Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu,
Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama
akiwasalimia wananchi wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipofungua
Maonyesho ya Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi ya Serikali kwenye uwanja wa
Uhuru mjini Dodoma Aprili 18, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi
Mkurugenzi wa manispaa ya Dodoma, Bw. Godwin Kunambi (wapili kushoto)
hundi ya Shilingi 1, 469, 358,0 00/= kwa ajili ya vijana kabla ya
kufungua maonyesho ya Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi ya Serikali kwenye
uwanja wa mashujaa mjini Dodoma Aprili 18, 2017. Wanne kushoto ni Wziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na
Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama na kulia ni Naibu Wziri wake, Anthony
Mavunde. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini , Christina Mndeme na
watatu kushoto ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa wa Uwezeshaji
Wananchi Kiuchumi, Beng Issa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi
Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Mawasiliano wa Benki ya TPB, Noves
Moses (kulia) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo, Sabasaba Moshingi (
wapili kulia) cheti maalum cha kushiriki Maonyesho ya Mifuko ya
Uwezeshaji Wananchi ya Serikali kabla ya kufungu maonyesho hayo kwenye
uwanja wa Mashujaa mjni Dodoma Aprili 18, 2017. Kushoto ni Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu Jenista Mhagama. (picha na Ofiai ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akisalimiana na Mzee Maarufu wa Dodoma, Job Lusinde baada ya kufungua
maonyesho ya Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi ya serikali kwenye uwanja wa
Mashujaa mjini Dodoma Aprili 18, 2017. Wengine pichani kutoka kulia ni
Waziri wan chi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, AjiraKazi, Jijana,
ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini,
Christina Mndeme na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji
Wananchi Kiuchumi, Beng Issa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa
katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi walioshiriki katika
maonyesho ya Mifuko ya Uwezesha Wananchi ya serikali baada ya kufungua
maonyesho hayo kwenye Uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma Aprili 18, 2017.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa
katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi walioshiriki katika
maonyesho ya Mifuko ya Uwezesha Wananchi ya serikali baada ya kufungua
maonyesho hayo kwenye Uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma Aprili 18, 2017.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi
Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Mawasiliano wa Benki ya TPB, Noves
Moses (kulia) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo, Sabasaba Moshingi (
wapili kulia) cheti maalum cha kushiriki Maonyesho ya Mifuko ya
Uwezeshaji Wananchi ya Serikali kabla ya kufungu maonyesho hayo kwenye
uwanja wa Mashujaa mjni Dodoma Aprili 18, 2017. (Picha na Ofiai ya
Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Meneja wa PPF wa Kanda ya Mashariki na Kati, Bw. Michael Christian cheti maalum cha kushiriki Maonyesho ya Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi ya Serikali kabla ya kufungu maonyesho hayo kwenye uwanja wa Mashujaa mjni Dodoma Aprili 18, 2017. (Picha na Ofiai ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikilza
Bi. Evelyne Mandenje amabaye ni mmoja wa wajasiriamali walionufaika na
mikopo inayotolewa na Benki ya TIB wakati alipotembelea banda la
wasindikaji vyakula kabla ya kufungua Maonyesho ya Mifuko ya Uwezeshaji
Wananchi ya Serikali kwenye uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma Aprili 18,
2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akisalimiana na watumishi wa Benki ya Posta Tanzania (TPB) wakati
alipotembelea banda la benki hiyo kwenye maonyesho ya Mifuko ya
Uwezeshaji Wananchi ya Serikali aliyoyafungua kwenye uwanja wa Mashujaa
mjni Dodoma Aprili 18, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu, Jenista Mhagama wakijadili jambo katika maonyesho ya Mifuko
ya Uwezeshaji Wananchi ya Serikali yaliyofunguliwa na Waziri Mkuu
kwenye uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma Aprili 28, 2017. Kulia ni Afisa
Mwandamizi wa Fedha wa Benki ya TIB, Kenneth Lusesa(Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amelitaka
Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), lianze kufanya tathmini
ya kisayansi kuhusu manufaa ya Mifuko yote ya uwekezaji nchini ili
kujiridhisha endapo inawanufaisha wananchi kama ilivyokusudiwa.
Pia amelitaka baraza hilo lifanye
tathmini kuhusu namna ya kuunganisha mifuko hiyo bila ya kuathiri
majukumu ya msingi na mantiki ya kuanzishwa kwake, ili inayofanya kazi
zinazofanana iunganishwe .
Ametoa agizo hilo leo (Jumanne, Aprili
18, 2017) wakati akifungua maonesho ya mifuko ya uwezeshaji katika
uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma. Amesema uzinduzi wa maonesho hayo ni
fursa nzuri kwa wananchi kuweza kudadisi kuhusu huduma zitolewazo na
Mifuko hiyo na kutoa ushauri, ili kuboresha huduma.
“Lengo ni kuwa na Mifuko michache,
lakini inayobadilisha maisha ya wanufaika, ambao ni wananchi. Nitafurahi
kupata taarifa hiyo kabla au ifikapo Mwezi Mei, 2018,” amesema.
Aidha, Waziri Mkuu amesema mapambano
dhidi ya rushwa na ufisadi yanayofanywa na Serikali yanalenga
kuwawezesha Watanzania wengi wafanye shughuli za kujiongezea kipato
bila kusumbuliwa na baadhi ya Watumishi wasio waadilifu.
Ameongeza kuwa “uwezeshaji wananchi
kiuchumi ni jambo ambalo lipo kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka
2015, Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025; Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa
Miaka Mitano 2016/2017 – 2020/2021,”.
Amesema kuwawezesha wananchi kiuchumi,
sio ubaguzi wala upendeleo, bali ni jitihada za makusudi za
kuwashirikisha wananchi walio wengi ambao kwa sababu za kihistoria,
wamejikuta wakiwa nje ya mfumo rasmi wa kiuchumi, hivyo kubaki kwenye
hali duni jambo ambalo ni hatari kwa ustawi na usalama wa nchi.
Waziri Mkuu amesema jitihada za
uwezeshaji wananchi kiuchumi zilizoanza tangu Serikali ya Awamu ya
Kwanza na kuendelezwa na awamu zote zilizofuata, ambapo kwa sasa kuna
mifuko 19 ya kuwezesha wananchi kiuchumi.
Amesema mifuko hiyo imesaidia
upatikanaji wa mitaji kwa wajasiriamali na kupunguza kiwango cha
umaskini nchini. “Hadi kufikia mwaka 2016 Mifuko hiyo kwa pamoja ilikuwa
imetoa mikopo yenye thamani ya sh. trilioni 1.759 kwa wajasiriamali
400,000.
Awali Katibu Mtendaji wa NEEC, Bi. Beng`
Issa alisema maonesho hayo ya siku nne yatawezesha kuwaongezea wananchi
uelewa juu ya shughuli zinazofanywa na mifuko ya uwezeshaji.
Amesema kati ya mifuko 19 ya uwezeshaji
mifuko 13 imeweza kushiriki katika maonesho hayo ya kwanza kufanyika
nchini, ambapo kauli mbiu ya maonesho hayo ni “Wezesha wananchi kiuchumi
ili kujenga uchumi wa kati na Tanzania ya viwanda”
Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB Bank
PLC, Bw. Sabasaba Moshingi aliyezungumza kwa niaba ya washiriki alisema
madhumuni ya maonesho hayo ni kukuza uelewa juu ya uwepo wa mifuko ya
kuwezesha wananchi kiuchumi na fursa zitolewazo na mifuko hiyo.
Pia kuhamasisha wananchi juu ya
kujijengea utamaduni wa kujiwekea akiba na kuwekeza katika miradi yenye
kuleta faida pamoja na uanzishwaji na uimarishwaji wa vikundi na miradi
ya kiuchumi ili kuunganisha wananchi na fursa za huduma ya mikopo,
mafunzo na huduma nyingine zinazotolewa na mifuko hiyo.
0 comments:
Post a Comment