METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, April 18, 2017

DC JUMA HOMERA ATIKISA TAMASHA LA UZINDUZI WA UMOJA WA MAKANISA TUNDURU YALIYO CHINI YA CCT

Na Mwandishi Wetu, Ruvuma

Ahimiza wananchi waendele kulinda Amani ya Nchi yetu na kuti sheria bila shuruti.

Aelezea Mradi wa Maji Mchangani unao gharimu shilingi Milioni mia tatu, unatarajiwa kuanza muda wowote kwanzia sasa.

Aelezea fursa ya soko Mpya ya Kisasa ya Mpunga linalo jengwa Nakayaya, linatarajiwa kukamilika Mwaka 2018.

Atoa onyo kwa vyama vya msingi vinavyo hujumu mfumo wa stakabadhi ghalani, asema ataendelea kuvichukulia hatua mfano mzuri ni chama cha Tingasam.

Ahaidi Shilingi laki mbili na kuomba wananchi wote washirikiane kwenye mambo ya maendeleo bila kujali tofauti za Dini, Kabila, Siasa n.k

Mwenyekiti wa  CCT Tunduru ahaidi Muungano wao  kushiriki ujenzi wa kituo cha Afya Nakayaya.

Mkuu wa wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Mhe. Juma Zuberi Homera, jana alihudhuria tamasha la uzinduzi wa Muungano wa makanisa yaliyo chini ya Christian Council of Tanzania (CCT). Tamasha hilo lilifanyika katika eneo la Kanisa la Bibilia Tunduru iliyopo karibu na uwanja wa ndege wa zamani.

Makanisa yaliyo shiriki tamasha hilo ni Kanisa la Bibilia Tunduru, Kanisa la Kiinjili la kilutheri Tunduru, Moravian Tunduru, Anglican Tunduru, Kanisa la Upendo na Kristu Masihi n.k.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com