METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, May 31, 2017

KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE AZINDUA MRADI WA UJENZI WA JENGO LA ZAHANATI YA MBURAHATI KATIKA ENEO LA MTAA WA NHC KATA YA MBURAHATI

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Ndg Amour Hamad Amour amezindua Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Zahanati ya Mburahati katika eneo la Mtaa wa NHC Kata ya Mburahati, Wilaya ya Ubungo, Jijini Dar es salaam.

Zahanati hiyo ikikamilika inataraji kusogeza huduma zaidi karibu na wananchi kwa kujenga zahanati katika Eneo hilo ili wananchi wahudumiwe vyema waliopo karibu na kituo hicho ili kuondoa msongamano katika Kituo cha Afya cha Makurumla.

Mradi huu utahudumia zaidi ya wananchi elfu 30,000 walioko katika Kata ya Mburahati na mitaa yake ya Barafu, Kisiwani na NHC lakini pia itahudumia kata zingine zinazozunguka eneo hilo kama Kata za Mabibo, Makurumla na Kigogo.

Mradi huu wa ujenzi wa zahanati  ulianza kutekelezwa tangu Juni 2014 na kukamilika mnamo Oktoba 2016 chini ya Manispaa ya Ubungo, kwa gharama ya kiasi cha Tshs 84,000,000.00.

Mradi huo ni moja kati ya miradi ambayo Halmashauri imekusudia kufanya kwa jamii.

Mradi huo utaboresha huduma za afya na kupunguza msongamano katika zahanati zilizo jirani.

Imetolewa Na;
Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com