Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani leo tarehe 12 Novemba, 2018 amevunja rasmi Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) iliyokuwa ikiongozwa na Dkt. Gideona Kaunda.
Uamuzi huo ameutoa katika Mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika katika Ofisi za Wizara ya Nishati jijini Dodoma.
Alisema kuwa, Bodi hiyo iliundwa mwaka 2017, kwa mujibu wa Sheria ya Wakala Vijijini Na.8 ya Mwaka 2005 (The Rural Energy Act. No.8 of 2005).
“ Bodi hii imetekeleza majukumu yake kwa takriban mwaka mmoja (1) sasa na katika kipindi hicho ambapo Bodi hii imekuwepo, ninapenda kuwajulisha kwamba kwa ujumla sijaridhishwa na utendaji wake,” alisema Dkt Kalemani.
Hivyo alieleza kuwa, kwa mujibu wa mamlaka aliyopewa chini ya kifungu 9(3)(b) cha Sheria Na. 8 ya Nishati Vijijini ya 2005, ameamua kuivunja Bodi hiyo kwa kutengua uteuzi wa Mwenyekiti pamoja na Wajumbe wa Bodi.
Aliongeza kuwa, Bodi nyingine mpya itaundwa baadaye kwa mujibu wa Sheria ya Nishati Vijijini ya mwaka 2005. Bodi hiyo ilizinduliwa mwezi Aprili mwaka 2017 na ina wajumbe Saba.
Monday, November 12, 2018
KARIBU TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA
KARIBU TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA
Popular Posts
-
Kiongozi wa chama cha upinzani cha Forum for Democratic Change (FDC) nchini Uganda Kizza Besigye amekamatwa tena na maafisa wa polisi. ...
-
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza Kikao cha Kamati ya Pamoja ya Serikali ya Jamhuri ya...
-
Na Debora Charles (Mtakwimu) Sensa ya watu na makazi ni utaratibu wa kukusanya, kuchambua, kutathimini na kuchapisha na kusamba...
-
📌 Asema Rais, Dkt. Samia anafanya kazi kubwa ya kuwaunganisha Watanzaia 📌 Atak...
-
Mbunge Jimbo la Nyamagana Mhe Stanislaus Mabula kabla na baada ya ziara zake za mrejesho wa Bunge la bajeti kwa wananchi kila Kata, sasa ame...
Powered by Blogger.
0 comments:
Post a Comment