METDO Tanzania

METDO Tanzania

Sunday, April 16, 2017

DC JUMA HOMERA AZINDUA MKOA MPYA WA UKWATA UITWAO SELOUS

Mkuu wa wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Mhe. Juma Zuberi Homera, jana alihudhuria misa ya Ijumaa Kuu katika  ukumbi wa Aula uliyopo ndani ya Taasisi ya Kiuma katika kijiji cha Mironde kata ya Matemanga.

Misa hio maalum iliandaliwa na Umoja wa Kikristu wa Wanafunzi Tanzania-UKWATA kwa lengo la kuzindua mkoa mpya wa Ukwata uitwayo Selous.

Dc Homera alikuwa mgeni mwalikwa katika misa hio maalum ya kuzindua mkoa mpya na kufungua semina ya siku nne iliyoanza jana Ijumaa na inatarajiwa kuisha Jumatatu tarehe 17, semina hio inashirikisha wana Ukwata toka Mkoa wa Ruvuma, Lindi pamoja na Mtwara.

Mkoa mpya  wa Ukwata wa Selous utaunganisha wilaya tatu za Tunduru, Namtumbo na Nanyumbu. Wilaya ya Tunduru na Namtumbo zipo mkoa wa Ruvuma na wilaya ya Nanyumbu ipo mkoa wa Mtwara.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkuu wa wilaya ya Tunduru alisema tukio hilo ni la kihistoria na hatua ya kuzindua mkoa maalum wa ukwata, ipo siku serikali inaweza ona tija ya kuwa na mkoa rasmi wa Selous. aliwasisitiza zaidi vijana toka mikoa ya Kusini hususani Tunduru wanapaswa kusoma kwa bidii ili tuwe na jamii yenye Elimu.

"Tukio la leo ni la kihistoria, hatua iliyofikiwa na viongozi wa Ukwata ni ya kupongezwa na naamini ipo siku serikali itaona tija ya kuwa na Mkoa rasmi wa Selous, sasa vijana wa mikoa ya Kusini hususani Tunduru mnapaswa kusoma kwa bidii ili tuwe na jamii yenye Elimu ambao ni chachu ya Maendeleo".

Alimalizia kwa kuwa omba wananchi wote waendelee kumwombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Joseph Magufuli aendele kuwatumikia vyema wananchi na alimshukuru Dr. Matomola Matomola Mkurugenzi wa Taasisi ya Kiuma kwa huduma bora anayo toa kwa wananchi kama Malezi ya Imani, Hospitali kubwa inayotoa Matibabu na Upasuaji Mkubwa kwa garama nafuu, Shule ya Sekondari, Kituo cha Kilimo, Chuo cha Uuguzi na Ualimu n.k.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com