Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania
(JWTZ) linasikitika kutangaza kifo cha Brigedia Jenerali Albert
Costantino Frisch (mstaafu) kilichotokea tarehe 13 Aprili 2017.
Marehemu Brigedia Jenerali Albert
Costantino Frisch (mstaafu) alizaliwa tarehe 13 Novemba 1944, mtaa wa
Uhuru, Tarafa ya Kariakoo, Wilaya ya Ilala, Mkoa wa Dar es Salaam.
Alisoma na kuhitimu Shule ya Msingi mkoani Dar es Salaam na baadaye
kuendelea na masomo ya Sekondari katika Shule ya Sekondari St. Joseph
Convert School, Dar es Salaam hadi alipohitimu Kidato cha Nne mwaka,
1963.
Marehemu Brigedia Jenerali Albert
Costantino Frisch (mstaafu), alijiunga na JWTZ tarehe 07 Desemba 1964 na
kutunukiwa Kamisheni tarehe 22 Juni 1967. Alistaafu Utumishi Jeshini
kwa Heshima tarehe 30 Juni 1999.
Katika utumishi wake Marehemu alishika Nyadhifa mbalimbali Ikiwemo Mkaguzi Mkuu wa Jeshi Makao Makuu mpaka anastaafu.
Mwili wa Marehemu unatarajiwa kuagwa rasmi tarehe 20 Aprili 2017 katika Hospitali ya Jeshi Lugalo kuanzia saa 10:30 Asubuhi.
MUNGU AILAZE MAHALI PEMA PEPONI ROHO YA MAREHEMU
BRIGEDIA JENERALI ALBERT COSTANTINO FRISCH (MSTAAFU)
AMINA
Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P 9203, Dar es Salaam, Tanzania.
0 comments:
Post a Comment