Na Mwandishi wetu Zanzibar
Kalenda ya uchaguzi ngazi ya matawi ya CCM ni 27-30/05/2017 ratiba ambayo imepitishwa na mkutano mkuu wa CCM taifa.
Kwa ratiba hiyo leo 27/05/2017 Mh mbunge wa Jimbo LA Chumbuni ametimiza haki yake ya Msingi ya kikatiba kwa kupiga kura yake katika tawi la Mwembe Makumbi jimbo la Chumbuni.
Mh Amjadi mara baada ya kupiga kura na kuchagua viongozi wapya wa Chama ambao watakuwa madarakani kwa miaka mitano alipata fursa ya kusema maneno machache.
"Jana nilikuwa Dodoma bungeni kwenye kikao cha bajeti ila akili yangu yote ilikuwa Zanzibar nilikuwa nikiwaza ni kwa jinsi gani ningeweza kukamilisha zoezi la kuchagua viongozi wangu wa tawi ambalo Mimi ni mwanachama".
Aidha MH Amjadi aliongeza kuwa
"Siku zote sisi viongozi wa juu tulikuwa tunawahamasisha wanachama wenzetu wajitokeze kujaza fomu za kugombea ili waweze kuchaguliwa na kuchagua sasa isingekuwa busara kwa sisi wahimizaji kukosa kupiga kura" alisema Pondeza
MH Pondeza aliwapongeza wanachama wote waliofika katika mkutano mkuu huo wa tawi la Mwembe Makumbi na kuwataka wachague viongozi bora na sio bora viongozi kwa maana hao ndio watakaotekeleza dhamira ya Chama kuendana na kasi ya mabadiliko ya kimfumo na dhamira ya Chama kupelekwa wa wanachama ili tuipate CCM mpya Tanzania mpya.
Aliwakumbusha viongozi watakao chaguliwa leo ndio watakaotegemewa kuhakikisha wanasimamia vyema CCM ishinde kwa kishindo uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 kwa hiyo wachaguliwe viongozi imara watakao kivusha Chama uchaguzi mkuu 2020.
Mwisho MH Pondeza aliwataka wale wote ambao kura hazitatosha kwa ngazi ya tawi watambue kuwa nafasi zipo nyingi katika ngazi za wadi, Jimbo, Wilaya, Mkoa na Taifa hivyo muda ukifika wajitokeze kwa wingi wajaze nafasi hizo MH Amjadi ameridhika na muitikio wa wanachama kujitokeza kwa wingi kujaza fomu za kugombea nafasi mbali mbali ngazi ya tawi kwa Chama na Jumuiya kwa ujumla.
0 comments:
Post a Comment