Rais wa Marekani Donald Trump amesema
anapongza uamuzi wa Vladimir Putin kuisaidia Marekani kuokoa fedha
ilizokua ikitumia kwa afisi zake nchini Urusi.
Rais wa Marekani Donald Trump amepongeza uamuzi wa Rais wa Urusi
Vladimir Putin wa kuwafukuza wafanyakazi 755 wa afisi za balozi za
Marekani nchini Urusi.
Hivi karibuni Rais Putin aaliagiza
kuondoka wafanyakazi 755 kutoka afisi za kibalozi za Marekani nchini
Urusi, akilipiza kisasi hatua ya Marekani kuiwekea Urisi vikwazo zaidi.
Bw Putin alisema wafanyakazi wao
walitakiwa kuondoka kufikia tarehe 1 Septemba, na kufikisha idadi ya
wafanyakazi katika afisi za kibalozi wa Marekani hadi 455, sawa na
wafanyakazi wa kibalozi wa Urusi walio Washington.
Katika mkutano na waandishi wa habari
mjini New Jersey, Rais Donal Trump amesema anapongza uamuzi wa Vladimir
Putin kuisaidia Marekani kuokoa fedha ilizokua ikitumia kwa afisi zake
nchini Urusi.
Hata hivyo uchunguzi unaendelea nchini
Marekani kuhusu madai ya Urusi kuingilia Uchaguzi Mkuu wa Marekani wa
mwaka 2016, licha ya Trump kushtumu uchunguzi huo.
Chanzo:RFI
0 comments:
Post a Comment