Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya fedha na Uongozi Manispaa ya Ubungo wakiangalia eneo la ujenzi wa shule ya Sekondari Mavurunda Kata ya Kimara
Mwenyekiti wa kamati ya fedha na uongozi Manispaa ya Ubungo ambaye ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe Boniface Jacob akiwafundisha wanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari Mburahati ili kupima ufahamu wao wakati wa ziara ya kikazi katika shule hiyo
Naibu Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe Ramadhani Kwangaya akisaini kitabu cha wageni wakati wa ziara ya kikazi ya kutembelea miradi ya maendeleo
Kamati ya Fedha na Uongozi ya Manispaa ya Ubungo Leo April 25, 2017 imefanya ziara ya kikazi kwa kutembelea Miradi ya Maendeleo katika Manispaa ya Ubungo.
Ziara hiyo iliyoongozwa na Mwenyekiti wa kamati ambaye ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe Boniface Jacob imezuru katika miradi hiyo kwa lengo la kujionea hali halisi ya shughuli mbalimbali zinazoendelea ikiwemo ujenzi.
Miongoni mwa miradi iliyotembelewa na Kamati ya Fedha na
Uongozi ya Manispaa ya Ubungo ni pamoja na kuona hali halisi ya ujenzi wa
Zahanati ya Kata ya Mburahati sambamba na ujenzi wa choo katika shule ya
Sekondari Mburahati.
Miradi mingine ni kuona hali halisi ya ujenzi wa matundu 12
ya choo cha shule ya Msingi Mabibo Jeshini, sawia na Ujenzi wa madarasa manne
katika shule ya Sekondari Saranga.
Mwenyekiti wa kamati hiyo ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya
Ubungo Mhe Boniface Jacob na Katibu wake ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo
Ndg John Lipesi Kayombo
Imetolewa na;
Kitengo cha Uhusiano
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo
0 comments:
Post a Comment