Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka amewataka wanafunzi wa kidato cha tano na sita shule ya sekondari Emanuel Nchimbi, kata ya Msamala Songea Mjini kusoma kwa bidii ili wapate ufaulu mzuri utakaowapa vigezo vya kujiunga na vyuo vya elimu ya juu pamoja na kupata mikopo ya elimu ya juu.
Rais Samia kupitia serikali anayoiongoza imetenga shilingi bilioni 985 kwa ajili ya uboreshaji wa mazingira ya vyuo vya elimu ya juu pamoja na kuongeza bilioni 70 kwenye bajeti ya mikopo ya elimu ya juu ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025 ibara ya 80."
Akiwa katika shule hiyo Shaka amesema CCM itachangia shilingi milioni 30 kwa ajili ya kukamilisha bwalo la chakula kwa wanafunzi huku Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini Mheshimiwa Dkt. Damas Ndumbaro ambaye pia ni Waziri wa maliasili na utalii aliunga mkono kwa kuchangia shilingi milioni 20 hivyo kupatikana Kiasi cha shilingi milioni 50 kitakachotosha kukamiilisha bwalo hilo.
Hatua hiyo ya CCM kuchangia ametokana na risala ya Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Mwalimu Stanley Mwasi wakati akiwasilisha taarifa ya maendeleo ya miundombinu ya ujenzi huo uku akiishukuru serikali kwa kutoa fedha zilizo endesha ujenzi wa bwalo hilo kwa kuwapatia shilingi Milioni MiaMoja ambapo mpaka sasa ujenzi huo umefikia Asilimia 95
Shaka amehitimisha ziara yake Songea Mjini ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa ziara ya Sekretarieti ya CCM Taifa inayoongozwa na Katibu Mkuu Ndg Daniel Chongolo katika mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma na Njombe.
0 comments:
Post a Comment