METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, May 31, 2017

KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU KITAIFA AZINDUA KITUO CHA MABASI SIMU 2000 (SINZA)

Kiongozi wa Mbio za Mwemge Kitaifa Mwaka 2017 Ndg Amour Hamad Amour amezindua Mradi wa Mabasi SIMU 2000 Uliopo katika Kata ya Sinza, Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es salaam.

Amewasihi madereva wa daladala Kulipa Kodi ili kukifanya kituo hicho kiweze kujisimamia vyema sambamba na kuagiza kituo Cha Polisi kilichopo katika eneo hilo kufanya upekuzi wa Kila namna kwa abiria Ili kuepuka Dawa za kulevya.

Amour alisema kuwa Wananchi wanapaswa kuendeleza Mapambano dhidi ya Ukimwi, Malaria na vifo vitokanavyo na Ukimwi ili kunusuru watanzania wanaofariki kutokana na kadhia hiyo.

Ujenzi wa mradi huo umejumuisha ujenzi wa kituo cha kuegesha magari (kituo cha daladala), ujenzi wa kituo cha polisi na ujenzi wa choo.

Lengo kuu la kuanziasha mradi huo ni  kurahisisha upatikanaji wa usafiri kwa wananchi kuelekea sehemu mbalimbali za jiji la Dar es salaam na nje ya mkoa.

Ujenzi huo wa mradi wa  simu 2000 ulianza kufanya kazi  tarehe 23 /10/2014 kikiwa na mabasi (daladala) zipatazo 500 na  mabasi yaliyokuwa yanatoa huduma kwenda Mikoa jirani kama vile Pwani, Morogoro na Tanga yalikuwa mabasi 350.

Kwa sasa kituo hicho kinahudumia mabasi (daladala) 560 na  bajaji 25 na  magari yaliyokuwa yanaenda nje ya mkoa yalihamishwa kwenda kituo cha Mbezi Luis.

Kituo hicho kimejengwa kwa kutumia fedha zilizotokana na Mapato ya Ndani (Own Source)  Gharama yake ni Shilingi 2,376,647,991.89 chini ya Mkandarasi M/S DEL MONTE (T) LTD.

Imetolewa Na;
Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com