Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori (Kulia), Diwani wa Kata ya Kimara Mhe Manota wakikagua eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa shule ya Sekondari ya Kata ya Kimara Jijini Dar es salaam. Leo Mei 26, 2017
Baadhi ya Wakazi wa Kata ya Kimara wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori wakati akizungumza nao mara baada ya kuzuru kukagua eneo litakalojengwa Shule ya Sekondari ya Kata ya Kimara Jijini Dar es salaam. Leo Mei 26, 2017
Diwani wa Kata ya Kimara Mhe Manota akizungumza na wananchi wa Kata hiyo kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori kuzungumza na wananchi mara baada ya kuzuru kukagua eneo litakalojengwa Shule ya Sekondari ya Kata ya Kimara Jijini Dar es salaam. Leo Mei 26, 2017
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori akiwaongoza wananchi kukagua eneo litakalojengwa Shule ya Sekondari ya Kata ya Kimara Jijini Dar es salaam. Leo Mei 26, 2017
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori akikagua ukarabati wa Zahanati ya Mavurunza mara baada ya kuzuru kukagua eneo litakalojengwa Shule ya Sekondari ya Kata ya Kimara Jijini Dar es salaam. Leo Mei 26, 2017 ambapo ameahidi kusaidia kukamilika haraka kwa ujenzi huo.
Hali ya ukarabati wa Zahanati ya Mavurunza iliyopo katika Mtaa wa Mavurunza Kata ya KImara
Diwani wa Kata ya Kimara Mhe Manota akimuongoza Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori kukagua ukarabati wa Zahanati ya Mavurunza mara baada ya kuzuru kukagua eneo hilo. Leo Mei 26, 2017 ambapo ameahidi kusaidia kukamilika haraka kwa ujenzi huo.
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori akizungumza na wananchi mara baada ya kuzuru kukagua eneo litakalojengwa Shule ya Sekondari ya Kata ya Kimara Jijini Dar es salaam. Leo Mei 26, 2017
Katibu Tawala wa Wilaya ya Ubungo Ndg James Mkumbo akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Mavurunza Kata ya Kimara Jijini Dar es salaam muda mchache kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Ubungo kuzungumza na wananchi wa Kata hiyo. Leo Mei 26, 2017
Wananchi wa Kata ya Kimara wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori mara baada ya kuzuru kujionea eneo litakalojengwa Shule ya Sekondari ya Kata hiyo Jijini Dar es salaam. Leo Mei 26, 2017
Baadhi ya Wakazi wa Kata ya Kimara wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori wakati akizungumza nao mara baada ya kuzuru kukagua eneo litakalojengwa Shule ya Sekondari ya Kata ya Kimara Jijini Dar es salaam. Leo Mei 26, 2017
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori akizungumza na wananchi mara baada ya kuzuru kukagua eneo litakalojengwa Shule ya Sekondari ya Kata ya Kimara Jijini Dar es salaam. Leo Mei 26, 2017
Na Mathias Canal, Dar es salaam
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare
Matiku Makori Leo Mei 26, 2017 ameiagiza Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya
Ubungo inayoongozwa na Ndg John Lipesi Kayombo kuanza haraka ujenzi wa Shule ya
Sekondari kwa ajili ya Kata ya Kimara Jijini Dar es salaam.
Agizo hilo amelitoa wakati akizungumza
na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja
vya shule ya Msingi Mvurunza mara baada ya kufanya ziara ya kikazi katika Kata
hiyo ili kujionea hali ya maendeleo ya elimu sambamba na kubaini changamoto
zinazowakabili wananchi katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Ubungo na
hatimaye kuzitatua.
Katika ziara hiyo ya Mkuu wa Wilaya ya
Ubungo imehudhuriwa pia na Katibu Tawala wa Wilaya ya Ubungo, Afisa Tarafa ya
Kibamba, Afisa Elimu Sekondari Manispaa ya Ubungo, Diwani wa Kata ya Kimara,
Mtendaji Kata ya Kimara, Wenyeviti na Watendaji wa Mitaa sambamba na Baadhi ya
Wananchi wa eneo hilo.
Agizo la Mkuu wa Wilaya ya Ubungo
linakuja zikiwa ni siku chache zimepita tangu kutoa maagizo kama hayo katika
Shule ya Msingi Ubungo Plaza, Shule ya Msingi Kawawa na Shule ya Sekondari
Mburahati ambapo kote huko ameelekeza kuanza haraka ujenzi wa Madarasa sambamba
na Vyoo kwa ajili ya wanafunzi na walimu.
Mhe Makori alisema kuwa madarasa
anayoagiza yaanze kujengwa yatapunguza kadhia ya mbanano wa wanafunzi darasani
ambapo pia amewaahidi wananchi hao kujengwa madarasa kwa viwango vya kisasa.
Naye Moses Mzakwe na Deogratius Stephano
ambao ni wakazi wa Mtaa wa Mavurunza wameomuomba Mkuu wa Wilaya kutilia mkazo
swala la upimaji wa viwanja ili wananchi waweze kumiliki ardhi huku
wakimpongeza kwa kuzuru katika eneo hilo kwani ameonyesha uwezo wa kujali
wananchi anaowaongoza.
Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha
Mkuu wa Wilaya kuzungumza na wananchi hao Diwani wa Kata ya Kimara Mhe Manota
alimpongeza Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kwa kutekeleza sera na
kuisimamia ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015/2020 na kuwaomba watanzania wote kwa
kauli moja pasina itikadi za vyama kumuunga mkono kwani atakuwa imara na
madhubuti zaidi katika utendaji wake iwapo ataungwa mkono na watanzania wote.
Alisema kuwa Rais Magufuli anapaswa
kutilia mkazo zaidi kwa kuwawekea kufuli watu waliokuwa wanalihujumu Taifa kwa
wizi na ufisadi katika sekta mbalimbali nchini.
Mhe Manota alisema kuwa tayari
zimetolewa jumla ya shilingi milioni mia moja kwa ajili ya kuanza ujenzi wa
Shule hiyo ambapo mara baada ya kukamilika itawarahisishia wanafunzi kupata
elimu bora pasina mateso wanayoyapata sasa kutokana na ukosefu wa shule ya
serikali ya Sekondari katika Kata nzima ya Kimara.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment