**************************************
Waziri Mkuu
Kassim Majaliwa amemuagiza Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Bw. Julius
Mtatiro ahakikishe anaondoka na Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho hadi
Tunduru ili wakahakiki ni kwa nini wakulima hawajalipwa.
“Nimefurahi
kusikia minada ya korosho inakwenda vizuri. Lakini sijafurahia habari ya
Tunduru. Mheshimiwa Rais aligiza sh. milioni 40 zipelekwe kwa wakulima.
Na ninajua kwamba zimeshalipwa. Sasa ni kwa nini wakulima bado
wanadai?, alihoji.
“Ukitoka hapa
kwenye mkutano nenda pale jengo la Bodi ya Korosho. Ondoka na Mtendaji
Mkuu wake, mwende Tunduru akafuatilie ni kwa nini malipo ya mwaka jana
hayajalipwa hadi sasa.” Bw. Mtatiro ni Mkuu wa Wilaya ya Tunduru.
“Nataka
afuatilie fedha zimekwama kwa nani. Kaimu Mkuu wa Mkoa ukigundua
wanaokwamisha ni viongozi wa ushirika, shughulika nao hukohuko kama
ambavyo umekuwa ukifanya,” amesisitiza.
Ametoa agizo
hilo leo mchana wakati akifungua kongamano la siku moja la Wakandarasi
na Wazabuni wa mikoa ya Kusini lilioandaliwa na benki ya CRBD kwenye
ukumbi wa Benki Kuu (BoT) mjini Mtwara.
Akizungumzia
kuhusu kongamano hili ambalo kaulimbiu yake ni “Pamoja nawe kukuza
uchumi”, Waziri Mkuu amewataka wakandarasi hao baada ya kupata elimu
kidogo kuhusu shughuli za benki hiyo, anataraji kuwa wataenda kwenye
Halmashauri zao na kutafuta ……..
“Serikali
inajenga miradi mikubwa kama vile bwawa la kuzalisha umeme kwa nguvu ya
maji la Mwalimu Nyerere, bomba la mafuta la kutoka Hoima hadi Tanga na
miradi ya maendeleo kama ile ya barabara, reli, ujenzi wa hospitali,
madarasa na nyumba za walimu. Miradi yote hii inawatarajia ninyi
wakandarasi mkaijenge.”
Alisema
Serikali imeendelea kuimarisha na kusogeza karibu kwa wananchi huduma za
jamii ikiwemo ukarabati wa miundombinu ya kufundishia na kujifunzia
katika ngazi zote za elimu.
“Katika kipindi cha Januari hadi Juni 2019,
kwa shule za msingi, Serikali imejenga madarasa 473, matundu ya vyoo
1,405, nyumba za walimu 24 na kukamilisha maboma ya madarasa 2,760. Kwa
shule za sekondari, Serikali ilijenga madarasa 465, matundu ya vyoo 736,
nyumba za walimu 23 na kukamilisha maboma ya madarasa 2,392,” alisema.
Waziri Mkuu
alitumia fursa hii kutoa wito kwa viongozi na watendaji wazingatie
utekelezaji wa Sheria ya Ununuzi wa Umma kwa kutenga zabuni zenye
thamani ya chini ya shilingi bilioni 10 kwa ajili ya wazabuni Watanzania
ili kuwajengea uwezo na kushiriki katika zabuni. Alisema Serikali kwa
upande wake itaendelea kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Ununuzi ili
kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Alimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa CRDB kwa kubuni programu hiyo ya tofauto ambayo imelenga kuwainua wakandarasi wadogo na wa kati.
Mapema,
akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na washiriki qa kongamano hilo,
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Bw. Gelasius Byakanwa alisema hadi sasa jumla
ya tani 67,000 za korosho zimeuzwa mkoani humo kupitia minada mitatu.
Oktoba 30,
mnada wa kwanza ulipofanyika bei ilikuwa sh. 2,468/- kwa kilo na mnada
wa tarehe 15 Novemba, ulishihudia bei ikipanda na kufikia sh. 2,890/-
kwa kilo, alisema.
Alisema
katika msimu huu, korosho zimeingiza sh. Bilioni 1.75 ambapo kati ya
hizo, sh. Bilioni 1.20 zimeshaingizwa kwenye akaunti na kupelekwa kwa
wakulima.
Naye Mkurugenzi
Mkuu wa benki ya CRDB, Bw. Abdulmajjid Nsekela alisema bei hiyo
inamsaidia mteja kwa kutoa ushauri, kumwezesha na kushirikiana naye
kuijenga nchi.
“Leo tuko
Mtwara, lakini tumeshaendesha makongamano kama haya katika mikoa ya Dar
es Salaam, Arusha, Mbeya, Mwanza. Na hapa Mtwara tumejumuisha pia mikoa
ya Lindi na Ruvuma,” alisema.
Alisema benki
hiyo ina hisa trilioni 6.3 ambazo ni sawa na asilimia 20 ya hisa za
mabenki yote na kwa upande wa amana, Mkurugenzi Mkuu huyo alisema amana
za benki hiyo zinafikia trilioni 4.9 ambazo ni sawa na asilimia 23 ya
amana za benki zote nchini.
0 comments:
Post a Comment