Vikosi vya usalama vyatumwa kwa wingi katika maeneo kulikofanyika msako, Aprili hii 18.
Watu wawili wenye msimamo mkali wanaotuhumiwa kuandaa mashambulizi
makubwa nchini Ufaransa wamekamatwa jumanne hii Aprili 18 katika mji wa
Marseille. Taarifa hii imethibitishwa na Waziri wa Mambo ya Ndani
Matthias Fekl baada ya kukamatwa kwa watu wawili wenye umri wa miaka 23
na 29.
Rais Francois Hollande amekaribisha hatua hiyo ya kukamatwa kwa watu hao.
Watu hao wawili wamekamatwa, siku tano
kabla ya duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais, shirika la habari la AFP
limearifu likinukuu vyanzo vilio karibu na uchunguzi.
Wawili hao "wanatuhumiwa kutaka kuchukua
hatua kutekeleza mashambulizi makali," chanzo kimoja kimesema.
Walikamatwa na maafisa wa usalama wa taifa kwa minajili ya uchunguzi kwa
kosa la kushirikiana na wahalifu wa kigaidi. Kesi hiyo imefunguliwa
mjini Paris.
Waziri wa Mambo ya Ndani amesema kuwa
washukiwa waliokamatwa walikuwa na mpango wa kufanya mashambulizi
"katika siku chache zijazo." Matthias Fekl pia amekumbusha kwamba polisi
50,000 watapelekwa kwa kila moja ya duru mbili za uchaguzi wa urais
mnamo tarehe 23 Aprili na 7 Mei
0 comments:
Post a Comment