METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, November 18, 2019

TAALUMA YA MAENDELEO NA USTAWI WA JAMII IWE CHACHU YA MABADILIKO KATIKA JAMII: DKT. JINGU


Katibu Mkuu maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. John Jingu akisalimiana na Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Uyole Bw. Rajab Kaleranda wakati alipowasili mkoani Morogoro kufungua mkutano uliowakutanisha Wakuu wa vyuo na Taasisi za Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii nchini.
Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. John Jingu akizungumza na Wakuu wa Vyuo na Taasisi za Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii nchini wakati wa kikao kilichowakutanisha wakuu hao katika kupanga Mikakati ya kuboresha Kada za Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii.
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Patrick Golwike akielezea jinsi Kada ya Maendeleo ya  Jamii inavyosaidia katika kueta mabadiliko na kusaidia jamii wakati kikao kilichowakutanisha Wakuu wa Vyuo na Taasisi za Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii nchini kupanga Mikakati ya kuboresha Kada za Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii.
Kamishna wa Ustawi wa Jamii Dkt. Naftali Ng’ondi akielezea jinis a Kada ya Ustawi wa Jamii inavyosaidia katika kueta mabadiliko na kusaidia jamii wakati kikao kilichowakutanisha Wakuu wa Vyuo na Taasisi za Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii nchini kupanga Mikakati ya kuboresha Kada za Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii.
Wakuu wa Vyuo na Taasisi za Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii nchini wakisikiliza mada mbalimbali katika kikao kilichowakutanisha kupanga Mikakati ya kuboresha Kada za Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii.

Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW

……………………
Na Mwandishi Wetu Morogoro

Katibu Mkuu Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu amevitaka Vyuo na Taasisi za Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii nchini kutoa elimu itakayowasaidia wahitimu kuleta mabadiliko katika jamii zao na kuweza kujiajiri na kuajiri watu wengine kuliko kutegemea kuajiriwa.


Dkt.John Jingu ameyasema haya leo mkoani Morogoro wakati akifungua kikao kazi cha wakuu wa Vyuo na Taasisi za Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii nchini kilicholenga kubadilishana uzoefu kwa wakuu hao wa vyuo katika utendaji kazi na kujengeana uwezo ili Taasisi na Vyuo viweze kufanikisha malengo ya Taifa.


Dkt. Jingu amesema kuwa taaluma ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii  lazima iwe nyenzo ya kutatua changamoto zilizopo katika jamii ikiwemo tatizo la ajira kwa vijana kwa kutoa taaluma itakayowapa fursa wahitimu kujiajiri kutokana na taaluma waliyopata.


“Umefika wakati sasa Taasisi na Vyuo kuja na Mpango Mkakati wa namna ya kutekeleza dhana ya kujiajiri  kwa lengo la kuzalisha wahitimu mahiri ” alisema Dkt. Jingu.

Ameongeza kuwa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii vimetoa mchango mkubwa sana katika kutatua changamoto za jamii na hivyo jamii kuthamini uwepo wa vyuo katika jamii na mafanikio yaliyoonekana  kwa vyuo hivyo yaonekane kwa kila chuo.

Aidha Dkt. Jingu amevitaka Vyuo hivyo kuanzisha Vituo vya kielektroniki vya ubunifu na maarifa (Digital Innovation Centre) ambao utarahisisha upatikanaji wa maarifa na ujuzi kwa haraka zaidi kuliko kusoma vitabu na itatoa fursa ya kupata maarifa katika muda mfupi. 

“Natumaini ushiriki wetu katika kikao kazi hiki utatuongezea ari na ubunifu wa kazi katika maeneo yetu na mtazingatia mafunzo na maelekezo yatakayotolewa katika kuhakikisha vyuo vinatoa matokeo chanya kwa kuzalisha wataalam wenye ujuzi na maarifa ya kazi.  
  
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii nchini Patrick Golwike amesema kuwa ili kujipambanua katika jamii umuhimu wa Kada ya Maendeleo ya Jamii inatakiwa kuwa na mbinu ya namna ambayo Vyuo vya Maendeleo ya Jamii itatoa wataalam wakaosaidia kuleta mabadiliko kwa jamii.

Naye Kamishna wa Ustawi wa Jamii nchini Dkt. Naftali Ng’ondi amesema kuwa Kada ya Ustawi wa Jamii ni moja kati ya Kada ambazo zina uwanda mpana wa kujiajiri na kuajiriwa hivyo Vyuo na Taasisi ya Ustawi wa Jamii zijikite katika kutoa elimu itakayowasaidia wahitimu hasa kujiajiri.

Wakuu wa Vyuo na Taasisi za Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii wamekutana mkoani Morogoro katika kikao kazi kilicholenga kutafuta namna bora ya taaluma ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii katika kuleta mabadiliko katika jamii.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com