fisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya
Usambazaji Maji Jijini Dar es Salaam (DAWASCO) Mhandisi Cyprian Luhemeja
(kushoto) akimkaribisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji
Prof. Kitila Mkumbo wakati alipotembelea kampuni hiyo mapema hii
jana jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya
Usambazaji Maji Jijini Dar es Salaam (DAWASCO) Mhandisi Cyprian Luhemeja
(kulia) akimtembeza Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof.
Kitila Mkumbo katika baadhi ya ofisi za kampuni hiyo wakati
alipotembelea kampuni hiyo mapema hii jana jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya
Usambazaji Maji Jijini Dar es Salaam (DAWASCO) Mhandisi Cyprian Luhemeja
(kushoto)akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na
Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo wakati alipotembelea kampuni hiyo mapema
hii jana jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya
Usambazaji Maji Jijini Dar es Salaam (DAWASCO) Mhandisi Cyprian Luhemeja
(kulia) akieleza kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof.
Kitila Mkumbo, mipango na mikakati ya kampuni hiyo katika kutatua
changamoto za upatikanaji wa maji safi na salama katika jiji la Dar es
Salaam wakati Katibu Mkuu alipotembelea kampuni hiyo mapema hii
jana jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya watumishi wa Kampuni ya
Usambazaji Maji Jijini Dar es Salaam (DAWASCO)pamoja na watumishi wa
Mamlaka ya Maji Safi na Maji taka Jijini Dar es Salaam (DAWASA)
wakifuatilia kikao cha Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji
Prof. Kitila Mkumbo wakati alipowatembelea mapema hii jana jijini Dar es
Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji
Safi na Maji taka Jijini Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Archad
Mutalemwa (kulia) akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na
Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo (kushoto) wakati Katibu Mkuu alipokutana
na watedaji wa Kampuni ya Usambazaji Maji Jijini Dar es Salaam
(DAWASCO) pamoja na watumishi wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji taka
Jijini Dar es Salaam (DAWASA), katikati ni Afisa Mtendaji Mkuu wa
Kampuni ya Usambazaji Maji Jijini Dar es Salaam (DAWASCO) Mhandisi
Cyprian Luhemeja.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na
Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo (kushoto) akizungumza na watendaji wa
Kampuni ya Usambazaji Maji Jijini Dar es Salaam (DAWASCO) pamoja na
watumishi wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji taka Jijini Dar es Salaam
(DAWASA) wakati alipowatembelea mapema hii jana katika Ofisi za DAWASCO
jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Eliphace Marwa – Maelezo)
Na: Frank Shija – MAELEZO
Kampuni ya Usambazaji wa Maji Dar es
Salaam (DAWASCO) pamoja na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es
Salaam (DAWASA) zatakiwa kuongeza kasi ya usambazaji kwa wananchi ili
kufikia malengo ya Serikali katika kuwatumikia wananchi wake kwa kuwapa
huduma za msingi.
Wito huo umetolewa na Katibu Mkuu wa
Wizara ya Maji na Umwagiliaji Profesa Kitila Mkumbo wakati akiongea na
Menejimenti ya Mamlaka hizo leo Jijini Dar es Salaam.
Profesa Kitila amesema kuwa licha ya
ongezeko la upatikanaji wa maji, ipo vhangamoto ya idadi kubwa ya
wananchi kutofikiwa na huduma hivyo hivyo ni lazima sasa Mamlaka husika
kuongeza kasi ya usambazaji wa miundombinu ya maji katika maeneo ambayo
bado hayajafikiwa.
“Pamoja na kazi nzuri mnayofanya ya
kuhakikisha upatikanaji wa maji hakikisheni mnaongeza kasi ya usambazaji
wa huduma hii muhimu kwa wananchi, kwakufanya hivyo mtakuwa mnatendea
haki dhana ya kuwa mnaongoza kwa mapato lakini pia mnatoa huduma stahiki
kwa wananchi,” alisema Profesa Kitila.
Aidha Profesa Kitila ametoa rai kwa
wateja wote wa Dawasco na Dawasa zikiwemo taasisi za umma kutii agizo la
Mhe. Rais kwa kulipia huduma wanazopatiwa ili kuziwesha mamlaka hizo
kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa
Kampuni ya Usambazaji wa Maji Dar es Salaam (DAWASCO) Mhandisi Cyprian
Luhemeja amesema kuwa katika kuhakikisha uzalishaji wa maji umeongezeka
kwa kutoka lita za ujazo wa mita 160 Milioni kwa siku hadi kufikia lita
za ujazo mita 271Milioni kwa siku ambazo ni sawa na asilimia 100.37% ya
lengo la upatikanaji wa maji ambalo ni lita 270 Milioni kwa siku.
Mhandisi Luhemeja aliongeza kuwa jumla
ya Vizimba 560 (Gati za kuuzia maji) vimeunganishwa kwa ajili ya
kuwahudumia wananchi ikiwa ni muendelezo wa kuongeza kasi ya usambazaji
na upatikanaji wa huduma ya maji miongoni mwa jamii.
Katika hatua nyingine Afisa Mtendaji
Mkuu huyo amesema kuwa katika kutekeleza agizo la Mhe. Rais Dkt. John
Pombe Magufuli la kuhakikisha wanakina mama wanatua ndoo za maji
kichwani Dawasco inatarajia kuanza utekelezaji wa mradi wa kuongeza
usambazaji wa huduma ya maji katika eneo la takribani 1,427Km
unaohusisha maeneo ya Tegeta, Mpiji hadi Bagamoyo ifikapo mwezi Julai
mwaka huu ambapo tayari fedha Tsh. 117Bilioni kwa ajili ya mradi huo
zimepatikana kupitia Benki ya Dunia.Mradi huo utakapokamilika
unakadiriwa kuongeza idadi ya watumiaji wa maji takribani laki moja.
Katika kuhakikisha inafikia azma ya
kuongeza kasi ya usambazaji wa huduma ya maji kwa wananchi Dawasco
inaendesha Kampeni ijulikanayo “Mama Tua Ndoo ya Maji Kichwani Ndani ya
Siku 90” ikiwa na lengo la kuwaunganisha na huduma ya maji wateja
takribani 151,000 wataunganishwa na huduma hiyo katika eneo linalopakana
na Barabara ya Morogoro. Kampeni hiyo imeanza kuanzia tarehe 1 Aprili
hadi 30 Juni, 2017.
0 comments:
Post a Comment