Meneja
Huduma kwa Wateja wa Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL), Aron Msonga
(kulia) akiwagawia line za TTCL zenye huduma za 4G LTE kwa baadhi ya
washiriki wa shindano la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016
walipotembelea Makao Makuu ya Ofisi za TTCL jijini Dar es Salaam leo.
TTCL ndiye mdhamini mkuu wa shindano la Miss Higher Learning
Institutions kwa mwaka 2016.
Washiriki wa shindano la TTCL Miss
Higher Learning Institutions 2016 wakiwa katika pozi walipotembelea
Makao Makuu ya Ofisi za TTCL jijini Dar es Salaam.
Meneja
Huduma kwa Wateja wa Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL), Aron Msonga
akizungumza na washiriki wa Shindano la TTCL Miss Higher Learning
Institutions 2016 pamoja na wageni wengine walipotembelea Makao Makuu ya
Ofisi za TTCL jijini Dar es Salaam. Nyuma yake ni washiriki wa shindano
la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016.
Meneja
Huduma kwa Wateja wa Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL), Aron Msonga
akizungumza na washiriki wa Shindano la TTCL Miss Higher Learning
Institutions 2016 pamoja na wageni wengine walipotembelea Makao Makuu ya
Ofisi za TTCL jijini Dar es Salaam. TTCL ndiye mdhamini mkuu wa
shindano la Miss Higher Learning Institutions kwa mwaka 2016.
Mkuu wa
Hitifaki Kamati ya Miss Tanzania 2016, Albert George Makoye (wa kwanza
kushoto) akizungumza kutoa shukrani kwa kampuni ya TTCL kwa kukubali
kuwa mdhamini mkuu wa Miss Higher Learning Institutions 2016. Wengine ni
viongozi na washiriki wa TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016.
TTCL ndiye mdhamini mkuu wa shindano la Miss Higher Learning
Institutions kwa mwaka 2016.
Mratibu
wa shindano la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016, Bi. Maya
Nkiru (kushoto) akizungumza kuishukulu kampuni ya TTCL kwa kukubali kuwa
mdhamini mkuu wa shindano hilo. Kulia ni Meneja Masoko wa TTCL, Beda
Kinunda akiwa katika hafla hiyo.
Mkuu wa
duka la huduma za TTCL Makao Makuu ya shirika hilo jijini Dar es Salaam,
Diana Obed (kulia) akitoa maelekezo kwa washiriki wa shindano la TTCL
Miss Higher Learning Institutions 2016 juu ya bidhaa na huduma
mbalimbali za TTCL zinazopatikana katika duka hilo.
Meneja
wa Biashara wa TTCL Mkoa wa Dar es Salaam, Augustino Mwakyembe (kushoto)
akitoa ufafanuzi kwa washiriki wa Shindano la TTCL Miss Higher Learning
Institutions 2016 walipotembelea Kituo cha Huduma kwa Wateja cha TTCL
Makao Makuu ya Ofisi za TTCL jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu.
KAMPUNI
ya Simu nchini Tanzania (TTCL) wameingia kama mdhamini mkuu wa
mashindano ya urembo kutafuta mrembo toka vyuo vikuu nchini 'TTCL Miss
Higher Learning Institutions 2016' atakaye shiriki katika fainali za
urembo kumpata mlibwende wa Tanzania 2016.
TTCL
wametangaza kuingia katika udhamini huo leo jijini Dar es Salaam ambapo
warembo wa shindano la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016
walipotembelea Makao Makuu ya TTCL kujifunza mambo mbalimbali
yanayofanywa na shirika hilo la umma nchini Tanzania.
Akizungumza
katika tukio hilo Meneja Huduma kwa Wateja wa TTCL, Aron Msonga amesema
shirika hilo limevutwa kusaidia mashindano hayo ili kuweza kuwapata
warembo wenye sifa stahiki watakao shinda katika kinyang'anyiro cha
'TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016' na baadaye kushiriki
shindano la Miss Tanzania 2016.
Amesema
TTCL kwa sasa inafanya mageuzi makubwa ya kibiashara na uendeshaji
ambayo yameboresha huduma za shirika hilo na bidhaa zake kwa ujumla
yanayoinufaisha jamii, hivyo haiwezi kujitenga na shughuli za kijamii
ikiwemo mashindano ya urembo.
Aidha
amewashauri waandaaji wa TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016
kufuata taratibu zote bila upendeleo ili kuweza kuwapata wawakilishi
wasomi na wenye sifa za ulimbwende ambao watashiriki vema katika kumpata
Miss Tanzania 2016.
Kwa
upande wake Mratibu wa shindano la TTCL Miss Higher Learning
Institutions 2016, Bi. Maya Nkiru ameishukuru kampuni ya TTCL kwa kuunga
mkono mashindano hayo na kuahidi kutoa ushirikiano wa hali ya juu ili
kuhakikisha yanafanyika kwa mafanikio makubwa na hatimaye kupatikana
warembo wenye vigezo na sifa kuwakilisha tawi hilo kwa ufasaha. Mratibu
huyo alisema shindano la kumpata mrembo atakayewakilisha 'TTCL Miss High
Learning 2016' kwa mwaka huu limeboreshwa na litakuwa na burudani za
kutosha na utofauti mkubwa hivyo kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi
siku hiyo ili kuweza kushuhudia shindano hilo. Aidha alitaja baadhi ya
wasanii watakaotumbuiza katika shindano hilo kuwa ni pamoja na msanii
Ney wa Mitego, MB Dog, Msaga Sumu na kundi la QS. TTCL Miss Higher
Learning Institutions 2016 itafanyika Septemba 17, 2016 katika Ukumbi wa
TTC Chang'ombe jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment