VITUO 48 VYA AFYA KATIKA MANISPAA YA UBUNGO KUTOA HUDUMA YA MAMA NA MTOTOTAREHE 24-30/2017

 Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mh. Kisare Matiku Makori
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mh. Kisare Matiku Makori akitoa tone la chanjo kuashiria uzinduzi wa wiki ya Chanjo

Na Bornwell Kapinga, Dar es salaam

Hayo yamebanishwa leo katika maadhimisho ya uzinduzi wa wiki ya chanjo katika Mkoa wa Dar es Salaam, Maadhimisho yenye kauli mbiu " Jamii iliyochanjwa ni Jamii yenye Afya " uzinduzi ambao umefanyika katika kituo cha afya Kimara Halmashauri ya Ubungo. Maadhimisho ya uzinduzi huo yamehudhuriwa na wataalamu mbalimbali wa afya katoka katika Manispaa tano za jiji la Dar es Salaam ambazo ni Kinondoni, Ilala,

Temeke, Kigamboni na Ubungo ambayo ilikuwa mwenyeji wa maadhimisho ya uzinduzi huo. Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mh. Kisare Matiku Makori ndiye alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya uzinduzi, ambapo wakati wa uzinduzi huo alipongeza maadhimisho hayo kufanyika katika Manispaa ya Ubungo licha ya kuwa ni Manispaa mpya " mmetuamini kwamba tunaweza kufanikisha zoezi hili muhimu ambalo limefana sana" alisema Kisare Makori. 

Mkuu wa Wilaya Mh. Kisare Makori ameishukuru Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya afya Maendeleo ya jamii Jinsia Wazee na Watoto ambayo ndiyo imebeba dhamana kubwa ya kuhakikisha afya za wananchi zinaboreshwa kwa kupata kinga dhidi ya magonjwa yanayosumbua Taifa na Dunia kwa ujumla. 

Pia amebainisha uzinduzi wa wiki ya chanjo ngazi ya Mkoa ambo umefanyika leo ni sehemu ya jitihada za hatua mahususi zinazochukuliwa na Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais wetu Dr. John Pombe Magufuli kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha watoto wa kitanzania wanakuwa na afya bora. 

Katika kuhakikisha kila mwaka mwezi April kunakuwa na wiki ya chanjo Mkuu wa Wilaya amewashukuru wadau muhimu ambao ni Shirika la Afya Duniani na wadau wengine kwa kuwa na mchango chanya ambao watoto wote wanapata fursa ya kupatiwa chanjo pamoja na wale ambao hawakukamilisha mzunguko wa awali. Mkoa wa Dar es Salaam unajumla ya vituo tiba 270 vya Umma na binafsi vitakavyotoa huduma ya Mama na Mtoto katika zoezi hili la kuwapatia watoto wetu chanjo, Mchanganuo wa vituo hivyo ni kama Kinondoni vituo 67 , Ilala vituo 71 , Ubungo 48 Temeke 65 na Kigamboni vituo 19. 

Vituo vyote vitakuwa wazi kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa kumi na moja jioni kwa wiki nzima ya maadhimisho wahudumu wetu watatoa huduma ya chanjo kwa siku zote wazazi / walezi wenye watoto chini ya miaka mitano ambao hawajapata chanjo au wale ambao hawajakamilisha chanjo waje wapatiwe chanjo katika vituo vyetu. Kaimu Mkurugenzi ambaye pia ni Afisa Utumishi Mkuu wa Manispaa ya Ubungo Ndg Juma Ally alipopewa nafasi ya kuzungumza alisema kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo anawaomba watumishi hususani Wauguzi kutoa huduma kwa weledi na aliwahakikishia wafanyakazi wa kituo cha Afya Kimara kuwa changamoto zao za uhaba wa majengo zitatatuliwa kwa kuwa kwa mwaka wa fedha 2017/2018 tayari kuna bajeti ya ujenzi wa Gorofa katika kituo hicho. 

Pia suala la watumishi anazungumza na Mganga mkuu wa Manispaa kuona namna ya kurekebisha ikama ili kuweza kuongeza Watumishi katika kituo cha Kimara. Alisema Juma Ally.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com