METDO Tanzania

METDO Tanzania

Sunday, April 16, 2017

TAARIFA YA KUKAMILIKA KWA CHOO KIMOJA CHA MZUNGUKO CCM KIRUMBA

Uongozi wa uwanja wa CCM Kirumba kupitia Meneja wa Uwanja Ndg *Steven E. Shija* unapenda kuwajulisha kuwa ukarabati wa Choo kimoja chenye Matundu 3 na eneo la Kukojolea kimekamilika kwa kiwango cha Kimataifa

Hivyo Uongozi wa Uwanja unapenda kuwataarifu watumiaji, punde tutakapo kamilisha vingine lazima tuwe wastaarabu katika matumizi, maana tumedhamilia kuweka ulinzi kila Choo ili kuepusha uhalibifu wa Makusudi unaoweza kufanywa na watumiaji wasiokuwa wastaarabu, tukumbuke tumetumia gharama kubwa sana kuvikarabati kwenye viwango bora kabisa

Pia tunaendelea na awamu nyingine ya Ukarabati wa Chumba maalumu cha huduma ya Kwanza kwa Wachezaji (Dooping Room) na Choo kimoja, tunaamini kabla ya Mwezi Mei tutakuwa tumekamilisha na kuendelea hatua nyingine ili kuuboresha zaidi uwanja wetu katika kiwango cha Kimataifa.

Mwisho tunaushukuru Uongozi wa CCM Mkoa wa Mwanza kwa kuhakikisha wanatimiza kila tulichoomba ili kufanikisha awamu hii ya Ukarabati wa Vyoo na Kurekebisha Uwanja wetu (Pitch), pia tunawashukuru Wadau wote wa Michezo hususani *Mwanza Veterans*, Ndg *Jamal Babu* (MNEC - Nyamagana), *Mkurugenzi Nyanza Roads*, Ndg *Patrick Kambarage* , Waandishi wa Habari na Wajasiliamali wanaozunguka Eneo lote la Uwanja ( Mafundi na Mama Lishe) kwa namna wanavyotupa ushirikiano Mkubwa kwenye kutimiza wajibu wetu, zaidi tunawashukuru Watumishi wote wa Uwanja kwa namna wanavyojituma na kujitoa kwa hali na mali katika kutimiza wajibu wao wakati wote

*We Walk the talk*

*Imetolewa na:-*
*Uongozi wa Uwanja*
*CCM Kirumba - Mwanza*
*16.04.2017*

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com